Mgaza Othman: Wanaotetea Muungano wa mkataba wana ajenda ya siri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgaza Othman: Wanaotetea Muungano wa mkataba wana ajenda ya siri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Aug 9, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Na Mwinyi Sadallah | Nipashe | 9th August 2012

  Mwanasiasa mkongwe Zanzibar, Mgaza Othman Mgaza, amesema viongozi wanaotetea Muungano wa mkataba kuzingatiwa katika mabadiliko ya Katiba mpya, wana ajenda ya siri ya kutaka kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Mgaza aliyasema hayo jana katika mahojiano maalum na NIPASHE nyumbani kwake Kisauni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Alisema iwapo marekebisho ya Katiba yatazingatia hoja hiyo, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utavunjika na kubakia historia yake.

  "Nashaanga sana kuona viongozi wanatetea Muungano wa mkataba wakati mfumo huo kama itakubalika, Muungano utakufa na kubakia historia yake," alisisitiza.

  Alisema wananchi wa Zanzibar lazima watumie busara na hekima kabla ya kuamua kuunga mkono hoja za kuvunja Muungano huo.

  "Muungano kama unavunjika kila upande raia wake watalazimika kuondoka, jambo ambalo litaleta athari kubwa kwa wananchi wa pande mbili," alisema.

  Alisema kitendo cha Zanzibar kuwa na bendera yake na kiti Umoja wa Mataifa chini ya muundo wa Muungano wa mkataba, sawa na kuuvunja Muungano wenyewe.

  Mgaza alisema kama kuna viongozi wa chama na serikali Zanzibar wanaafiki mfumo wa Muungano wa mkataba, hakuna sababu ya Muungano wa Tanganyika kuendelea kuwepo nchini. Alisema kitendo cha Zanzibar kuwa na kiti chake Umoja wa Mataifa na bendera, sawa na kuvunja Muungano wenyewe. Mgaza ambaye aliwahi kuwa mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano kupitia cha cha TLP 2010, alisema wananchi lazima wawe makini na kampeni zinazoendelea kufanyika za kutaka Zanzibar kujitenga katika Muungano.

  "Wazanzibari lazima tutumie busara na hekima kabla ya kuamua kuvunja Muungano, sisi ndiyo tutaumia na nje ya Muungano suala la Upemba na Unguja litaibuka tu," alisema.

  Aidha, alisema Wazanzibari wengi wamenufaika na ardhi Tanzania bara pamoja na kutumia soko la biashara la watu milioni 40 na kupata mafanikio makubwa katika sekta ya biashara. Kadhalika, alisema vijana wengi Zanzibar wamekuwa wakinufaika na ajira kupitia Vikosi vya Ulinzi na Usalama mbali na masomo ya elimu ya juu kila mwaka. Mgaza alisema kwamba pamoja na wananchi wa Pemba kuwa ni watu wanaonufaika kwa kiwango kikubwa na fursa za Muungano, bahati mbaya ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kupinga Muungano.

  "Ajabu watu ambao wananufaika na Muungano ndiyo wanaokuwa mstari wa mbele kuupinga," alisema.

  Aliongeza kuwa kampeni za kuvunja Muungano zinazoendelea na baadhi ya viongozi katika Chama na Serikali Zanzibar kunatokana na kuweka maslahi binafsi mbele badala ya maslahi ya Taifa. Pia alisema mfumo wa serikali mbili ndiyo mwafaka katika kulinda Muungano isipokuwa Rais wa Zanzibar awe Makamu wa Pili Rais katika itifaki ya Tanzania.
   
 2. p

  pedeshee makambo Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uvunjike tu maana wazanzibari wananufaika sana kuliko watanganyika.:israel::yawn:
   
 3. jamesbond007

  jamesbond007 Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe unazani watanganyika walioko zenj, wanapenda kuiona zanzibar ikawa huru? kiasi aseme hayo ila tunawatoa hofu watanganyika wote waishio zenj, cc shida yetu ni zanzibar huru sasa hatuna wala hatutasubutu kumfukuza mtu yyte zanzibar kwakuwa yy si mzanzibar ila sheria za kimataifa zifuatwe tu!
  tuachiwe tupumuwe! halas, urembo mwengine baadae:yawn:
   
 4. nambokola

  nambokola JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 299
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kabisa Mkuu si walikuwepo kabla ya uhuru na wataendelea kuwepo tuu na wazanzibari walikuwepo tanganyika kbla ya uhuru na wataendelea kuwepo eti tukigawana mbao inabidi wananchi warudi makwao hawa viongozi wanaoongea wanajua sheria lakini ama wanaongea pumba tuu kwa maslahi yao binafsi
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,111
  Trophy Points: 280
  ..kama nia yao ni kuuvunja muungano, basi mimi kama Mtanganyika nawaunga mkono!!

  ..LET ZANZIBAR GO!!!
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Na Ukivunjika itawasaidia kutosafiri kuja bara; itawabidi wawe na passport; na walio Dar Wazanzi-bara itabidi waondoke

  na ni wengi sawasawa na population ya Zanzibar ni 300,000...

  Wengi wao Ardhi zao ni nzuri labda hapo ndipo nitakapogawiwa...
   
 7. m

  mkataba Senior Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo ni mwanasiasa uchwara
   
Loading...