Mgawanyiko kati ya Wahutu na Watutsi waibuka jeshini Burundi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
Mgawanyiko kati ya Wahutu na Watutsi waibuka jeshini Burundi
Huku mzozo nchini Burundi ukizidi na kuwa katika hatari ya kuwa wa kikabila ,Rais Pierre Mkuzunziza wa Burundi ametisha kukabiliana na wanajeshi wa kusimamia amani wa Umoja wa Afrika.


Rais Pierre Nkurunziza amesema kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika ambacho kimependekezwa kitakiuka katiba ya Burundi ambayo inapinga uingiliaji wowote iwapo kuna serikali inayofanya kazi na hakuna vita kati ya pande mbili.

Rais huyo amesema Burundi itachukulia hatua hiyo kuwa ya uvamizi na ikiwa wanajeshi wa kigeni wataingia nchini humo,watawakabili.

Nkurunziza ambaye ni kutoka kabila la Hutu anaonekana kuwatenga maafisa kijeshi wa kitutsi ambao utiifu wao unatiliwa shaka.Baadhi ya Watusti wanaanza pia kuliasi jeshi na tayari kanali mmoja alitangaza kuunda kundi jipya la waasi wiki iliyopita.

Kuasi kwa Luteni huenda kukazidisha mzozo

Kuasi kwa Luteni kanali Edouard Nshimirima,kumeeneza uvumi kuwa wanajeshi wengine Watusti watamfuata,na kusababisha kuzidi kwa mzozo huo na umwagikaji mkubwa wa damu.

Serikali ya Burundi imelaumu Rwanda ambayo ina makabila sawa na Burundi na inayoongozwa na Rais Mtusi kwa kusajili na kutoa mafunzo kwa waasi wanaompinga Nkurunziza,madai ambayo serikali ya Rwanda imeyakanusha.Zaidi ya watu 800,000 kutoka kabila la Watsusi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawawa nchini Rwanda wakati wa mauwaji wa halaiki 1994.


Muandamanaji akiweka kizuizi wakati wa maandamano ya kumpinga Rais Nkurunziza

Mzozo wa sasa nchini Burundi ulizuka baada ya chama tawala CNDD-FDD kutangaza mwezi Aprili kuwa Nkurunziza awanie muhula wa tatu ,hatua ambayo waangalizi wengi walisema ilikiuka mikataba yote miwili ya amani iliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuwa kinyume pia cha katiba.Mtetezi mmoja maarufu wa haki za binadamu aliliambia shirika la habari la AP mgawanyiko mkubwa wa kikabila wa muda mrefu nchini Burundi ni changamoto kubwa inayoikabili tena nchi hiyo.

Baadhi ya wanachama wanakumbuka mauaji yaliyotokea

Anschaire Nikoyagize,Rais wa muungano wa mashirika ya haki za binadamu amesema wakati serikali madarakani ikihimiza juu ya maridhiano,baadhi ya wanachama wa chama tawala wanakumbuka mauaji yaliyotokea nchini Burundi mwaka 1972 na kukandamizwa wa watutsi walio wachache dhidi ya Wahutu walio wengi chini ya Serikali za kijeshi zilizotawala kati ya miaka ya 1960 na mwisho wa miaka ya 1980.

Jeshi la Burundi liliangaliwa kuwa ufanisi mkubwa wa ule mkataba wa amani wa Arusha wa 2000 kwa kuwaleta pamoja wanajeshi wa Kihutu na wale wa Tutsi na kuwa jeshi moja.

Kwa sasa ufanisi huo unaonekana kuvurugika kutokana na machafuko yamesababisha vifo vya watu 200 na kutishia kuchukua mkondo wa tafauti za kikabila.

Mwandishi:Bernard Maranga/AP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
Source.Mgawanyiko kati ya Wahutu na Watutsi waibuka jeshini Burundi | Matukio ya Afrika | DW.COM | 31.12.2015
 
Viongozi wengine ni majanga na mkosi mkubwa kwa mataifa yao - huyu Nkurunzinza ni balaa kwa Warundi. Mungu awasaidie
 
Nkurunzinza Hafai Kabisa, Lakini Kwa Kutojua Msuluhishaji wa Mgogoro Huu Ni Dictator M7 Ambaye Pia Anafuata Mkondo Ule Ule wa Nkrunzinza.

Africa Ni Majanga, Angalia Jeneral Kagame Nae Ni Yale yale... Duuuh!!!!
 
Mungu awape moyo na amani itawale kama la rais aachie ngazi otherwise he will regret kama maafa yatatokea makubwa zaidi
 
Ukabila na Udini ni hatari sana kwa ustawi wa nchi yoyote ile.

Nkurunziza akae chini aunganishe makabila yote.

Na vita vya kikabila vikitokea Burundi basi tutegemee na Rwanda vikatokea.

Kwasababu makabila haya yapo humo pia.
 
Huyu chizi Nkurunziza anataka wangapi wafe ndio aachie ngazi? angeachia tuu kuepusha disaster inayokuja mbeleni,sioni akitoboa huyu ataishia asipopataka soon
 
Huyu chizi Nkurunziza anataka wangapi wafe ndio aachie ngazi? angeachia tuu kuepusha disaster inayokuja mbeleni,sioni akitoboa huyu ataishia asipopataka soon
hivi kati ya shetani wako kagame na nkurunzisa, kuna tofauti gani? aliowaua nkurunziza ni wachache kuliko aliowaua kagame. hawa wote wapo katika chungu kimoja, ni majanga katika eneo hili la afrika mashariki.
 
