Mganga wa jadi kutoka Sumbawanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mganga wa jadi kutoka Sumbawanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ABEDNEGO, Jul 18, 2011.

 1. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Leo asubuhi toka ninatoke home Kibamba kwa Mkurya nimehesabu mabango ya Mganga wa jadi kutoka Sumbawanga hadi Ubungo kwenye mata yapata 19 ,Ni mabango tofauti yako kando ya barabara na moja pale Kimara Baruti liko kituoni kabisa,Sasa swali langu, Kwanza haya mabango wanalipia ushuru? Pili hawa waganga wa Sumbawanga ndiyo wana soko sana hapa Jijini? Na ni kwanini wajitangaze hivyo?Ina maana kwetu tuliotoka Sumbawanga ndiko chimbuko la uganga wa jadi????
   
 2. k

  kbhoke Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Wameandika mabango kadiri ya sehemu wanakotoka, maana hawaonei aibu taaluma yao. Ilikuwepo kabla ya dawa za kisasa kuwepo. Hawa ni tofauti na wale waliozika jadi zao kwa kutanguliza mbele jadi za wengine. Wanatoa fundisho la kujali jadi.
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Hao wote ni waongo, kuna mmoja nimewahi kwenda nikakuta ameyapanga madawa yake majina ya vijiji vya Sumbawanga. Alipogundua mimi ni wa huko akawa mkali na akanifukuza, kisa nilimsemesha kilugha kumbe hata sumbawanga hakufahamu. Kifupi ni kuwa wengi wanatumia Sumbawanga kujipatia wateja!
   
 4. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Siongezi wala sipunguzi. Posutaaa "mkombe".
   
 5. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kenya mabango kama hayo yanasema "Mganga kutoka Tanzania ".
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  "Taitu kalesa"
   
 7. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 841
  Trophy Points: 280
  kumbe kuna madili mengine yapo nje nje hivi! Wacha nitafute mahali pa kufikia.
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135  Waganga wa kishenzi (kienyeji) ndio hao hao wachawi na vigagula wanaoumiza wanadamu
   
 9. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Yani hakika hawa viganga ni mapumbavu sana,yani ningekuwa na uweza ningewasweka wote ndani.
   
 11. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 613
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  kwa msisitizo nchini kenya huyaandika mabango yao mganga kutoka Tanganyika
   
 12. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mkuu wewe unaonekana mkweli,tunaomba utueleze ulienda kufanya nini kwa mganga?
  1-kutaka kupandiswa cheo
  2-Dawa ya nguvu za kiume
  3-kumwita mpenzi wa mbali
  4-kuomba mganga usikatiwe umeme nyumbani kwako
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Jul 19, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Ahahahahaaah!! Nilipita tu kutoa salamu kwa kujua ni mtu wa nyumbani, kumbe ni tapeli!!
   
 14. Esperance

  Esperance JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna mwingine Bukavu kaandika anatoka Sumbawanga Namanyere wateja kibao.
   
 15. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Hawo ni wengi sana Jijini Dar kila kona Mganga kutoka Sumbawanga anatibu kiharusi,kisukari,Ukimwi,Mvuto wa mapenzi,Kurudishiwa mali ulizoibiwa nk nk Hawa ni matapeli wa kupindukia wanatumia Sumbawanga kama deal ,Kwani tunaaminishwa kuwa huko ndiko kiboko ya wachawi.Jamani kama jirani yako ni mganga wa kutoka Sumbawanga mweendee kwa mjumbe amtimue maana ndo wanadanganya vijana wetu kuwa vibaka kwani wakiwafanyia dawa hawakamatwi!!! Piga ua hao ni matapeli ya mjini tuu.
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jul 19, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Yaani hawa jamaa wanakera sana, mbona Sumbawanga kwenyewe hatuwaoni.....huku nako wanatudanganya kuna vibao vya waganga kutoka Tanga na Bagamoyo!!!
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Jul 19, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Ahahahahaaaah!!! Na Sumbawanga nako kuna waganga kutoka Kongo...utapeli tu!!
   
 18. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Aisee great thinker kumbe na wewe huwa unaitumiaga hiyo huduma ya nguvu za giza? Ina maana asingetumia majina ya vijiji vya sumbawanga au usingeshtuka ulikuwa upate huduma ya kimapepo pale?
   
 19. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,198
  Likes Received: 520
  Trophy Points: 280
  Ulienda kwa mmoja then ukahitimisha kuwa wote ni waongo ? Nafikiri mganga atakuwa anatibu magonjwa yanayoeleweka na wengi,inapokuja mgnga anatibu hata vyeo maofisini binafsi hapo naona ni utapeli tu,Naamini mganga wa kienyeji atakuwa anatibu magonjwa ambayo ni hakika yanajulikana,Malaria,pumu,TB nk.Lakini mganga anayemwita mpenzi,anarudisha mali iliyopotea,anaongeza mvuto na mengine mengi yafananayo na hayo Hakika hizo ni nguvu za giza wala si uganga.
  Tuwape heshima zetu waafrika wenzetu wanaojua tiba za asili za magonjwa yetu,tuache kuwabeza waganga wa asili wa ukweli.
   
 20. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Taitu kalesa, mwalinda uli?, katilumi.
   
Loading...