Mgao wa Umeme wa Gesi, muhimu lakini bad timing

muonamambo

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
875
545
Hata kama hatua inayotakiwa kuchukuliwa ni muhimu, lakini kusema mgao kuanza Feb 1 -10 ni kuwatukana wananchi.

Kwa miezi 3 iliyopita Taifa hili limepita kwenye Mgao mkali usio rasmi.

Mgao huo umeziacha familia nyingi kwa mashaka makubwa kwa kuwa maisha yao yanategemea Umeme.

Ukiacha hayo kaya nyingi zimeingia kwenye gharama zisizo za lazima kutokana na kukatika kwa umeme .

Mbaya zaidi si Tanesco wala wizara , waliojitokeza hadharani na hata kutoa Taarifa ya Mgao , hatua wanazotegemea kuchukua na hata kuomba Radhi.

Leo baada ya miezi 3 . TANESCO wanakuja na tena mgao mwingine juu ya mgao wa awali.

Kulikuwa na minongono kuwa mgao unatokana na ukosefu wa Mvua .

Je ni kwa nini TANESCO wasingesubiri mvua zirejee ili mitambo ya kufufua umeme wa maji irejee kwenye kiwango chake ndipo waje kuanza kuzima umeme wa Gesi ?

Sasa tuna deficit kwenye umeme wa Maji wanaongeza na deficit kwenye Gas .serious ?

Mama anaupiga Mwingi , Makamba anatakiwa kumsaidia .

Kuacha mambo yaende tu …

Atakuja kuvuna mabua
 
20220128_221607.jpg
 
Back
Top Bottom