Ngamanya Kitangalala
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 501
- 1,214
Nchi yetu kwa sasa imepata changamoto ya upungufu wa mvua, hii ni kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA), jambo lililopelekea upungufu wa uzalishaji wa umeme hapa nchini, hiyo ni kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na shirika letu la umeme hapa nchini (Tanesco) jana tarehe 18 Novemba 2021
Ukisoma kwenye tovuti rasmi ya shirika letu la umeme (Tanesco) inaonyesha shirika letu hilo kwa sasa lina uwezo wa kuzalisha umeme wa MW 1602
Ambapo kati ya hizo, vyanzo vya maji pekee (Hydroelectric) vinazalisha MW 561.843 , ambazo ni sawa na asilimia 36.64 ya umeme wote unaozalishwa hapa nchini na gesi (Thermal gas) na dieseli kwa pamoja zinazalisha takribani MW 796.34 , sawa na asilimia 63.36%
Lakini ukisoma kwenye ILANI YA UCHAGUZIYA CHAMA CHA MAPINDUZI YA MWAKA W020-2025 kwenye ukurasa wa 99, unaozugumzia kuhusu NISHATI, inaonyesha nchi yetu imefanikiwa kuongeza uzalishaji wa umeme, kutoka MW 1308 mwaka 2015, mpaka MW 1602 mwaka 2020, ambapo ongezeko hilo limefanya nchi yetu kujitosheleza na umeme na kuzalisha umeme wa ziada wa MW 445, ukilinganisha na mahitaji ya sasa ya umeme nchini ya MW 1120.12
Sasa taarifa ya jana ya Tanesco, inaonyesha kwa sasa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea, shirika lina upungufu wa uzalishaji wa umeme kwa MW 345 sawa na asilimia 21 ya umeme wote unaozalishwa na shirika hilo wa MW 1602.
Sasa swali la kujiuliza, kama tulikuwa na ziada ya umeme kwa MW 445 na sasa kuna upungufu wa uzalishaji wa umeme kwa MW 345, huo mgao unaendelea unatoka wapi?