Mgawo wa fedha: Ngeleja na Malima walikatiwa kitu kidogo toka makusanyo ya Jairo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgawo wa fedha: Ngeleja na Malima walikatiwa kitu kidogo toka makusanyo ya Jairo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gobret, Aug 16, 2011.

 1. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  • WADAIWA KUPATA MGAWO WA SH 4 MILIONI KILA MMOJA KUTOKA FEDHA ZILIZOKUSANYWA NA JAIRO
  15, Agosti 2011

  TUHUMA zilizosababisha kupelekwa likizo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo zimezidi kupanuka na sasa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima wanadaiwa kupokea sehemu ya fedha zilizosababisha mtendaji huyo kupewa likizo ili kupisha uchunguzi dhidi yake.

  Jairo yupo likizo baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kuanzisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa bungeni kwamba aliwaandikia barua wakuu wa idara chini ya wizara yake ili watoe fedha kusaidia kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo, fedha ambazo zinatafsiriwa kwamba zililenga kuwahonga wabunge.

  Lakini wakati umma wa Watanzania ukisubiri hatima ya Jairo huku suala lake likiwa bado halijafikia mwisho, imebainika kuwa Ngeleja na Malima kila mmoja alinufaika na mgawo wa fedha hizo kwa kila mmoja kupewa kiasi cha Sh4 milioni, kwa maelezo kwamba ni fedha za kuwakirimu wageni.

  Imeelezwa kuwa kiasi cha fedha kilichokusanywa na Jairo na kuingizwa katika akaunti ya Tanzania Geological Survey (GST), namba 5051000068 kwenye Benki ya NMB, Tawi la Dodoma ni Sh460 milioni na siyo bilioni moja kama ilivyodaiwa awali.

  Hesabu kwamba fedha hizo zingefikia Sh1 bilioni ilitokana na barua iliyosomwa bungeni na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ambayo ilikuwa ikibainisha kwamba fedha zilizoombwa ni Sh50 milioni, ambazo zikizidishwa kwa idadi ya idara na taasisi 21 zilizopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zinaleta jumla hiyo ya kiasi cha fedha.

  Mwandishi wa gazeti hili aliona dokezo la Julai 16, mwaka huu la Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Nishati na Madini aliyefahamika kwa jina la I.H. Swai kwenda kwa Jairo likipendekeza kwamba Waziri na Naibu wake wapewe kila mmoja kiasi cha Sh4 milioni kwa ajili ya kuwakirimu wageni: "Hasa katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti."

  Dokezo hilo lilisema: "Kulingana na uzito wa kazi za Wahe. Waziri na Naibu Waziri, nashauri wapewe entertainment allowance ya Sh4 milioni kila mmoja, ili kuwawezesha kubalishana mawazo/kushauriana na wadau muhimu na wananchi wa majimbo yao, wanaofika Dodoma kuwaona kwa masuala mbalimbali ya maendeleo ya majimbo yao, katika kipindi hiki cha Bunge la bajeti."

  Dokezo hilo liliidhinishwa na Katibu Mkuu, Jairo Julai 18, 2011 kwa kuandika neno "Sawa" kisha kulisaini ikiwa ni kukubaliana na mapendekezo ya Swai na siku hiyo fedha hizo kiasi cha Sh8 milioni kililipwa kwa wahusika.

  Hata hivyo, maelezo ya dokezo hilo yanatofautiana na yale yaliyo kwenye fomu iliyotumika kwa ajili ya kufanya malipo hayo ambayo inasomeka "Fomu ya Malipo ya Entertainment Allowance kwa ajili ya wajumbe kuwezesha uwasilishaji wa hotuba ya bajeti kwa mwaka 2011/12."

  Chini ya kichwa hicho kuna neno tarehe........ ikiacha nafasi wazi kwa ajili ya kujaza tarehe ambayo malipo hayo yalifanyika na katika fomu ya malipo ya Ngeleja na Malima imeandikwa 18/7/2011.

  Kwa mujibu wa fomu hiyo ya malipo, waliochukua fedha hizo Julai 18, 2011 ni wawakilishi wa viongozi hao ambao mmoja ametakwa kwa jina moja la Massola kwa niaba ya Ngeleja na mwingine aliyefahamika kwa jina la E. Shija aliyesaini fedha hizo kwa niaba ya Malima. Msaidizi wa Waziri Ngeleja anaitwa Sosthenes Massola, wakati msaidizi wa Malima anajulikana kwa majina ya Emmanuel Shija.

  Julai 18, mwaka huu ni siku ambayo Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda iliamua kuiondoa bungeni Hotuba ya Bajeti ya Nishati na Madini baada ya wabunge karibu wote waliopata fursa ya kuchangia kukataa kuunga mkono, hadi iliporejeshwa bungeni Agosti, 13 mwaka huu na kupitishwa baada ya Serikali kuwasilisha mpango wa dharura wa kukabiliana na tatizo la umeme nchini.

  Bajeti ya wizara hiyo iliwasilishwa bungeni Ijumaa, Julai 15, 2011 na wabunge wengi waliopata nafasi ya kuchangia walieleza wazi kwamba hawako tayari kuiunga mkono kutokana na sababu mbalimbali zilizokuwa zikigusa sekta za madini na umeme.

  Taarifa za awali za kiuchunguzi zilidokeza kuwa siku moja baadaye (Jumamosi, Julai 16, 2011) na Jumatatu Julai 18, 2011 kilichukuliwa kiasi kikubwa cha fedha kutoka katika akaunti ya GST, hali iliyozua maswali kuhusu mtiririko huo wa utoaji wa fedha.

  Akaunti hiyo ndiyo iliyotumika kukusanya fedha kutoka katika taasisi mbalimbali zilizoko chini ya Wizara ya Madini kwa ajili ya kile kilichodaiwa kuwa ni kwa ajili ya kufanikisha uwasilishaji wa bajeti ya wizara bungeni.

  Uchukuaji wa fedha nyingi ulizua hoja na wasiwasi kwamba huenda madai kwamba hakukuwa na nia njema ya matumizi ya fedha hizo yalikuwa ya kweli.

  "Wachunguzi wetu wanajenga hoja hapa kwamba kwa nini fedha hizi nyingi zilichukuliwa Jumamosi baada ya mambo ya wizara kuonekana kuwa siyo mazuri siku iliyotangulia (Ijumaa)?," kilihoji chanzo chetu na kuongeza kuwa:

  "Hata hizi fedha nyingine zilizochukuliwa Jumatatu nazo zina walakini, lazima hapa tuchunguze kwa sababu kuna kitu ambacho siyo cha kawaida."

  Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, shughuli za kibajeti ni pamoja na posho za vikao (sitting allowance), posho za kujikimu (per diem), ununuzi wa vyakula na vinywaji na gharama za mafuta kwa magari ya watumishi hao.

  Ngeleja na Malima

  Ngeleja na Malima walipoulizwa kwa nyakati tofauti bungeni Dodoma jana kuhusu madai ya kupewa posho hizo, hawakuthibitisha wala kukanusha.

  Ngeleja kwa upande wake alisema asingeweza kuzungumzia suala hilo kwani kwa kufanya hivyo ni kama angekuwa "akijitetea" hivyo kutaka suala hilo aulizwe Mkurugenzi wa Mipango ya Wizara yake na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

  "Mimi nadhani uwaambie watu wenu wa Dar es Salaam waende pale kwa Mkurugenzi wa Mipango, pale ofisini kwetu ili waweze kupata maelezo, yeye (mkurugenzi) na mhasibu mkuu ndiyo wanaofahamu haya mambo ya posho," alisema Ngeleja.

  Kwa upande wake, Malima alisema suala la msingi ni gazeti hili kufutilia suala la posho za mawaziri na manaibu wao katika Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ili kubaini iwapo wao ndiyo waliolipwa fedha za aina hiyo tu au pia ni kwa mawaziri wengine.

