Mganga wa Kienyeji ashikiliwa Kwa Kudhalilisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mganga wa Kienyeji ashikiliwa Kwa Kudhalilisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 18, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  MGANGA wa kienyeji mmoja mkazi wa wilayani Nkasi mkoani Rukwa, anashikiliwa na polisi mkoani humo kwa tuhuma za kuwadhalilisha wanawake wawili kwa kutaka kufanya nao mapenzi bila ridhaa yao nakudai hayo ndiyo masharti ya dawa yao. Ilidaiwa kuwa mganga huyo alikuwa akiwapeleka wanawake hao katika msitu mmoja mkali na kuwavua nguo zote na kisha kuwachanja chale mwili mzima na kuwanyoa vinyoleo vilivyopo sehemu za siri.


  Ilidaiwa kuwa hiyo ndiyo ilikuwa ni kawaida yake ndani ya wiki moja katika zoezi la kuwaahidi akina mama hao kuwa hayo ndiyo yalikuwa masharti ya dawa yao ili waweze kufanikiwa.


  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage alisema matukio hayo yalikuwa ni ya nyakati tofauti tofauti moja likiwa mwishoni mwa wiki iliyopita na lingine mwanzoni mwea juma hili.

  Kamanda Mantage alifafanua kuwa tukio la kwanza lilitokea saa 10 jioni wakati mwanamke mwenye umri wa miaka 40 ambaye jina lake linahifadhiwa , mkazi wa kijiji cha Isunta kilichopo katika wilaya hiyo ya Nkasi aliyekuwa akisumbuliwa na maumivu ya tumbo pamoja na kuhara damu kwa muda mrefu alikwenda kwa mganga huyo kwa lengo la kupatiwa matibabu.


  Alisema alifika kwa mganga huyo kwa lengo la kupata tiba na kisha mganga huyo alimpeleka hadi katika msitu wa kijiji cha Mkangale kilichopo nje kidogo ya mji huo wa Namanyere kwa lengo la kumtengenezea dawa.


  Kamanda Mantage alisema kuwa inadaiwa kuwa mara baada ya kufika katika msitu huo mtuhumiwa huyo alimwamuru mama huyo kuvua nguo zote na kisha kuanza kumchanja chale mwili mzima na kumnyoa vinyweleo katika sehemu zake za siri.

  Alisema mara baada ya kumvua mama huyo nguo zote alimpaka dawa za kienyeji mwili mzima na kumuamuru mama huyo wafanya nae mapenzi kitendo mama huyo aligoma.


  Kamanda Mantage alifafanua kuwa baada ya mama huyo kukataa kufanya naye mapenzi ndipo mtuhumiwa huyo alipoanza kumtisha mama huyo kuwa ana uwezo wa kumletea nyoka ili aweze kumdhuru na ndipo mama huyo aliposhikilia msimamo wake na kisha kuvaa nguo zake na kukimbia na kumwacha mganga huyo porini.

  Alisema tukio la pili lilitokea siku mbili baada ya lile la kwanza saa 11 jioni ambapo pale mama mwingine mwenye umri wa miaka 64 mkazi wa kijiji cha Kipundu Kalla aliyekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mkono wake wa kulia.


  Alisema kuwa mama huyo alivuliwa shanga zake 24 na kupatiwa vitisho vingi kutoka kwa mganga huyo, lakini naye aling'ang'ania msimamo wake wa kutotaka kufanya nae mapenzi na mganga huyo.


  Alisema mara baada ya taarifa hizo kulifikia jeshi hilo, msako mkali ulifanywa mara moja na kufanikiwa kumkamata mganga huyo nyumbani kwake na katika hali ya kushangaza alikutwa akiwa amevaa shanga 139 kiunoni kwake na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa mganga huyo hakuwa na kibali cha chochote cha kumruhusu kuendesha shughuli za uganga wa jadi .


  Hata hivyo ilibainika kuwa wanawake hao wawili waliodhalilishwa na mganga huyo walikuwa wameolewa na waume zao hawakuwa na taarifa zozote za kwenda kupata matibabu kwa mganga huyo wa jadi.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3327730&&Cat=1
   
 2. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Waganga wa Aina hii, Sanaa Tupu!
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mh Mzidakaya anatokea huko eeehhhh
   
Loading...