Mganga wa kienyeji anayewasaidia majambazi akamatwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
JESHI la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kumkamata mganga wa kienyeji anayewasaidia majambazi toka jijini Dar es Salaam na Arusha kufanikiwa katika ujambazi huo
Mbali na kukamatwa na mganga huyo pia majambazi hao wapatao watano wamekamatwa katika msako huo uliofanywa na jeshila polisi kwa kushirikiana na kikosi cha pikipiki.

Watuhumiwa hao walinaswa wakiwa na bastola yenye risasi tisa, rungu, panga na tunguri, na dawa mabalimbali za kienyeji wakiwa kwenye harakati za kuvamia kwa mfanyabiashara mmoja maarufu wa Manispaa ya Arusha.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Leonard Paul, alisema majambazi hao walinaswa wakiwa katika baa ya Zumbukuku wakwia na mganga wao huyo, wakiendelea na vinywaji huku wakijiandaa kuvamia kwa mfanyabiashara huyo kwa lengo la kupora mali

Alisema majambazi hao, pia walikutwa na gari aina ya Toyota Corolla T 153 ANY iliyotarajiwa kutumika katika uporaji huo na pikipiki aina ya Honda XL 250 T 375 ATY ambayo huitumia kwa uchunguzi kabla ya kufanya ujambazi wao.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Halidi Omari (35) mkazi wa Kibonde maji jijini Dar es Salaam ambaye ndiye mganga wao wanayetembea nae, Frank Sikawa (40) Temeke, Fredy Mkenya (30) mkazi wa Sombetini Arusha, Gift Mushi (28) mkazi wa Sakina na Silasi Msechu (29) wa makao mapya mjini hapa.

Hivyo ilidaiwa baada ya mahojiano hayo walibainisha kuwa walikuwa wanasaidiwa na nmganga huyo kufanikisha katika ujam,bazi wao waliouanza kwa muda mrefu.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3580298&&Cat=1
 
Ni utata mtupu, kwani serikali inaamini mambo ya uchawi/uganga wa kienyeji? Taarifa kama hii katika majumuisho yake ni utata mtupu kwa wananchi, kwani serikali hiyo hiyo itasema kwamba haiamini mambo ya ushirikina halafu tena hiyohiyo imkamate mganga wa kienyeji ati anashirikiana na majambazi. Hii ina maana kwamba, kwa kuwa kitu kisicho aminika na serikali hakiwezi kutungiwa sheria. Hivyo pamoja na kwamba hata kama ni kweli anashiriki kufanikisha matukio ya ujambazi kwa utaalamu wake wa tunguli lakini akifikishwa mahakamani hana kesi ya kujibu.

Je serikali yapaswa kujipanga upya ki tamaduni zaidi?
 
tukubali kuwa polisi wetu bado sana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom