Ulukolokwitanga
JF-Expert Member
- Sep 18, 2010
- 8,396
- 7,968
Jenereta ya jirani yangu inayoniamsha usingizini saa 12 kila siku leo haisikiki kabisa....
Salon ya nywele hapa jirani naona mayankee wanatabasamu tu meno yote nje wanakamua hela leo...
Jamaa wanochomelea mageti na welding nao wanachapa mzigo tu wako full shangwe....
Nimeona hata wauza Ice cream leo wako mtaani na madeli yao...
Mashine za Car wash ziko full pressure, magari yanaingia yanatoka vijana wanakamata hela...
Kuna mtanga mmoja hapa jirani huwa anatukamulia juice ya miwa naye anapiga kazi... Anasema leo hata muazini aliita waenda masjid sa11...
Stationery zimefunguliwa Jumapili watu wanafanya typing na madesktop yao wana make mahela....
Mwenye ratuba ya mgao wa umeme atujuze jamani tunashangaa jana na leo mambo sio mabaya ingawa jana tuliangalia game ya yanga hadi half time. Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete, hivi hupendi watanzania hao hapo juu ambao wako kwa maelfu wakiendeleza matabasamu waliyonayo leo yawepo kesho, keshokutwa, wiki ijayo, mwezi ujao, mwaka ujao na hadi 2015 unaondoka na watu wakukumbuke kuwa ulileta umeme na sio kukumbukwa kwa kucheza Kiduku...