Mganga mtengeneza vibali kwenda nje ya nchi

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
7,420
7,080
Je wewe ni mfanyakazi wa serikali na umeathirika na katazo la kutosafiri kwenda nje ya nchi kwa makongamano, semina elekezi na Mikutano? Mganga Maarufu toka Zanzibar anakuhakikishia safari kadhaa nje ya nchi kila mwezi kwa malipo yafuatayo;
Nchi za Afrika Mashariki (Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi & S. Sudan) = 50,000 (T.Shs).
Kusini & Afrika Magharibi (S. Africa, Botswana, Nigeria, Ghana) = 75,000/=
Asia (China, UAE, Oman & Thailand) = 100,000/=
Ulaya (UK, Netherlands, Germany, Turkey) =120,000/=
America (USA & Canada) =150,000/=
NB: Tuna Uzoefu wa kutosha tumefanikisha safari kadhaa za watumishi wa umma wakiwemo viongozi mashuhuri, MAJIBU NDANI ya SAA 12
UBORA: ISO 9001:2001 Certification
MAWASILIANO: 0777850004
 
Je wewe ni mfanyakazi wa serikali na umeathirika na katazo la kutosafiri kwenda nje ya nchi kwa makongamano, semina elekezi na Mikutano? Mganga Maarufu toka Zanzibar anakuhakikishia safari kadhaa nje ya nchi kila mwezi kwa malipo ya 50,000 tu (T.Shs).
MAWASILIANO: 0777850004
Anza wewe ukirudi ndio utangaze
 
mkuu binafsi nakumbuka tulikuwa tunakula shushu training DUBAI mwezi mzima, tiketi EMIRATES, per diems nene kila siku x 30 days =....... USD.
 
Tatizo siyo kibali tatizo ni visa lazima serikali wakuombee.

Au anatoa na viza.
 
kibali mpaka kitoke lazima uwe na sababu lukuki bora sangoma umeturahisishia
 
Loh watu na fursa...kwake kutafurika na itabidi awe na mtu maalum wa kupokea simu
FURSANKILA SEHEMU KAKA MSHANA

LEO KKKT TUMETANGAZIWA MAKANISAN NDOA SASA WATAKUWA WANALIPA LAKIMOJA BW N BIBI KWA SEMINA SIJUI ANAEFUNDISHA ANATOKEA MBINGUNI AZITOACHANA

MBAYA ATI UKANDA WA PWAN WANAKWENDA AZANIA FRONT WOTE KAMA SIO UTAPELI N NN ...LOH
 
Back
Top Bottom