Mgaya ang'ara mbele ya Kikwete. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgaya ang'ara mbele ya Kikwete.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kasyabone tall, Oct 6, 2010.

 1. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  NAIBU katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) Nicolaus Mgaya jana alikuwa kivutio kikubwa mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati aliposhangiliwa kwa muda wa zaidi ya dakika kumi baada ya kutambulishwa ili asalimie walimu.

  Mgaya alikuwa akitambulishwa katika maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani ambayo yalifanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea na kuhudhuriwa na walimu wengi na wananchi wengine.

  Mgaya alitambulishwa na katibu mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Yahya Msulwa ambaye alimtaka asimame na kuwasalimia wananchi pamoja na walimu.

  Baada ya Mgaya kuitwa, alisimama na kushangiliwa kwa zaidi ya dakika kumi na maelfu ya walimu waliokuwepo uwanjani hapo, huku wakimuita mkombozi na mtetezi wao mkubwa.

  Pamoja na kuwa naibu katibu mkuu, Mgaya ndiye aliyeonekana kuwa mstari wa mbele kufanikisha mgomo wa wafanyakazi wote uliopangwa kufanyika Mei 5, lakini haukufanyika baada ya Rais Kikwete kutoa onyo dhidi ya mfanyakazi ambaye angeshiriki.

  Wakati akihutubia wazee wa Dar es salaam kuhusu mgomo huo ambao ungefanyika katika kipindi ambacho nchi ilikuwa ikiandaa mkutano mkubwa wa kimataifa wa kiuchumi, Kikwete alikuwa akitaja jina la Mgaya mara kwa mara kwenye hotuba yake

  Tucta iliitisha mgomo huo kuishinikiza serikali kushughulikia madai yao ya muda mrefu, ikiwa ni pamoja na kuongeza kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi wa sekta ya umma, kuboresha kiwango cha pensheni na ufanisi wa mabaraza ya wafanyakazi.

  Akizungumza baada ya utambulisho huo, Msulwa alisema ukombozi wowote unaanzia kwa walimu hivyo ni vema serikali ikaona umuhimu wa kuboreshewa maslahi yao na kuusifu utawala wa Rais Kikwete kuwa umejitahidi kuboresha maslahi ya walimu na kutenga Sh73 bilioni kulipa madeni yao katika kipindi cha 2008 -2010.

  CWT iliitisha mgomo mwaka 2008 ikiishinikiza serikali kulipa malimbikizo yao ya muda mrefu, kupandishwa daraja, kulipwa posho za nauli na fedha za uhamisho, lakini siku moja kabla, serikali ilikwenda Mahakama ya Kazi ambayo ilitoa uamuzi wa kuzuia mgomo huo usiku.

  Msulwa alisema bado kuna matatizo mengi ambayo yanawakabili walimu, ukiwemo upungufu wa nyumba za walimu 181,440 na kuwa hali ni mbaya zaidi vijijini ambapo hakuna nyumba za kupanga hivyo kuwasababishia walimu kuishi katika mazingira magumu.

  Aliyataja matatizo mengine ya walimu kuwa ni pamoja na kutolipwa malimbikizo yao ya mshahara, fedha za uhamisho, matibabu pamoja na posho za kufundishia na kuiomba serikali iwaharakishie.

  Akihutubia mkutano huo, Rais Kikwete alisema amesikia matatizo yanayowakabili walimu na ameahidi kuwa atayafanyia kazi yote, ikiwa ni pamoja na na kuboresha zaidi maslahi ya walimu na kuwataka wafanye kazi kwa bidii ili kuinua kiwango cha elimu nchini.

  Kikwete aliwahimiza walimu kujiunga na vyama vya akiba na mikopo ili kupunguza makali ya maisha na kuwa Saccos ndiyo mkombozi pekee katika kusaidia namna ya kuendesha maisha ya kila siku.

  Alisema pamoja na mapungufu yaliyopo, shule za kata zimefanikiwa kujenga usawa kati ya wanafunzi wanaojiunga na masomo ya sekondari tofauti na miaka ya nyuma wakati hali ilipokuwa mbaya. Alisema ili kutatua tatizo la upungufu wa walimu, serikali itakuwa ikiajiri walimu 24,000 kila mwaka.

  Rais Kikwete alisema baadhi ya watendaji kwenye halmashauri za miji , manispaa na wilaya hapa nchini wamekuwa wakifanya ubabaishaji katika kushugulikia madai ya walimu na amemuagiza katibu mkuu wa Utumishi kushugulikia madai yao ya mshahara, likizo, matibabu pamoja posho ya kufundishia.

  Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe aligeuza mkutano huo kuwa uwanja wa kampeni wakati alipopewa nafasi ya kuzungumza. Baada ya kupewa nafasi ya kusalimu, Prof Maghembe alimpigia debe Kikwete na kuwataka walimu wamuongezee miaka zaidi ili aweze kuleta mafanikio kwenye sekta ya elimu.

  Alisema Tanzania imefanikiwa kimataifa katika nyanja ya elimu na hadi sasa imefanikiwa kuwa na sekondari nyingi zaidi, vyuo vya ualimu pamoja na vyuo vikuu na serilikali imejipanga kutumia teknolojia ya mawasiliano kufundishia katika mradi wake ujulikanao kama "Beyond Tommorow."
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Waalimu chonde chonde, tusirudie makosa ya kumpa HAYAWANI kura zetu.
  Shime tuungane kuondoa utawala wa kidhalimu ili kuboresha hali zetu za kiuchumi na kuboresha mazingira yetu ya kufanyia.
  TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA.
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Kama bado wanaamini uwalimu ni wito, then JK ni mtu wao. Ila naamini JK kafungua mkutano akiondoka ndiyo mchakato wa chinichini utakapoanza. Nafikiri Mgaya atkuwa na nafasi ya kuzungumza na kuwambia walimu kuwa wachague kiongozi atakayewajali.
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  duu kweli kazi ipo mwaka ulee si aliahidi kujenga nyumba za walimu alijenga ngapi na wapi!? Tunaweza kupata pic ya nyumba hizo.
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Aminia Mgaya
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,957
  Likes Received: 23,634
  Trophy Points: 280
  Duh! Unamaanisha nani hapo kiongozi? Mi simo!
   
 7. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  anazidi kumwaga ahadi wakati wakati ule wa mika 5 iliyopita hakuna liyoitekeleza hadi ikawa inatolewa kwenye matangazo na asasi za kiraia, huyu jamaa bana, anapenda madaraka wakati utekelezaji wake ni zero
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  JK ni lazima anamwonea gere Mgaya angelitamani waalimu wampe sifa hizo walizomwagia mwenzie.

  JK ni vyema akafahamu kuwa atavuna alichopanda na wala siyo vinginevyo.
   
Loading...