Mganga wa jadi kortini akidaiwa kutapeli Sh70 mil | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mganga wa jadi kortini akidaiwa kutapeli Sh70 mil

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Aug 5, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Mganga wa jadi kortini akidaiwa kutapeli Sh70 mil
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 05 August 2011 08:47 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Hadija Jumanne
  MGANGA wa jadi, Ismail Idd (42), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu shtaka la kutapeli na kujipatia Sh70 milioni kwa njia ya udanganyifu.
  Idd, ambaye ni mkazi wa Yombo Buza, alipandishwa katika mahakama hiyo jana kujibu shtaka hilo baada ya kumlaghai mlalamikaji, Oscar Kushi, kuwa ampatie fedha hizo ili azitengeneze na zitaongezeka maradufu, huku akijua ni uongo.
  Mwendesha mashtaka wakili wa serikali, Sakina Sinda, alidai mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Novemba mwaka jana mtaa wa Zanaki, Dar es Salaam.
  Ilidaiwa kuwa mshtakiwa, siku ya tukio saa 5:00 asubuhi eneo hilo, mshtakiwa alijipatia Sh70 milioni, mali ya Oscar Kushi.
  Sinda aliendelea kudai kuwa, mshtakiwa alijipatia fedha hizo kutoka kwa mlalamikaji baada ya kumlaghai kuwa, ana uwezo wa kutengeneza fedha za majini.
  Alidai kuwa huku akijua kuwa ni uongo, mshtakiwa aliendelea kumlaghai mlalamikaji kuwa, angemtengenezea fedha za majini zikawa zinakuja nyumba kwake kila anapokuwa na shida.
  Mshtakiwa alikana shtaka na Hakimu Karimu Mushi, aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 18, mwaka huu itakapotajwa tena.
  Mshtakiwa alirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakao saini nusu ya mali iliyoibwa.
  Katka kesi nyingine, Mkazi wa Kinondoni, Alex Katabazi (25), amefikishwa katika mahakama hiyo kujibu shtaka la wizi wa pikipiki.
  Mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali, Anuciatha Leopard, alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 29, mwaka huu eneo la Mnazi Mmoja, mtaa Indra Ghandi.
  Leopard alidai siku ya tukio saa 11:00 jioni, mshtakiwa aliiba pikipiki moja aina ya Bajaj yenye thamani ya Sh2.2 milioni, mali ya Samson Shikoya.
  Mshtakiwa alikana shtaka na Hakimu Janeth Kaluyenda aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 17, mwaka huu itakapotajwa tena.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  [h=4]Comments [/h]


  0 #4 mekaki 2011-08-05 11:09 pole...pole...pole...pole...akili ni mali..kwanini hiyo hela usingetafuta wataalamu hata mambo ya biashara ndogongo ukaizalisha..easy comes....easy goes..inaonekana kabisa hiyo hela si ya halali na kama ni ya dhuluma au y akiganga ukakiuka masharti basi imekula kwako...unapeleka hela yote hiyo kwa mganga bila hat maandishi wala shahidi? sasa itajulikanaje kama kweli ulimpa...acha akuruke maana hukutumia akili hata kidogo.jaribu kuwa na busara.kwanza dhna ninayopata wewe ni mchoyo na acha mungu akuadhibu kwa sababu hiyo...kwanini hiyo hela usingewasaidia nayo hata watoto wa shule?shame on you mungu amekuumbua....acha uone moto maana pesa za kutafut akwa ujanja huondoka kwa ujanja hivyo hivyo.na wengine nso waajifunze acheni kutegemea pesa zamashetani
  Quote

  0 #3 brian 2011-08-05 10:39 Unaweza uwe na hela na bado ukawa na akili za ovyo, kesho na kesho kutwa utamsikia mtu kama huyo oscar analalamika eti maisha magumu!!
  Quote

  0 #2 laiza 2011-08-05 09:20 Inawezekana kweli fedha zote milioni sabini mtu ukazihesabu moja mbili kumi ishirini mia elfu milioni hadi milioni sabini halafu ukamkabidhi mtu hivhivi? hapana tafadhali. Kama ukiniambia ulikuwa unampatia milioni mojamoja nitakubali lakini kwa milioni sabini kwa mpigo inabidi tukuhoji umepata wapi
  Quote

  0 #1 mimi 2011-08-05 08:51 Huyo aliyetapeliwa naye kama akili zake sufuri. Hivi milioni 70 umeshindwa kufikiri namna ya kuzalisha kijasiriamali? Crap!
  Quote
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  wajinga ndiyo waliwao..........................kama mganga anao huo uwezo kwa nini ahangaike kukusanya maburunkutu ya wengineoi?????????????? si angelijitengenezea za kwake akaishi raha mustarehe...............................anatafuta za wajinga kwa kuelewa ya kuwa hakuna lolote lile............
   
 4. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Bora ulivyojipigia na kucheza mkuu manake post za majukwaa mengine hazipati wachangiaji isipokuwa mmu na mambo ya kikubwa! Tukirudi kwa mada ni kwamba hiyo inaitwa "diabre" asili yake ni Nigeria na DRC, usiombe hawa jamaa wakakuingiza kwenye 18 zao! ni watu wanaotumia ndumba kwanza kukupumbaza unakuwa kama ndondocha kila watakalokuamrisha unafanya bila kufikiria. Utaambiwa uza mali zako lete hela tukutengezee zizae nyingi, nawe kama zuzu utafanya.Ila lazima anayetumiwa kwenye njama hizo ni ndugu yako au mtu wako wa karibu ndio anapeleka taarifa zako za awali kwao juu ya kiasi gani cha pesa au mali unamiliki, na huyo ndio atapewa madawa ya kukupumbaza ye aanze kukufanyia kabla ya kukutana nao
   
 5. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ama kweli akili ni nywele kila mtu ana zake. Duh yaani jamaa alipewa nusu kaputi nin?
   
Loading...