Mgao wa Maji ni Somo Kwetu Kuhusu Ubaya wa Ufujaji

IslamTZ

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
309
182
Abuu Kauthar

Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni liliingizwa katika mgao wa maji kwa sababu ya ukame ulioikumba nchi hivi karibuni. Jambo la kushukuru ni kwamba mvua zimeanza kunyesha.Kipindi mgao ulipokuwa mkali, eneo letu Mburahati halikupata maji kabisa kwa wiki tatu. Vijana wa nyumbani walilazimika kwenda kuchota maji kwa kutumia ndoo kutoka kwa jirani mtaa wa pili ambaye ana kisima.

Wakayti tukimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuletea mvua, tuna si vema kuacha mgao ule wa maji upite bila kujifunza. Binafsi, nina mambo mawili. Kwanza, uhaba ule wa maji ulifundisha thamani ya rasilimali hii muhimu. Pili, niligundua kuwa tunatumia rasilimali ya maji kwa fujo sana pale yanapokuwepo.

Kipindi cha uhaba, niliweza kuoga hata nusu ndoo na kuwa msafi. Ndoo nzima ilinitosha kwa kila kitu: kutimiza haja ndogo, kupiga mswaki na hatimae kuoga. Labda nilipohitaji kufanya haja kubwa ndipo nilihitaji ndoo mbili kwa sababu ya kuondoa uchafu (flushing).

Hata hivyo, nikikumbuka wakati ule hatuna tatizo la maji, tuliyachezea mno. Kwa kutumia bomba la juu, mtu anaweza kutumia hadi ndoo nne! Tulifungua mabomba hadi mwisho kwa ajili ya kunawa mikono tu huku maji mengi yakipotea bure.

2.jpeg

Nijuavyo, hata dini zimekataza matumizi ya fujo ya rasilimali au kuchupa mipaka. Badala yake binadamu tumehimizwa kutumia ziada ya rasilimali tulizonazo katika kutoa sadaka kwa maskini sio kuzifuja. Dini zinasema matumizi ya fujo ya rasilimali hayafai kama ambavyo pia ubahili haufai. Hayo nimehakikishiwa na marafiki zangu Wakristo na Waislamu.

Tatizo la matumizi mabaya ya rasilimali na ufujaji ni kubwa na la kidunia. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na mazingira (UNEP), moja ya tatu ya chakula kinachozalishwa duniani kwa ajili ya matumizi ya binadamu (sawa na tani bilioni 1.3) hupotea.

Kiasi cha chakula kinachopotea kinagharimu kiasi cha dola za Kimarekani bilioni 680 katika nchi za viwanda zilzioendelea na kinafikia dola za Kiamarekani dola bilioni 310 katika nchi zinazoendelea. Matunda, mboga za majani, pamoja na vyakula vya mizizi ndiyo aina ya vyakula vinavyopotea zaidi kuliko aina nyingine. Kila mwaka, wakazi wa nchi tajiri wanapoteza au wanafuja chakula (tani milioni 222) takriban sawa na kiasi chote kinachozalishwa na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kinachofikia tani milioni 230.

Kujua zaidi kuhusu upotevu wa chakula, kuna ripoti nzima ya Umoja wa Mataifa iliyotoka mwaka huu inayopatikana hapa
33.jpeg

Ufujaji huu unatokeaje? Bila shaka ni katika mlolongo mzima wa uzalishaji kuanzia kinapovunwa shambani hadi kinapopikwa na kuliwa. Inakera kuona familia zinapika chakula kingi kuliko mahitaji yao na kuishia kukimwaga. Hivi yawezekanaje, kwa upande mmoja kuwa na watu wenye njaa wasiomudu hata mlo mmoja lakini kwa upande mwingine kuna watu wanakula robo sahani na kumwaga kilichobakia?

Ndugu zangu naandika kwa uchungu kuwaomba wenye tupambane na tatizo hili ambalo ni kubwa kuliko tunavyoweza kufikiri la kufuja sio tu chakula bali hata maji. Hebu pitieni hapa muone nukta kumi kuhusu ufujaji wa chakula na mtashtuka. Je mnajua kuwa zaidi ya 1/3 (theluthi) ya chakula kinachozalishwa duniani kote kinafujwa? Je mnajua kuwa thamani ya chakula kinachofujwa duniani kote ni takriban dola za Kimarekani trilioni moja na ni sawa na tani bilioni 1.3? Je mnajua kuwa watu wote wanaolala na njja zaidi ya bilioni moja duniani kote wangeweza kulishwa kwa chini ya robo ya chakula kinachofujwa Marekani, Uingereza na Ulaya?

Mengine ambayo myajue ni kuwa eneo la ukubwa zaidi ya China linatumika kuzalisha chakula ambacho hatimaye hakiliwi, yaani kinafujwa na kwamba
robo ya asilimia 25 maji ya baridi (yasiyo na chumvi) ya dunia yanatumika kuzalisha chakula ambacho hatimaye kinafujwa. Mbaya zaidi ni kuwa zaidi ya nusu ya ufujaji wa chakula hutokea nyumbani.

Baadhi yetu tukiona kuwa tatizo hili ni kubwa na la kidunia tutasema: "Itasadia ni mimi nikifanya chochote." Hayo ni makosa. Kwanza, mabadiliko yanaanza na wewe. Pili, ni wewe ndiye utajibu kwa Mwenyezi Mungu wako (kama Muumini) juu ya ufujaji ulioufanya (Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe). Tatu, hata kama huna dini huamini katika ubinadamu na utu?

Nimalize kwa kusema, watu bilioni 2.3 wataongezeka duniani ifikapo mwaka 2050. Ongezeko hili litahitaji kupandisha kwa asilimia 60-70% uzalishaji wa chakula duniani, au vinginevyo ili kukabiliana na changamoto ya midomo hiyo ya kuilisha, basi tuache tu kufuja chakula
 
Mkuu unachosema ni kweli,Ufujaji ni tabia mbaya sana.kwa sisi ambao tumewahi kulala na njaa tunaelewa hasa jinsi njaa inapouma.Natumaini ujumbe wako utaamsha hisia sahihi
 
Mkuu unachosema ni kweli,Ufujaji ni tabia mbaya sana.kwa sisi ambao tumewahi kulala na njaa tunaelewa hasa jinsi njaa inapouma.Natumaini ujumbe wako utaamsha hisia sahihi
Shukran
 
Back
Top Bottom