MGAWANYIKO CCM > Vita vya panzi furaha ya kunguru

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Tumeshuhudia mengi yaliyotokea kipindi cha uchaguzi, na dalili wazi ya wagombea nafasi kadhaa za uongozi toka chama cha CCM kuangukia pua au kupata mwanguko wa mende tuliutazamia na tumeshuhudia kwa macho yetu.
Kabla hatujatulia tayari makundi mawili ndani ya CCM yanaanza kutifuliana vumbi kwa kugombea kukalia uongozi wa meza kuu ya kutunga sheria nchini USPIKA ili kila kundi kulinda maslahi yao IKIWA NI KUNDI LA WENYE PESA KUTETEA MASLAHI YA ULAJI PESA ZA WALIPA KODI AU KUNDI LINALOTETEA MASLAHI YA WANANCHI NA TAIFA KWA JUMLA.
Kwa mtazamo wangu jipu ndani ya CCM bado hata uvundo kamili kuwepo kwani kwa sasa tunachoshuhudia ni maumivu makali ndani ya uvimbe na ipo siku litakapovunda na kupasuka anza toa usaha ndo vyama vya upinzani vitakapochekelea kuna barabara imenyoka kwenda Ikuku,
Tusidanganyike kwamba kuna jitihada za kuondoa tofauti zao, vinginevyo wangetambua ishara za nyakati na maana ya usemi huu ngoma inayovuma sana haikawii kupasuka. Mwenye masikio haambiwi sikia au mwenye macho hana haja ya kuambiwa tazama.
Kwa uzoefu wangu mtu ambaye ana ile moral (maadili) ndani ya moyo na imani yake Chenge mbunge mchaguliwa toka kanda ya Ziwa asingethubutu kutia guu lake kugombea Uspika kwani jina lake lishachafuka sana tu na bado kesi mahakamani, na itakuwa aibu kesi ikiisha mahakamani spika wa bunge la Muungano wa Tanzania anahukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia katika ajali ya gari na kosa la kuendesha gari bila bima, hayo nayasema kwa mfano tu kama ishara za nyakati kama mahakama ikimwona ana kosa.
Vema chenge akae kando na kama amefaulu kutetea ubunge wake ashukuru Mola vinginevyo aone vyombo na wananchi walivyochachamaa kwa kujitosa kutetea kiti ili kulinda maslahi ya wenye nazo.
 
Anatumwa na Lowasa ili amsafishie njia kwenda kwenye Urais hapo 2015.
 
Back
Top Bottom