  "Mimi nadhani mnatakiwa kuwauliza watu wa Utumishi ili wawaambie maana hapa tunapokuwa bungeni, kuna mambo mengi yanafanyika, sasa ni vizuri mkauliza ili mfahamu waziri na naibu wake ni stahili zipi wanazopaswa kupewa kama allowances (posho)," alisema Malima na kuongeza:

  "Maana mnapaswa mjue na muusaidie umma wa Watanzania katika haya mnayoyaandika, kwamba hata kama tulichukua posho hiyo msingi wake ni nini? Halafu jingine kwani ni sisi tu au ni utaratibu wa Serikali kwa mawaziri wake?"

  Mhasibu mkuu afafanua
  Akizungumzia suala hilo, Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo, Rose Waniha alisema kuna taratibu zinazotumika katika kutoa posho hizo za kujikimu kwa waziri, naibu na katibu mkuu wawapo katika shughuli maalumu hasa vikao vya Bunge.Waniha alisema kiutaratibu, wakuu wa idara huwa wanafahamu kiasi cha fedha hizo za kujikimu kutegemea aina ya kazi za kiofisi.

  "Kwa hiyo hata kunapokuwa na vikao bungeni mtu anayehusika anaangalia labda kila siku waziri au naibu anapaswa kupata kiasi gani cha fedha. Inawezekana ikawa Sh500,000 kwa ajili ya kukirimu wageni . Kwa hiyo hilo dokezo unalolizungumzia ninavyofahamu litakuwa ni la siku za vikao siyo siku mbili ndiyo zilipwe Sh4 milioni kwa mtu mmoja," alisema.

  Alipoulizwa kama kuna utaratibu rasmi wa kutoa fedha hizo za kukirimu wageni na viwango maalumu, alisema hakuna viwango maalumu vilivyomo katika dokezo lolote zaidi ya watu wa idara kuangalia uzito wa kazi na idadi ya wageni.

  Kuhusu posho ya siku ya kawaida, alisema kwa kawaida waziri, naibu au katibu mkuu anapokuwa safarini, posho ya siku ni Sh80,000 lakini ni tofauti na fedha hizo za kukirimu wageni.

  "Posho na fedha hizi za kukirimu wageni ni vitu viwili tofauti. Posho anazolipwa waziri au naibu ni Sh80,000 kama kawaida lakini pesa nyingine za kujikirimu hazina uhusiano na posho," alisema.


  -------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
  Kweli nchi hii tutafika? RAIS NAYE TUMEPATA ***** LA AINA YAKE. Kweli tz watu wanaifaidi. Mtasikia mengi sana. Subiri uone
   
 2. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hivi kweli kwa jinsi hii tutafika? Raisi wetu ndio hivyo, mtu wa kukata anga. Sijui kama kuna kitu kitafanyika bongo. Tutakoma miaka 10 hii. Ndio tujifunze kuchagua vizuri
   
 3. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  this country has gone to the dogs.
   
 4. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Gobret na huyu mwandishi wote hamna hoja unless mthibitishe hela hazijatoka wizarani bali kwenye account ya Geological Survey inayochunguzwa.
   
 5. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Subiri tu Bw Tomaso
   
 6. D

  Derimto JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Acheni makelele maana bajeti imeshapita na tayari mafuta yamepanda bei na kurudia pale yalipo na hakuna cha kufanya tumeyataka wenyewe!
   
 7. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hii inaitwa sensational jornalism mwandishi kajaribu kuunga vitu viwili bila ya kiunganishi,wala usikubaliane nami wasubiri wachambuzi asubuhi kama wataona connection.
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Probably at this time Nyerere is not sleeping at peace; he told Marando that I can not go and rest in Butiama peacefully while leaving the country in hands of dogs. Unfortunately he may have unwillingly done so by blocking Marando and his company.
   
 9. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Nimepita tu, na nimekasirishwa na mengi!
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Ati hakuna viwango kweli? Haiwezekani serikali iwe inaendeshwa bila utaratibu kiasi hicho. Yaani aachiwe mtu ndio aangalie kiasi gani unatakiwa kulipa? Huo si uhasibu wala taratibu za serikali.

  Hapa kuna dalili za mulungula, posho tata, matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi, hongo, rushwa, kujikimu kusiko na mashiko, ulevi wa madaraka, kutojua taratibu za kihasibu, kutojua taratibu za malipo ya serikali (standing orders and Government Circulars) na upofu wa kufikiri. Wazirudishe tu kwa heshima yao.

