Mgao wa Umeme Umekwisha,Tunaombeni Radhi..TANESCO

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
MGAWO wa umeme uliokuwa ukiendelea nchi nzima sasa umekwisha baada ya mafundi kutoka Marekani kuwasili na kutengeneza mtambo mmoja wenye uwezo wa kuzalisha megawati 40.



Awali Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ilitangaza kuwepo kwa mgao wa umeme nchini nzima baada ya mitambo mitatu ya Kampuni ya Songas inayozalisha umeme wa gesi asilia ya megawati 182 kuharibika.



Akizungumza na Waandishi wa habari jana ofisini kwake Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masudi alisema mgao huo umesitishwa rasmi kuanzia sasa baada ya mafundi hao kufanikiwa kutengeneza mtambo mmoja.



“Kuanzia leo hakutakuwa na mgao wa umeme kwa sababu wataalamu kutoka Marekani waliwasili juzi na kuanza kazi ya kutengeneza mitambo iliyokuwa imeharibika,”alisema Masudi.



MYTAKE
TANESCO na SONGAS wanastahili kupongezwa kwa hili ila wanatakiwa wawe na mafundi ambao wanaweza kutengeneza mitambo hii kuliko kutefgemea watalaam kutoka marekani.wawatumie watanzania na kuwapa mafunzo ambayo yatawasaidia




Alisema megawati hizo 40 zilizoomgezeka pamoja zile 72 zilizokuwa zinazalishwa awali na kampuni hiyo zitaweza kusaidia na kwamba mbali na megawatt hizo pia wanategemea mitambo yao mingine inayotumia nguvu ya maji na mafuta.



Badra aliongeza kusema kwamba kutokana na hatua hizo Tanesco ina uhakika suala la mgao wa umeme halitakuwepo tena na kwamba kama kutakuwa na tatizo lolote watatoa taarifa mapema iwezekanavyo.



Kuhusu suala la Kampuni ya Songas kuharibikiwa mitambo yao wakati wameingia mkataba na Tanesco alisema kwa mujibu wa mkataba wao katika kipindi hiki ambacho Kampuni hiyo ilishindwa kuzalisha umeme katika kiwango kinachotakiwa hawatawalipa.



Alisema mkataba huo unawaelekeza wawalipe mara baada ya wao kuzalisha umeme tena kwa kiwango walicho kubaliana tu na kwamba kwa mantiki hiyo katika kipindi chote walichoshindwa kuzalisha kutokana na mitambo yao kuwa mibovu hawatalipwa.
 
Tuombe radhi ya nini? Kwani TANESCO wanakuomba radhi pale unaposhindwa kumudu kulipia umeme wao?
 
Back
Top Bottom