Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Makubi: Wananchi chukueni tahadhari za kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya magonjwa, msisubiri matamko

Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
2,938
2,000
Mganga Mkuu wa Serikali Prof Abel Makubi amewataka watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kadhalika wajikinge wenyewe na kuwakinga wengine.

Makubi amesisitiza kuwa hizi siyo nyakati za kusubiri matamko wakati unaona kabisa mbele kuna nyoka, jiongeze chukua tahadhari.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

----
Serikali ya Tanzania imetoa maelekezo jinsi ya kuchukua tahadhari kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.

Tamko hilo lililotolewa Jumatano Februari 10, 2021 na mganga mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi aliyeeleza kuwa magonjwa hayo ni yale yanayosababishwa na vimelea vya bakteria, virusi na wadudu mbalimbali na huambukiza kwa njia mbalimbali.

Ameyataja magonjwa hayo kuwa ni kuhara, homa za mapafu, kifua kikuu, mafua, malaria, dengue, homa ya bonde la ufa na kufafanua kuwa baadhi ya magonjwa ya kuambukiza yanaenda na vipindi vya majira ya mwaka au kutokea kwa mlipuko.

Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanawahi katika vituo vya afya mara tu wanapoona dalili za kuugua kwa namna yoyote mfano kuchoka, homa, kukosa hamu ya kula, mwili na kichwa kuuma na kwamba hiyo itasaidia mtoa huduma kumhudumia mhusika kwa wakati kabla mwili haujachoka na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kupona.

Profesa Makubi amewataka wananchi kuzingatia usafi wa mwili wa mtu binafsi, kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka kwa kutumia sabuni katika maeneo ya kazini, shuleni, vyuoni na nyumba za ibada.

Pia, kuhakikisha wanakunywa maji yaliyochemshwa kuanzia nyumbani na kila sehemu ikiwemo mahala pa kazi, kunawa kwa sabuni na maji tiririka mara baada ya kutoka maliwatoni au wanaposhika uchafu katika mazingira yoyote.

“Faida za utekelezaji wa usafi ni kujikinga na maambukizi kutoka mikononi kuingia ndani ya mwili kupitia mdomo, pua, ngozi.

Utekelezaji wa mkakati huu umeleta matokeo chanya kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita ambapo sasa nchi yetu haijapata visa vya kipindupindu,” amesema.

Kuhusu kuzingatia usafi wa mazingira pamoja na kuhakikisha nyumba zinakuwa safi amesema, “utekelezaji huu utakinga dhidi ya magonjwa ya mafua, homa ya mapafu, malaria, kifua kikuu.

Na matokeo yake ni mwili kuepuka kushambuliwa na maradhi yanayozuilika hivyo nguvu ya mwili kujikinga na maradhi kubaki kuwa imara muda wote.”

Katika tamko hilo, wananchi wametakiwa kuimarisha kinga za mwili pamoja na afua tajwa ambazo zinalinda kinga ya mwili kutotumika vibaya kutokana na kushambuliwa na maradhi ya mara kwa mara hususan yanayozuilika.

Nyingine ni kuzingatia lishe bora kuongeza kuimarika kwa kinga ya mwili akitaja vyakula kama mboga za majani, vyakula visivyo na sukari nyingi, matunda na maji kadri ya mahitaji ya mwili.

“Kufanya mazoezi ya mwili na viungo ni nguzo muhimu katika kujenga nguvu ya mwili kuimarisha mifumo ya hewa na mapafu, moyo na mzunguko wa damu.

Kuimarisha zaidi kinga dhidi ya magonjwa yanayoshambuliwa maeneo haya ya mwili na kujenga kinga yenye nguvu zaidi,” amesema.
It is an alarm and confirmation that Corona-19 and other related diseases are with us in plenty. Please take care. Observe social distance, put on the mask, use sanitizers, etc.
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,067
2,000
Hasa hao walioko bungeni ,kwenye mkusanyiko mmoja kwa zzaidi ya wiki mbili na ni watu wa umri kidogo wachukue taadhari aisee.
 
Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,764
2,000
Unasubiri tamko kwani mwili wako ni wa serikali,ukifa wanazaliwa wengine,we endelea kusubiria tamko.
 
Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
6,188
2,000
Nyie ndio kwenye mtihani mkiulizwa Lagos iko nchi gani, mnajibu Brazil.
Sawa jomba Cha msingi chukua tahadhari usiwe bwege na kuleta hoja zisizo na umuhimu...una behave Kama mtoto wa darasa la kwanza
Inaaminika kabisa kuwa Mungu husikia maombi ya watu; lakini hapendi watu hao hao aliowaumba kwa mikono yake wajimwambify badala ya kumtukuza yeye.Hivyo Anaweza kuwa kawithdraw maombi yetu.Lakini amejaa rehema kama tutapaangalia tulipojikwa.Kumbuka hata nchi zingine ziliamini kuwa Mungu amesikia maombi ya Tanzania
Kwani uongo jomba..kirusi Cha mwanzo Mungu alikiteketeza...kupitia maombi...ya watanzania..uongo??? Sasa subiri hiki kirusi Cha pili...kwa imani ileile Mungu ataenda kukisambaratisha...kuwa mtu wa imani jomba usiyumbishwe na mashetani hayo
 
Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
6,188
2,000
serikali isiyojali wananchi wake wakati wa majanga ni hii serikali nguruwe ya CCM.
Nadhan nguruwe ni wewe...mpumbaf mmoja tu usiyejielewa na shoga...wananchi asilimia zaidi ya 90 tumemkubal Magu na serikali..Sasa wananchi gani unaosema wewe...nguruwe pori
 
Bulamba

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
11,697
2,000
Mganga Mkuu wa Serikali Prof Abel Makubi amewataka watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kadhalika wajikinge wenyewe na kuwakinga wengine.

Makubi amesisitiza kuwa hizi siyo nyakati za kusubiri matamko wakati unaona kabisa mbele kuna nyoka, jiongeze chukua tahadhari.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

----
Serikali ya Tanzania imetoa maelekezo jinsi ya kuchukua tahadhari kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.

Tamko hilo lililotolewa Jumatano Februari 10, 2021 na mganga mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi aliyeeleza kuwa magonjwa hayo ni yale yanayosababishwa na vimelea vya bakteria, virusi na wadudu mbalimbali na huambukiza kwa njia mbalimbali.

Ameyataja magonjwa hayo kuwa ni kuhara, homa za mapafu, kifua kikuu, mafua, malaria, dengue, homa ya bonde la ufa na kufafanua kuwa baadhi ya magonjwa ya kuambukiza yanaenda na vipindi vya majira ya mwaka au kutokea kwa mlipuko.

Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanawahi katika vituo vya afya mara tu wanapoona dalili za kuugua kwa namna yoyote mfano kuchoka, homa, kukosa hamu ya kula, mwili na kichwa kuuma na kwamba hiyo itasaidia mtoa huduma kumhudumia mhusika kwa wakati kabla mwili haujachoka na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kupona.

Profesa Makubi amewataka wananchi kuzingatia usafi wa mwili wa mtu binafsi, kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka kwa kutumia sabuni katika maeneo ya kazini, shuleni, vyuoni na nyumba za ibada.

Pia, kuhakikisha wanakunywa maji yaliyochemshwa kuanzia nyumbani na kila sehemu ikiwemo mahala pa kazi, kunawa kwa sabuni na maji tiririka mara baada ya kutoka maliwatoni au wanaposhika uchafu katika mazingira yoyote.

“Faida za utekelezaji wa usafi ni kujikinga na maambukizi kutoka mikononi kuingia ndani ya mwili kupitia mdomo, pua, ngozi.

Utekelezaji wa mkakati huu umeleta matokeo chanya kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita ambapo sasa nchi yetu haijapata visa vya kipindupindu,” amesema.

Kuhusu kuzingatia usafi wa mazingira pamoja na kuhakikisha nyumba zinakuwa safi amesema, “utekelezaji huu utakinga dhidi ya magonjwa ya mafua, homa ya mapafu, malaria, kifua kikuu.

Na matokeo yake ni mwili kuepuka kushambuliwa na maradhi yanayozuilika hivyo nguvu ya mwili kujikinga na maradhi kubaki kuwa imara muda wote.”

Katika tamko hilo, wananchi wametakiwa kuimarisha kinga za mwili pamoja na afua tajwa ambazo zinalinda kinga ya mwili kutotumika vibaya kutokana na kushambuliwa na maradhi ya mara kwa mara hususan yanayozuilika.

Nyingine ni kuzingatia lishe bora kuongeza kuimarika kwa kinga ya mwili akitaja vyakula kama mboga za majani, vyakula visivyo na sukari nyingi, matunda na maji kadri ya mahitaji ya mwili.

“Kufanya mazoezi ya mwili na viungo ni nguzo muhimu katika kujenga nguvu ya mwili kuimarisha mifumo ya hewa na mapafu, moyo na mzunguko wa damu.

Kuimarisha zaidi kinga dhidi ya magonjwa yanayoshambuliwa maeneo haya ya mwili na kujenga kinga yenye nguvu zaidi,” amesema.
Kha kudadeki Wizara imejikita na miti shamba
 
Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
10,534
2,000
Sawa jomba Cha msingi chukua tahadhari usiwe bwege na kuleta hoja zisizo na umuhimu...una behave Kama mtoto wa darasa la kwanza

Kwani uongo jomba..kirusi Cha mwanzo Mungu alikiteketeza...kupitia maombi...ya watanzania..uongo??? Sasa subiri hiki kirusi Cha pili...kwa imani ileile Mungu ataenda kukisambaratisha...kuwa mtu wa imani jomba usiyumbishwe na mashetani hayo
Bado nasema, ni watu kama ninyi mliopewa akili nzuri tu na Mungu kupambanuaukweli na hatari mbele yenu, badala ya kuchukua hatua stahiki mnapiga magoti na kuomba miujiza.
Watu wengi wameshakufa kwa ujinga huu wa kukosa maarifa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom