Mganga wa jadi BUJINGWA JOHN akamatwa kwa mauaji ya mwanafunzi KAGERA.

mende 2014

JF-Expert Member
Apr 13, 2014
763
131
Mganga huyo anashikiliwa kwa mauaji ya mwanafunzi Fausta wa shule ya msingi. Alimuita akiwa na wanafunzi wenzake na alippfika alimvuta hadi kwake na baadae Alimnyonga hadi kufa na kukata mkono wa kushoto, Sikio la kushoto na kumchuna ngozi na baada ya hapo alichimba kaburi uvunguni mwa kitanda chake na kumzika.Alipohojiwa alikiri kufanya tukio hilo kwa sababu ya umaskini ili atengenezee dawa za bahati za kuleta utajiri. Source COSMAS MAKONGO ITV.
 
Huyo ni mshenzi sana na anastahili kunyongwa wala sio kubembelezwa. Ametoa uhai wa mtu bila hatia so likewise auwawe.
 
Kwanza akatwe pumbu mikono asikie maumivu na yeye asikie maumivu yake ndipo anyongwe
 
Lol mganga John amefanya jambo la kikatili sana na yeye akatiliwe ivo ivo
 
Alimkata mikono na kumfukia chini ya kitanda

John-Mujinga-May24-2014(1).jpg

Mganga Mujingwa John akiwa na matunguli yake.picha ya kulia akionyesha jinsi alivyomkaba na kumnyonga mtoto mdogo pia kukata viungo vyake kisha kuchimba shimo chini ya kitanda chake na kuuzika mwili wa mtoto huyo.

Mtoto wa darasa la kwanza, Fausta Geofrey (8), ameuawa kikatili kwa kunyongwa na kukakatwa viungo na mganga wa kienyeji na mwili wake kuzikwa ndani ya nyumba.

Kwa mujibu wa Afisa mtendaji wa kijiji cha Bisole kata Muhutwe wilayani Muleba, Khamis Hassan, baada ya mauaji hayo, muuaji alimkata mtoto huyo mikono yake miwili kabla ya kumzika.

Hassan alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 21, asubuhi katika kijiji hicho wakati mtoto huyo akiwa na wenzake wakielekea shuleni. Inadaiwa kuwa mtoto huyo aliitwa na kukamatwa na mganga huyo Mujingwa John (20).

Alisema kuwa baada ya taarifa za mtoto huyo kutoonekana kuzagaa, wanakijiji walikusanyana na kuanza msako ambapo walikamata kundi la vijana wanaohofiwa kuhusika na tukio hilo.

Alisema baada ya kukamata watu hao waliwaweka sehemu moja na kuwaita wanafunzi waliokuwa na marehemu ambapo walimtambua mganga huyo kuwa ndiye aliyemwita na kumkamata mtoto huyo.

Mtendaji huyo alisema kuwa baada ya mganga huyo kutambuliwa, wananchi na polisi waliofika eneo hilo waliondoka naye hadi katika nyumba anamoishi na kumtaka awaonyeshe alipo mtoto huyo.

Alisema baada ya kumbana aliwaonyesha sehemu alikomzika ambapo walichukua jembe na kufukua maiti ya mtoto huyo iliyokuwa imezikwa ndani ya nyumba.

Alisema baada ya mganga huyo kumuua mtoto huyo, alimkata mikono yake miwili na kisha kuchimba shimo ndani ya nyumba na kumzika ambapo shimo alitandaza nyasi na juu akaweka kitanda.

Alisema kuwa alipohojiwa ili kujua nani kamtuma kutekeleza unyama huo, mganga huyo alisema kuwa aliota mizimu yake ikimtuma kumuua mtoto ili amkate viungo vyake kwa ajili ya kuchanganya na dawa.

Alisema kuwa mikono hiyo alitaka kuibanika kwenye moto ili aichanganye na dawa ambayo angewapatia watu wanaohitaji kupata utajiri.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera, George Mayunga, alisema kuwa mganga huyo alikamatwa na polisi kwa kushirikiana na wananchi ambapo alikutwa akibanika viungo alivyomkata mtoto huyo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwa kujiamini, mganga huyo alisema amefikia hatua hiyo kutokana na hali ngumu ya umaskini inayomkabili.

Alisema baada ya kumkamata mtoto huyo alimkaba shingo na kumvuta hadi katika nyumba alimokuwa akiishi, akamnyonga hadi kufa na baada ya kufa alimkata ngozi ya mgongoni, mkono wa kushoto anaodai una bahati, sehemu za siri na masikio.

"Nilikamata mtoto na kumuua maana niliona nikikamata mtu mzima atanizidi nguvu," alisema mganga huyo.
Alisema alipohakikisha amemuua alichimba shimo chini ya kitanda chake akamzika na kutandaza nyasi juu yake ili isigundulike kama eneo hilo kuna shimo.

Mganga huyo alisema viungo hivyo ambavyo hadi polisi wanafika alikuwa bado akivikausha angevichanganya na dawa ambayo angewapatia wateja wake ili iwasaidie kufanikisha mambo yao ikiwamo kupata bahati na utajiri.

Alisema yeye kabila lake ni Msukuma na kuwa ni mara yake ya kwanza kufanya tukio kama hilo ambapo alihamia kutoka mkoani Mwanza eneo la Nyanguge, wilaya ya Magu na kuhamia wilayani Muleba miaka miwili iliyopita.

Alisema alirithi uganga huo kutoka kwa babu yake mzaa mama na kuwa alianza kuwa mganga akiwa na umri wa miaka minane na hajawahi kwenda shule.

SOURCE: NIPASHE
 
WAKATI jamii ya Watanzania ikipigwa butwaa na
ukatili wa kutisha aliofanyiwa mtoto wa miaka
minne kwa kufungiwa ndani ya boksi kwa miaka
mitatu mjini Morogoro, ukatili mwingine wa kutisha
dhidi ya watoto umeripotiwa mkoani Kagera.
Katika mkoa huo, mganga wa kienyeji ametiwa
mbaroni, akituhumiwa kumuua kwa kumnyonga,
kumkata mikono na kumzika katika nyumba yake.
Mganga huyo, Mujingwa John (20) amekiri mbele ya
jeshi la polisi kuhusika na mauaji ya mtoto Fausta
Geofrey (8), mwanafunzi wa darasa la kwanza
katika Shule ya Msingi Kitunga kata ya Muhutwe,
wilayani Muleba.
Anatuhumiwa kwamba, alimkamata kwa nguvu
akienda shule na wenzake, akamuua, kumkata
mikono, nyama ya mgongo, masikio na sehemu za
siri kwa lengo la kuibanika na kutengeneza 'uchawi’
wake, kisha akachimba shimo na kuzika mwili ndani
ya nyumba.
Tukio hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa
wa Kagera, George Mayunga aliyesema mganga
huyo alikamatwa na polisi kwa kushirikiana na
wananchi, ambapo alikutwa akibanika viungo
alivyovikata kutoka kwa mtoto huyo.
Aidha, akiwa polisi, mganga huyo alipewa fursa ya
kueleza kilichotokea mbele ya waandishi wa habari,
ambapo alidai alifikia uamuzi wa kumuua mtoto
huyo, kutokana na hali ngumu ya umaskini
inayomkabili.
Alisema baada ya kumkamata mtoto huyo, alimkaba
shingo na kumvuta hadi katika nyumba aliyokuwa
akiishi, akamnyonga hadi kufa na baada ya kufa,
alimkata ngozi ya mgongoni, mikono akianzia na
mkono wa kushoto aliodai una bahati, sehemu za
siri na masikio.
“Nilimkamata mtoto na kumuua, maana niliona
nikikamata mtu mzima atanizidi nguvu na kupiga
kelele,” alidai.
Alidai kuwa, “Nilipomaliza kumuua nilichimba shimo
chini ya kitanda changu nikamzika na kutandaza
nyasi juu yake ili isigundulike kama eneo hilo kuna
shimo".
Mganga huyo aliyejitambulisha kuwa ni Msukuma,
alidai viungo hivyo ambavyo hadi polisi wanafika,
alikuwa bado akivikausha, angevichanganya na dawa
ambayo angewapatia wateja wake ili iwasaidie
kufanikisha mambo yao, ikiwamo kupata bahati na
utajiri na alitarajia kuuza kwa Sh 500 kwa kila
ujazo wa kijiko kimoja cha dawa yake.
Alisema hiyo ni mara yake ya kwanza kufanya tukio
la aina hiyo na kwamba alihamia Muleba mkoani
Kagera miaka miwili iliyopita akitokea Nyanguge
wilaya ya Magu mkoani Mwanza. Alisema alirithi
uganga huo kutoka kwa babu yake mzaa mama na
kuwa alianza uganga akiwa na umri wa miaka
minane na hakuwahi kwenda shule.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bisole katika Kata hiyo
wilayani Muleba, Khamis Hassan, akizungumzia tukio
hilo baada ya mauaji hayo, alidai muuaji alimkata
mtoto huyo mikono yake miwili kabla ya kumzika.
Hassan alisema kuwa tukio hilo ni la Mei 21 mwaka
huu asubuhi katika kijiji hicho, wakati mtoto huyo
akiwa na wenzake wakielekea shuleni, ambapo
inadaiwa aliitwa na kukamatwa na mganga huyo,
aliyetambulika kwa jina la Mujingwa John (20).
Alisema kuwa baada ya taarifa za mtoto huyo
kutoonekana kuzagaa, wanakijiji walikusanyana na
kuanza msako, ambapo walikamata kundi la watu
waliokuwa wakiwahofia kuhusika, hasa vijana.
Alisema baada ya kuwakamata watu hao,
waliwaweka sehemu moja na kuwaita wanafunzi
waliokuwa na marehemu, ambapo walimtambua
mganga huyo kuwa ndiye aliyemwita na kumkamata
mtoto huyo.
Mtendaji huyo alidai baada ya mganga huyo
kutambuliwa, wananchi na polisi waliofika eneo hilo,
walikwenda naye hadi katika nyumba anayoishi na
kumtaka awaonyeshe alipo mtoto huyo. Alidai
baada ya kumbana, aliwaonesha sehemu alikomzika,
ambapo walichukua jembe na kuanza kufukua mwili
wa mtoto huyo, uliokuwa umezikwa ndani ya
nyumba aliyoishi mganga huyo.
Alidai baada ya mganga huyo kumuua mtoto huyo,
alimkata mikono yake miwili na kisha kuchimba
shimo ndani ya nyumba, ambapo baada ya kumzika
alifukia shimo akatandaza nyasi juu yake na kisha
kuweka kitanda chenye godoro alilokuwa akilala.
Alisema kuwa alipohojiwa ili kujua nani kamtuma
kutekeleza unyama huo, mganga huyo alidai
ilitokana na yeye kuoteshwa na mizimu yake,
iliyomtaka kumuua mtoto ili amkate viungo vyake
kwa ajili ya kuchanganya na dawa.
Alisema mikono hiyo alitaka kuibanika kwenye moto
ili aichanganye na dawa, ambayo angewapatia watu
wanaohitaji kupata utajiri. Tukio hilo limekuja siku
chache wakati Jeshi la Polisi mkoani Morogoro,
likiendelea na uchunguzi wa kilichotokea mpaka
mtoto mmoja mkoani hapa , akateswa na mama
mlezi kwa kuwekwa katika boksi tangu akiwa na
miezi tisa, mpaka alipotimiza miaka minne.
 
Kuishi kanda ya ziwa tabu sna.sijui hawa watu hawajaenda shule mana matukio yao yanatisha.
 
Kuishi kanda ya ziwa tabu sna.sijui hawa watu hawajaenda shule mana matukio yao yanatisha.

Binafsi naishi kanda ya ziwa lakini hili swala ni la kitaifa, Mbeya,Sumbawanga,mtwara na hata huko kwenu hii tabia ipo.

Huu ni unyama wa kutisha,sijui mamlaka husika wana mkakati gani kukomesha hii tabia.Ukatili kwa watoto sasa imekuwa jambo la kawaida kwenye jamii yetu.Inabidi zitungwe sheria kali kwa ajili ya watu kama hawa.
cleardot.gif
 
Na kabla hajanyongwa atufuliwe macho wapewe mmbwa wayale.

Afanye huo uganga wake police wamwachie sasa
 
Duuuuuu, hyo kali najua wapo waliomtuma awatengenezee dawa kwa ajili ya 2015 ILA hata akiwataja kazi bure hitimisho uganga wa kienyeji marufuku TZ
 
Back
Top Bottom