Hizi nchi sijui wana laana!!
Mkuu nimejiuliza saana sure i support u, nchi hizi wana laana hata Afrika pia na waaarabu. Inaniuma sana Afrika yangu kuwa na viongozi wa design ya kina Nkurunzinza, watu wana kufa kila siku kisa wewe uwe kiongozi what such a shame to yu afrkani leaders? Hamna hata uwezo wa kuambiana ukweli pfuuuu i feel ashamed being an african.
 
Dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana ,Nyerere alisema dhambi hiyo ni kama kula nyama ya mtu ukianza hutoacha ,Watanzania tunawanyoshea Burundi na Rwanda vidole wakati wana siasa wetu wanaimba ubaguzi ,viongozi wa dini,wananchi wa kawaida,Mungu atuepushie mbali tu ,Nashindwa kuelewa kwanini Nkurunziza hataki kutumia busara tu ya kawaida japo siwezi mlaumu sana Nkurunziza kwa sababu hata hapa kwetu Shein pamoja na busara zake Zanzibar madaraka wamekataa kuyaachia ,
 
Last edited:
Yanayotokea Burundi haya na tofauti na yanayotokea Zanzibar tofauti iliyopo Zanzibar ni kwa kuwa wapinzani wameamua kuwa wapole.
Lakini wangeamua kuchukua mlengo wa machafuko hali ingekuwa mbaya.

Nchi za kiafrica zinafanana kama sio watawala kung'anag'ania madaraka,itakuwa vyama vya siasa haviko tayari kuachia nchi kwa vyama vingine na utawala mwingine.

Africa labda vizazi vijavyo.
 
kagame aache kuiingilia Burundi,mbona yeye kawa mtawala wa maisha Rwanda?why anamwonea wivu Nkurunzinza?Nkurunzinza hakuka kuachia madaraka endelea kudeal na hao vibaraka wa kagame
 
how dare you put your self in a moral position to judge others....."!! ya kwe2 Tz uko uzenjin yametushinda ya Burundi hayawahusu jar yenu
 
Tunastahili lawama kwa haya yanayoendelea huyu jamaa alikuwa hapa wkt wa mapinduz kwann tuliruhusu atoke na kujipenyeza tena burundi? Huyu tungemtuliza hapahapa saivi habari tungekuwa tunazungumza mengine
 
Tunastahili lawama kwa haya yanayoendelea huyu jamaa alikuwa hapa wkt wa mapinduz kwann tuliruhusu atoke na kujipenyeza tena burundi? Huyu tungemtuliza hapahapa saivi habari tungekuwa tunazungumza mengine
ah we kumbe haumjuwi mzee wa visasi aka mkwere! baada ya kupewa makavu kuhusu FDLR ndio njama za kitoto zilipoanza huku akichota pesa kutoka ufaransa kwa kupitia Membe, wakisaidizana na Nkurunziza kuivusha FDRL kutoka DRC nakuingizwa Burundi... lengo kubwa lilikuwa kutrain Imbonerakure kusudi waje kulazimisha warundi kumsikiliza Nkurumbi na baadaye kuja kuleta matatizo Rwanda... yani viongozi wasioona mbali ni tabu tupu... @jMali @Bukyanagandi @vyuma
 
kagame aache kuiingilia Burundi,mbona yeye kawa mtawala wa maisha Rwanda?why anamwonea wivu Nkurunzinza?Nkurunzinza hakuka kuachia madaraka endelea kudeal na hao vibaraka wa kagame

We inabidi ukapimwe akili inawezekana ipo robo we inaonyesha waona raha binadamu wenzako wanavyokufa kwaajili ya ulafi wa madaraka wa mtu mmoja.
 
Tunaiga mambo mengi sana toka kwa wazungu lkn tumeshindwa kuiga demokrasia, tuna nini sie lkn mbona tuna tia aibu
 
Mkuu nimejiuliza saana sure i support u, nchi hizi wana laana hata Afrika pia na waaarabu. Inaniuma sana Afrika yangu kuwa na viongozi wa design ya kina Nkurunzinza, watu wana kufa kila siku kisa wewe uwe kiongozi what such a shame to yu afrkani leaders? Hamna hata uwezo wa kuambiana ukweli pfuuuu i feel ashamed being an african.

Tatizo siyo hizo nchi. Tatizo nni watutsi. Nchi yoyote ikisha na watutsi hata 10% ujue ni shida. Ni watu wa ajabu sana. Nkurunziza hana tatizo sana kwani suala la muhula liko kisheria isipokuwa these blood thirsty tutsis wanachukua kisingizio hicho kuhalalalisha vurugu.

Lakini, nadhani hili suala la kinabii kwani kipigo watakachokipata Burundi kitaondoa ndoto zote za kifikiria tutsi-hima empire.
 
Huyu chizi Nkurunziza anataka wangapi wafe ndio aachie ngazi? angeachia tuu kuepusha disaster inayokuja mbeleni,sioni akitoboa huyu ataishia asipopataka soon

Tatizo siyo hizo nchi. Tatizo ni watutsi. Nchi yoyote ikisha kuwa na watutsi hata 10% ujue ni shida tupu. Ni watu wa ajabu sana. Nkurunziza hana tatizo sana kwani suala la muhula liko kisheria isipokuwa these blood thirsty tutsis wanachukua kisingizio hichohicho cha kuhalalisha vurugu.

Lakini, nadhani hili suala ni la kinabii zaidi kwani kipigo watakachokipata watutsi nchini Burundi kipindi hiki cha nkurunziza kitaondoa ndoto zote za watutsi kufikiria tutsi-hima empire. Tena nkurunziza asiachie ngazi hata wakileta gereda ili ikiwezekana mazungumzo yarudiwe upya ili hata %ge za lawmakers & military officials ziendane na asilimia ya kila kabila ndani ya nchi.
 
Back
Top Bottom