Mgao wa Umeme Vs Makamati ya Bunge Vs Maendeleo - Jee tutafika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgao wa Umeme Vs Makamati ya Bunge Vs Maendeleo - Jee tutafika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chidide, Feb 9, 2011.

 1. c

  chidide Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mambo yanyoendelea Tz yananikatisha tamaa sana. Mimi nipo nje ya nchi toka mwaka 2009, but nafuatilia sana mambo yanayoendelea huko through magazeti na humu kwenye JF. So bado nipo kwenye position ya kuelewa kinachoendelea nchini mwangu.
  Kitu kinachoniuma sana ni mgao wa umeme na jinsi wanasiasa wetu wanavyoshughulikia suala hili. Naongelea wana siasa kwa vile katika mfumo wetu Tz wanasiasa wana nguvu zaidi kuliko watendaji, na most of watendaji wamegeuka kuwa wanasiasa.
  Hivi mpaka sasa wakati tupo kwenye mgao since end of Nov, kuna mkakati gani wa kuondokana na kadhia hii? Nasema hivi kutokana na uhusiano uliopo kati ya matumizi ya umeme na maendeleo kama ninavonukuu paper hii ya Anjum Aqeel and Mohammad Sabihuddin Butt*,

  " By applying techniques of co-integration and Hsiao’s version of Granger
  causality, the results infer that economic growth causes total energy
  consumption. Economic growth also leads to growth in petroleum
  consumption, while on the other hand, neither economic growth nor gas
  consumption affect each other.
  However, in the power sector it has been
  found that electricity consumption leads to economic growth without
  feedback"


  source :http://www.unescap.org/drpad/publication/journal_8_2/AQEEL.PDF

  Nafikiri kila Mtanzania kwa sasa atakuwa anaona jinsi anavyoteseka/athirika na mgao wa umeme. Kwa wale wanaoishi mijini wanaweza kuona jinsi wananchi hasa wenye biashara ndogondogo/ajira isiyo rasmi wanavyo athirika na huu mgao. Sawa inawezekana ni tatizo ambalo lilikuwa nje ya uwezo wetu, but now tuna mkakati gani wa kulishughulikia?

  Kwa nini wanasiasa wetu wanashupalia mamabo ya kamati za bunge as if hiyo ndio tatizo letu kwa sasa? Kwa nini hatusikii hata mtu mmoja akituambia mgao utaisha lini?
  Mimi ninaamini mgao hautaisha Tanzania. Najua wengine hawawezi kunielewa bu facts ni kama hivi:

  1) TZ tunazalisha 750MW na mahitaji ni zaidi ya 800 MW.
  2) Demand inaongezeka by 14% ambayo ni 112 MW, hii ina maana lazima kwa mwaka tuongeze production by 150MW ili tuweze kutosheleza demand tuu
  3) Ili kuwa na umeme usio na maatizo lazima tuwe na kitu kinachoitwa spinning reserve, huu ni umeme wa ziada baada ya demand ambao utatumika iwapo kuna power plant itapata matatizo. South Afrika wana spinning reserve ya 8000 MW (8 GW) na bado wana invest for the next 20 years.

  Sasa sisi tutaendeleaje na kushupalia haya makamati ya bunge???????????Hakuna manufaa yoyote zaidi ya kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015. Inauma hasa unapoona jirani yako anamwachisha mtoro wake shule kwa kukosa ada kuokana na biashara yake ya welding kuathiriwa na mgao wa umeme. Tanzania hatuma shida ya energy sources. una shida ya maadili ya kuileea nchi maendeleo.

   
 2. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kma ulidhani kuna mwanasiasa hta moja aliye pale bungeni kutuondolea mattz yetu watanzania umeliwa,pale wote wachumia tumbo tu,kwanza wanaangalia kujineemesha wao na familia zao halaf koo zao halaf marafiki na makabila yao baada ya hapo ndo watanzania. Yan hakuna utaifa kbs nchi hii nyerere alikufa nao,si upinzani wala ccm wote wanachumia tumbo hakuna wa kutuendeleza hapa
   
