Mgao wa umeme wa kufa mtu watangazwa, Juni 2011 na kuendelea

Kuanzia tarehe 15 mwezi huu, mgao kwa mikoa yote iliyoungwa na gridi ya taifa. Hali sasa inarudi kulekule!! Source: Habari ITV saa mbili
 
Hivi ina maana serikali haina pesa za kununua mitambo mipya ili kukomesha tatizo hili? Mbona kila mara matatizo yanajirudia yale yale?
Mi nadhani kuna mchezo mchafu unaendelea ambao unasababisha serikali isiwe na nia ya dhati kukomesha tatizo hili.Anyway kila lenye mwanzo halikosi mwisho!
 
Hii Tanzania cjui inakwenda wapi..?nina wasiwasi na uwezo wa viongoz wetu..cjui ninyi wana jf mnatizamaje hili.
 
haya ndio matunda ya ccm! Ngoja nipate japo :majani7: ili nipoteze japo mawazo na kupunguza hasira mie.
Ahahahaaah!! Achana na majani wewe.....lakini kwa kweli hii hali inachanganya sana, hivi kweli muda wote huu hatujapata suluhisho la hili tatizo?
 
Wakuu hili ni pigo jingine tena toka TANESCO. Nimemsikia CEO wa TANESCO akisema kupitia TBC1 kuwa kutakuwa na mgawo wa umeme nchi nzima kuanzia taehe 19 hadi 29 mei ili mitambo ya gas ifanyiwe ukaguzi na kwa maana hiyo megwati 200 zitakosekana. Cha kushangaza ni kwamba alipoulizwa kuwa wana mpango gani kupunguza tatizo wakati wa ukaguzi huo anasema ati wako kwenye mchakato wa kukodi maitambo kama ambavyo wamekuwa wakiripoti. Sijui mchakato utachukua miaka mingapi!!
 
Ngeleja vp, bado anashughulikia malipo ya DOWANS? Naona tokea bosi wake amuadhiri mbele ya umma hana hamu ya kujua kina cha maji ya Mtera au gesi ina nini, teh!
 
Ni kapelo, shati na suruali za ccm ndizo zimetufikisha hapa. Yatupasa tuwe wakali sana hata kama watasema tunavuruga amani. Jamani wanyonge tuungane, tutoke ndani ya jf, tuingie mitaani tudai tunachoamini kuwa ni chetu. Bila ya hivyo, hasira zetu zitaishia humu jf na hakuna tutakachobadili.
 
Ni kapelo, shati na suruali za ccm ndizo zimetufikisha hapa. Yatupasa tuwe wakali sana hata kama watasema tunavuruga amani. Jamani wanyonge tuungane, tutoke ndani ya jf, tuingie mitaani tudai tunachoamini kuwa ni chetu. Bila ya hivyo, hasira zetu zitaishia humu jf na hakuna tutakachobadili.

Soon i will show an example of Peoples Power
 
Viongozi wetu wa serikali na mashirika ya umma ukiwaona wamevaa suti ndani ya mashangingi unaweza ukafikiri akili zao zimetimia, kumbe 99% ni majuha. Inawezekaneje nchi isiwe na mipango endelevu? Hatujawahi kuwa na vita wala majanga makubwa kama tsunami au matetemeko ya ardhi kama yanayotokea kwa wenzetu e.g. Japan tungesema labda haya majanga yalituharibia mipango yetu! Tena tuko chini ya serikali ya chama kimoja kwa karibu miongo 5 sasa, ningetegemea kuona consistency ktk utekelezaji wa mipango ya kimaendeleo. Hivi nani katuroga jamani?
 
Bora kwetu mama anatumia vibatari. Asubuhi anapenga makamasi meusi kwa sababu ya moshi. Hongera ccm kuendelea kuniulia mama yangu.
 
Where is ngeleja na kauli zake kwamba Umeme utakuwa historia tz?

Where is Makinda aliyezuia hoja binafsi bungeni? Pia akamkingia Ngeleja kifua alipotakiwa na Mnyika kutangaza upungufu wa Umeme janga la kitaifa?

Where are wabunge wa ccm waliokuwa wanashangilia kila Ngeleja akikingiwa kifua?
 
Dawa ni kufanya Nchi iwe kwenye Giza kabisa kwa mwaka means kulipua mitambo yote ya Tanesco ili Tanesco ife tuanze upya.
 
Nitawauliza pindi wakija na vitambi vyao miaka michache ijayo!...wametuhujumu maisha yetu,wametudanganya na kutubabaisha vya kutosha! Ni CCM nazungumzia
 
Hii nchi sijui imelaaniwa!? Kila kitu ni siasa siasa tu, ubabaishaji, kuchekacheka tu, mipango bubu. Maendeleo bila ccm inawezekana, wananchi tubadilike jamani tulitose hili lichama la wazee.
 
Mlimani tv habari

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco ametangaza kutakuwepo mgao wa Umeme kuanzia tarehe 19 May kutokana upungufu wa megawatt zaidi ya 200. Amesema mvua zinazonyesha hazijaketa nafuu yoyote

(nilipatwa na hasira kuhusu taarifa hizi nikashindwa kusikiliza vizuri maelezo zaidi)

Mkuu hiyo hasira si peke yako. Come to think of it! Kuna Tanesco, ministry husika bunge etc. Hivi hizi machinery zote zinafanya nini? 19 years gone same story michakato upembuzi sijui nini. Mr president jk for once be serious on hili. Jamani huku chini mnaotutawala hela ya mafuta ya kula ni shida je jenerata tutaweza? mmesahau kuwa mnakula na kipofu mbona mnatushika mkono@
 
Lazima upate hasira Mkuu, tatizo la umeme ni la miaka 19 sasa, ndiyo miaka 19 tangu 1992 lilipoanza rasmi na hadi leo hii hakuna ahueni yoyote ile ya kuondoa adha hii isiwepo tena.

Hivi planners wa hii nchi wako wapi?
 
kichefuchefu,TANZANIA tunakwenda wapi,tutavumilia mpaka lini.nani wakututatulia kero zetu hizi,bila umeme wa uhakika kila kitu bei juu,Watanzania wenzangu tumefika mahala pakukataa usanii huu,maisha yetu yanaangamia taifa la kesho hakuna,TUVUMILIA MPAKA LINI?
 
Back
Top Bottom