Mgao umeanza upya, gesi imeadimika kutoka Songosongo
Mkuu,
Acha kuposha. Otherwise tutakuwa tunawapa nafasi hao wanaoponda kuwa JF tunaweka habari za uongo. The fact ni kuwa kutawepo na upungufu mkubwa wa umeme katika Gridi ya Taifa kuanzia Mei 19 hadi 26 ili kutoa nafasi ya matengenezo makubwa katika visima vya gesi Songo Songo. Haina maana kuwa gesi imeadimika. Taafifa iliyotolewa na Tanesco ni kwamba mgao unatokana na kusimamishwa kwa uzalishaji wa gesi asili iliyopo katika Kisiwa cha Songo Songo mkoani Lindi na wamiliki wa visima hivyo Pan African Energy Tanzania Limited, wakiwa na lengo la kuvifanyia ukaguzi na ukarabati ili kuboresha uzalishaji wa gesi kwa ajili ya kufulia umeme.
Lengo la kuzimwa visima na mitambo hiyo ya gesi ni kuboresha viwango vya gesi inayozalishwa na kusafirishwa kutoka kisiwa cha Songo Songo hadi Dar es Salaam kwa kufua umeme na kutumiwa viwandani. Kati ya Mei 19 hadi 23, utakuwepo upungufu wa megawati 200 zinazofuliwa kwa kutumia gesi kutokana na visima vya Songo Songo kuzimwa kimoja baada ya kingine kwa ukaguzi wa kiufundi.
Kutokana na kuzimwa kwa visima hivyo vituo vya Songas, Ubungo Gas Plant na Tegeta Gas Plant vinavyotumia gesi asilia kufua umeme vitasitisha shughuli zake kwa siku hizo nne na hivyo kusababisha upungufu wa umeme katika Gridi ya Taifa kwa sababu umeme wa gesi huchangia karibu nusu ya umeme unaofuliwa katika vituo vyote nchini.
kuanzia Mei 23 hadi 26, mchana mgao wa umeme utakuwa megawati 300 kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 5 usiku na megawati 50 kuanzia saa 5 usiku hadi saa 2 asubuhi, hivyo kuwaomba wenye viwanda vikubwa kutumia kipindi hicho cha mgao kufanya usafi na matengenezo ya mitambo yao, hususan viwanda visivyokuwa na jenereta za dharura.
HabariLeo | Tanesco yatangaza mgao nchi nzima
Wakuu zangu, msifikiri kwamba sisi Watanzania bado mazuzu kiasi kwamba habari hii ikawa na sababu za msingi wakati ni vichekesho vitupu. Songosongo kusema kweli hawawezi kufunga mitambo yao kwa ajili ya ukarabati wakati hawana stock ya kutosha kwa kipindi ambacho wanataka kufanya ukarabati huo.
Napowasoma hapa janvini inaonyesha kaa vile Songo wanapovuna gas basi huenda moja kwa moja kutumika wakati sivyo. Kama kweli kulikuwa na mpango wa kufanya ukarabati hawa songo walitakiwa kuzalisha gas ya kutosha na kuwa na stock ya kutosha ili kukidhi hizo siku wanazotaka kufunga, hivyo kutoathiri ugawaji wa gas au laa nachoweza kufikiria hapa ni kwamba Songos kama wakulima wa kwetu hawana maghala ya kutosha kuhifadhia gas ama ni shirika dogo ambalo uzalishaji wake ni mdogo sana kuliko mahitaji hivyo wanauza kila wanachovuna kila siku..
Kwa wale wanaojua how the freemasons operate, hakuna jipya hapa.This is a deliberately created crisis.And mind you this will not be the last. They create one crisis after another ili tushindwe kupanga mambo yetu,tukose matumaini na to loose confidence in ourselves and evenly tuwe easy to manipulate and rule.