Bernard bakari
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 407
- 781
Muundo huu wa utawala wa mgawanyo wa kimadaraka yaan separation of power uliibuliwa na Montesqueieu's katika kitabu chake cha The spirit of the law (1748) ambapo alisisitiza kuwepo kwa mihimili mitatu inayofanya kazi bila kuingiliwa na mhimili mwingine yaan mahakama, bunge na serikali ( execurive) mihimili hii haipaswi kuingiliana katika utendaji wake wa kazi lakini kwa nchi hii na serikali hii ya awamu ya tano kwa maoni yangu falsafa hii haipo tena bali serikali (Executive) wamekuwa wakionekana kutoa maelezo namna gani mamlaka nyingine inatakiwa ifanye kazi yake mfano Rais alitoa maelekezo namna ya kudeal na kesi ya mama aliyesema mjane huku akitambua ni kazi ambayo haipo chini ya mamlaka yake na kumwamuru jaji kiongozi kuchukua namba ya simu ya mjane huyo, kwa mara kadhaa bunge limekuwa likijadili mambo ambayo yapo mahakan huku wakijua hawaruhusiwi kufanya hivyo Tanzania inatakiwa ibadilikw iwe nchi inayoheshimu mamlaka ya mhimili mwingine vinginevyo shida wanasiasa ndo watakuwa wanashikilia haki za watu na tukifikia huko tunakoelekea nchi itakuwa ya mashaka na haitakuwa sehemu ya kujivunia kuishi tuenzi utawala wa mgawanyo wa madaraka