  Kumbe Ngeleja aliomba msamaha kinafiki huku akijua Jairo alifacilitate yeye kukunja hela ya matundu 100 ya vyoo vya shule!!
   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hiyo iliyotajwa hapo ni kidogo sana. Ni kiini macho tu. Ngeleja na Malima walichukua zaidi. Hii ni biashara kubwa ya wanasiasa wetu. Uwaziri unakuwa mtamu kwa ajili hii.
   
 12. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Viongozi wetu mmezidi Ulafi. Hivi hizi Pesa mbona hawa jamaa wanapeana tu, hivi maposho yote yale wanayopewa lakini bado wana pesa za kukirimu wageni! halafu wanatuambia kasungura kadogo wakati wao wanakula kote. Tutaendelea kunyonywa na huyu mkoloni mweusi 'gambas' mpaka lini!

  Mkuu wa nchi naona sasa ameamua liwalo na liwe, yeye kazi ni kuandaa futuru, kukaribisha wageni ikulu na kusaini vitabu vya maombolezo, rais wa ajabu kabisa. Pesa hizi za kukirimu wageni ndio zinamfanya awe na kiburi, nina imani siku moja utasema tu, ukiwa tense au relaxed, that day is around the corner.
   
 13. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Gobret na mwandishi wana hoaj nzio sana. Inatalkiwa kujulikana hizo Mil 4 walizolipwa Ngeleja na Malima zilikuwa ni za nini kama Mhasibu anathibitisha kiwango cha posho ni Shs 80,000/= kwa siku tu. Huu ndio ubadhirifu wenyewe wakati hospitali zetu hazina dawa, vituo vya polisi havina karatasi, shule hazina madwati, waalimu vitabu n.k. Na kuhusika moja kwa moja katika kukusanya fedha kwa ajili ya kuwahinga wabunge.
   
 14. MLATIE

  MLATIE Senior Member

  #14
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tuzidi kuiombea tanzania kwa kweli wamesubiri budget ya ngeleja ipite jumamos ewura wakapandisha bei.sasa sisi tunashindwa kuelewa kabisa gavana anasema shillingi yetu imeimarika ewura wanasema imedorora duh!Tanzania Nyerere amka baba uone nchi yako inavyoangamia.
   
 15. s

  smz JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa sasa ndo utajua nini maana ya "ukoo wa Kambare".

  Ewura naye siku hizi ana meno. Anasema bei inaanza kutumika mara moja.
  Ngeleja anasema inasubiri stock ijayo.

  Kwa kifupi hii nchi inaongozwa na wenye pesa, yaani wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wa mafuta. hailleti maana kama waligoma, mkawapiga mkwara kidogo na wengine kuwatishia kuwafungia leseni kwa siku 90, hadi wakurugenzi kufikishwa mahakamani. Hii yote danganya toto, hakuna chochote.

  Inawezekanaje ndani ya wiki hiyo hiyo bei ya mafuta imepanda na kurudi kule kule?? Nchi hii bwana!! we acha tu.!!
   
 16. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hahahaha halafu wanasimama bungeni na kusema jamani "Ka Sungura kenyewe kadogo"
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Tume iliyoundwa kumchunguza Jairo imeundwa na akina Ngeleja. Hapo unategema jibu la namna gani? Kazi ipo!
   
 18. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  bado kuna mengi yataibuka
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  umeme nao????
   
 20. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #20
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Unaona sasa fedha zetu zinatumika bila utaratibu, watu eti kwa sababu ni wakubwa wanajichukulia tuu, hakuna kuacaunt for. Nchi imekuwa bora liende, hivi wabunge hawawezi kuuliza matumizi ya wizara ni vipi????????? Kama matumizi yenyewe yako hivyo, hizo budget zinatumiwaje???????
  Kwahiyo matumizi ya fedha zetu hayana kipimo wala mipaka ni bora liende, nchi imekwisha hatuna pa kutokea ni mufilisi tuuuu!!!!!!
   
Loading...