Mgawanyo wa majukumu katika utendaji wa serikali - mwaziri na makatibu wakuu

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Katika utendaji wa serikali, ninavyoelewa, mawaziri majukumu yao ni uanasiasa zaidi ya utendaji maana wao kama political commisars wa wizara zao wanatakiwa kusimamia sera na ilani ya uchaguzi wa chama kilicho madarakani.Aidha shughuli zote za kiutendaji ziko chini ya Katibu Mkuu ambaye ndiye chief executive officer wa wizara husika.KM ndiye pia accounting officer kwa maana ya kuwa budget ya wizara na maidhinisho ya matumizi ya fedha au malipo anapaswa kusimamia na kuwajibika moja kwa moja.Kinachonitatiza au kunishinda kuelewa ni vipi mawaziri wamegeuka watendaji wakuu na kuwa na nguvu na usemi zaidi kwenye masuala ya kiufundi na wakati mwingine hata katika fedha hasa ukizingatia kuwa Mawaziri si lazima wawe wataalam wa masuala yanayoshughulikiwa na wizara hizo.Mara nyingi hii hupelekea migogoro na vita baridi kwenye mawizara baina ya mafahali hawa wawili.Wakati mwingine watendaji au technocrats kwenye wizara hujikuta wakiumia kutokana na migongano hii na kukosa hata morale wa kufanya kazi.Tuchukulie hili suala la matumizi mabaya ya madaraka lililopelekea mawaziri wawili kushtakiwa mahakamani, ingekuwa mgawanyo wa kazi na madaraka unaheshimiwa, mawaziri hawa wasingepata hiyo jeuri ya kutumia nafasi zao vibaya.Suali la kujiuliza ni je, serikali imepata fundisho lolote hapa na hivyo kuweka bayana majukumu, madaraka, mamalaka na uwajibikaji katika utendaji wake? Pengine ni wakati muafaka kujiuliza na kurekebisha kasoro zilizopo ili kuwakinga wengine wasijikute wanaishia keko.
 
Back
Top Bottom