Mgao wa umeme umesitishwa, lakini matamshi haya ya TANESCO vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgao wa umeme umesitishwa, lakini matamshi haya ya TANESCO vipi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 30, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wananchi tumefurahi kwamba mgao wa umeme umesitishwa hasa kwa mikoa ambayo ilikuwa kwa njia moja au nyingine ilikuwa imeathirika na mgao huo.Lakini matamshi yaliyotolewa na TANESCO mbona hayaeleweki.Hivi TANESCO wanataka tuamini kwamba sababu za kusitisha mgao ni utengenezwaji wa mashine moja tu kati ya tatu na kuongezeka kwa uzalishaji Kidatu,Mtera na Pangani? Kwa mtizamo wa karibu,hii ina maana kwamba usitishwaji wa mgao umesababishwa hasa na kuongezeka kwa uzalishaji Kidatu,Mtera na Pangani,kwa vile mashine moja isingeweza kuongeza uzalishaji kiasi hicho.Mimi si elewi ni miujiza gani imetumika kuongeza umeme Kidatu,Mtera na Pangani,hasa tukizingatia kwamba maji yanaendelea kupungua kwa vile tumeshaanza kipindi cha ukame.Nionavyo mimi ni kwamba kuna ujanja wa sungura hapa.Tusisahau kwamba tunaelekea kwenye uchaguzi,na mambo mengi yatafanywa ili ionekane kwamba serikali ina wajali watu wake.Tuwe macho wadau,vinginevyo tutaingizwa mkenge.Inawezekana hata tatizo halikuwepo,'it could be an ochestrated scenario.'
   
 2. M

  Makfuhi Senior Member

  #2
  Sep 30, 2008
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nafikiri sababu sio hiyo tu. Kuna njama nyingine kwani nimesikia wakimtaja richmond. Isije ikawa ni sababu ya kumsafisha na kuona kwamba hatuwezi bila yeye!
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  shida ya umeme iko na mgao uko. Nenda Kigoma uone kama hakuna mgao. Wanaposema sasa hakuna shida ya mgao nchini kwa sababu tu Dar umeme unawaka bila katizo they are wrong. Waseme ukweli kwamba kulikuwa na shida Dar na sasa imeisha.
  Tena kwa upande wangu naona hakuna hata haja ya kututangazia kwani kama umeme haupo Kigoma mbona hakuna anayetangaza?
  Lets be fair jamani!
   
Loading...