 3. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kama unajiandaa na 2015 basi utalia tena manake wakati wa uchaguzi watu mawazo yao yanakuwa mengine lakini baada ya uchaguzi watu wanalia. Jiulize, wala usiende mbali hapo Dar ni majimbo mangapi bado CCM inapeta?:coffee:
  Haya ndio mavuno ya uchaguzi uliopita!!
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Naungana nawe katika suala zima la athari za mgao wa umeme, ila kwa upande wa hizo kamati, labda nikujuze kidogo kazi ya hizo kamati na kwisha/kuendelea kwa mgao wa umeme.
  Tanesco ni shirika la umma linalomilikiwa na serikali 100%
  Tanesco ndilo pekee linaruhusiwa kuuza umeme kwa wateja, kwa hiyo mzalishaji yeyote inabidi aliuzie tanesco.
  Mgao wa umeme umesababishwa na uzalishaji mdogo wa umeme ingawa mwenyewe unakiri kuwa TZ hatuna uhaba wa vyanzo vya umeme, Kuna vyanzo ambavyo haviendelezwi kikamilifu kwa sababu havina ulaji kwa wakubwa. Ndiyo maana wang'ang'ania mitambo ya kutumia mafuta nk ambayo ni rahisi kuchakachua bei na kupata 10% sasa 100% commission, wanaacha chanzo kama rufiji.
  Nini kazi za kamati?
  Kwa kuwa tanesco ni shirika la umma kamati ya bunge ya mashirika umma ndiyo yenye jukumu la kuchunguza kama tanesco inatenda sawa sawa. Kama kamati hii itachakachuliwa na kuingiza watu waaohusika na uchukuaji wa hizo commissions na uigiaji wa mikataba mibovu ya umeme, basi tatizo la umeme halitaisha kwani wakati wote wataelekeza mawazo yao kwenye kuingiza mitambo na mikataba itakayowaingizia commission kubwa.
  Kwa kuwa shirika hili ni la serikali 100% na serikali ndiyo inalaumiwa kwa kutotenda haki katika kushughulikia umeme, then watchdog ni kamati ya bunge.
  Nini kazi ya upinzani?
  Upinzani kwa kifupi ni kioo cha serikali, na ni serikali inayosubiri kuingia madarakani iwapo hiyo iliyopo itashindwa kazi.
  Kamati kama hiyo ikiongozwa na upinzani, serikali itakuwa makini isije ikawa dhaifu na udhaifu wake ukaanikwa na hatimae wananchi kuichukia na kutoichagua.
  Wananchi wamechagua CDM kiwe chama kikuu cha kufanya kazi hiyo; hivyo unapoona chama tawala (serikali) kinajichagulia nani wa kukichunga, then ujue kuna kitu kinataka kufichwa - nadhani unayajua ya downs, iptl, kiwira nk yote yanahusiana na umeme.
  Hivyo CDM wanaponga'ng'ania hizo kamati, wnafanya hivyo kwa maslahi ya wananchi waliowachagua kuwa wapinzani (kambi kuu). Wakishindwa kutumikia kile wananchi walichowachagulia, watakujaje baadae kuomba kikubwa zaidi - kuongoza nchi?
  Huo ni mfano mmoja wa kamati moja tu. Hivyo hivyo kwa mahesabu ya serikali, serikali za mitaa nk.
  Watu hawakuwa wajinga walipoweka mfumo kuwa kamati fulani lazima ziongozwe na upinzani!
   
 5. n

  ngoko JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  chidide, hapa TZ matatizo haya ya power ni kweli hayawezi kuisha maana yamefanywa mtaji wa kuombea kura kwa wananchi na kwa kuwa mtaji kama umeendeshwa vizuri huzalisha faida vivyo hivyo wanasiasa wetu hupata faida kwa kutafuta cheap and expensive solutions ambazo kwa nyuma yake wananufaika kipesa e.g. Richmond, IPTL , Dowans etc , Return on Investment (ROI) kwa hawa wanasiasa wetu wanaiangalia kwa kupungua uzalishaji na hivyo kuwapa nguvu ya kuomba kura na kutoa ahadi lukuku. Mwisho wa siku mikataba ni siri ili msielewe utumbo uliomo ndani, na mkibahatika kuiona mkipiga kelele wanajipanga ku defend kisheria even if ni ICC watafika ...., we acha tu nchi hii siku itafika tutapiga U-turn.
   
 6. S

  Sina pa kwenda Senior Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Good idea! Nadhani hao wanaopanga hizo kamati majumbani mwao kuna umeme na hata kama unakatika majenereta yapo so kwao sio shida, shida kwetu sie walalahoi.

   
Loading...