Mgao wa umeme ni mpango wa kutaka kuipa dowans hela zaidi ya zile za kesi

MWANASHERIA

Member
Aug 20, 2010
84
11
Kuna habari za kiinteligensia na za kuaminika, kuwa pamoja na kupungua kwa vina vya maji kwenye mabwawa ya kuzalishia umeme, makali ya mgao wa umeme yameongezewa nguvu kwa makusudi ili kutushawishi watanzania mitambo ya DOWANS inunuliwe na serikali, ukizingatia kwamba DOWANS hawana biashara nyingine wala eneo lingine la kuweka hiyo mitambo. hata hao wanaojidai wanataka kununua mitambo ni wale wale, ili baadae ibaki hapa hapa kwa kuingia mkataba na hao watakaojiita wengine, na hii ni kama na kuiuzia Tanesco litashindikana.

Hata huu mpango wa kutaka kuiwasha hii mitambo ni kutaka either DOWANS wakatushitaki tena, ili wapate hela nyingine ukiacha hizi ambazo wanakaribia kupewa AU tuingie nao makubaliano ya kutuuzia umeme pamoja na kapacity charges za 152 million per day vile vile.
Na hata kuwekwa January Makamba kwenye kamati ya Nishati ni mpango mahususi uliosukwa kuwezesha DOWANS kupata hela zaidi, na mpango umesukwa toka juu kwa mkuu wa kaya, ukizingatia Makamba alikua msaidizi wa JK wa karibu, huku akijifanya sasa hivi anaishauri serikali cha kufanya kuhusu umeme, wakati amekua na JK kila siku kwa miaka mitano.


NB: Kwa mujibu wa kamati ya akina MWAKYEMBE, hiyo mitambo ya DOWANS, serikali inaweza kuinunua toka kiwandani Houston, Marekani kwa shiliingi Billioni 42 tu, kwani serikali imeshindwa kununua mipya mpaka leo wanaongelea kukodi ya dharula.
OOH TANZANIA, NCHI YA DEAL, EVERYTHING IS DEAL, MPAKA MAISHA YA WATU NI DEAL....
 
teh, jikaze mwanakwetu. Ipo siku utakubali kuingia road, kwa sasa bado hujakamatika sawa sawa.
 
Taifa linaangamia, dharura miaka 15.!! Tangu IPTL Richmond hadi Dowans. Wasitake kutusadikisha Wizi kwa kisingizio cha dharula. Habari za ukame na mgao hazijaanza leo. Chonde chonde Bunge, msibariki wizi huu. Na tukae gizani ili tupate suluhu muafaka. Jino bovu alipozwi na panado. Fuatilieni hata mitambo ya dizeli ya mwanza . Kuna issue. WABUNGE msikubali mtego huu.
 
Back
Top Bottom