Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Makubi: Wananchi chukueni tahadhari za kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya magonjwa, msisubiri matamko

Nyie wabishi mnaosubiri Jina hilo... Ngoja iwatandike ndo mtajua umuhimu wa kuchukua tahadhari. Ujumbe unaeleweka prof... waache ufipa kama wao hawataki mungu atawaadhibu.
 
Tumekuelewa. "Mwenye macho haambiwi ona" ni kauli fulani ya tahadhari kusema ukweli na hapo hapo kutomuudhi mzee. balance statement, japo kitaalamu alitakiwa aongee facts wazi tatizo 1, 2, 3 kama Daktari mkuu.
 
Kwanini huwa wanajitokeza kwenye media kinapotokea kipindupindu? Wajibu wake kama kiongozi ni nini kama siyo pamoja na kuufahamisha umma juu ya mambo ya kiafya yanayohatarisha watu anaowatumikia?

Suala la kujikinga wenyewe wananchi wanalitambua na wala hawahitaji kukingwa na serikali, wananchi wanahitaji kupewa taarifa rasmi na chombo chao rasmi kwakuwa wakati mwingine hutokea taarifa za kizushi na serikali hukanusha.
 
Prof ktk ubora wake, ila mjanja sana. Nimesoma maelezo sijaona mahali alipofunguka na kutaja ugonjwa wa Corona ( covid 19),au ndiyo kauwasilisha kama Homa ya mapafu? Hahahaaa!
 
Prof ktk ubora wake, ila mjanja sana. Nimesoma maelezo sijaona mahali alipofunguka na kutaja ugonjwa wa Corona ( covid 19),au ndiyo kauwasilisha kama Homa ya mapafu? Hahahaaa!
Magonjwa ya kuambukiza unaelewa maana yake!
 
naapa ukiwasikiliza wanasiasa wetu hawa watakupeleka kaburini siku sio zako. Kadhalika ukiwasikiliza wataalamu wetu wa afya nao watakupeleka hukohuko!

Sijui kwanini wanasiasa hatawataki kuwa wazi na kusema ukweli! sijui kwanini wataalamu wa afya hawataki kuwa wazi kwa mujibu wa taaluma zao!
 
naapa kwa jina langu,kuanzia leo thread za Corona basi..sita coment tena.maana kila siku Ni zile zile,juz Jana na Leo na kesho na.....na kuendelea.mnaoniunga mkono kwenye huu mgomo weka like hapo.mgomo unaanza rasmi kesho saa kumi na mbili asbh.
 
Tatizo jingine kuchukua hatua za kujikinga, kwanini watu wakichukua hatua za tahadhari wenyewe Serikali inatumia nguvu kubwa sana kuzipinga hizo tahadhari.

Watu wanalazimishwa kuomba radhi kwa kutoa tahadhari.

Watu wanalazimishwa kuvua barakoa.
 
Kila watu wana wajibu..., kila kiumbe ana wajibu wa kujilinda yeye na kutowaweka wenzake hatarini...

Na taasisi zenye majukumu ya afya na wananchi na zile zinazochukua pesa zetu / kodi ili zizitutumikie zina wajibu wa kutoa miongozo / elimu kwa watu ili waendelee kulinda afya zao, mfano suala la pneumonia kuzidi wana plan B za watu wakizidiwa kuhakikisha kwamba wanapata huduma zote wafikapo hospitali...., in short facilities zinatosha ?

Kama ilivyo wataalamu wa hali ya hewa kuwaeleza watu wanategemea kuna mvua itatokea ndivyo Taasisi ya afya inabidi iwe inatupa mirejesho kuhusu afya za jamii..., sasa kama wanapiga kimya tu, na watu wanatafuta habari wanadhani watu watazitoa wapi kama sio vijiweni ?
 
Jaribu kuufikirisha ubongo wako kwenye side nyingine, fikiria wao wanachukua tahadhari lakini wanakufa vile wewe ambaye uchukui tahadhari utakuaje
THE BEST ANSWER! Wao wanachukua kila aina ya tahadhari pamoja na huduma bora za afya daraja la kwanza lakini wanakufa. Je, sisi ambao huduma zenyewe ni sifuri si ndio tulipaswa kuchukua tahadhari mara elfu kuliko wao? Badala yake tunajiendea kama kuku tu! Asante Chief!
 
Kwahiyo sasa wanakubali kuwa mbele kuna nyoka sio na tahadhari ni Muhimu?

Sasa naomba niwaulize wale wote waliokuwa vimbelembele humu ndani kupinga kuwa Tanzania kuna corona na hali ni Mbaya, bado msimamo wao ni huo tu?
... wanasemaga kenge hasikii hadi damu zimtoke Mkuu. Matone mekundu yameanza kuonekana somo limeanza kueleweka japo kwa kuchelewa sana. Maana maprofesa waliofyekwa juzi kati sio mchezo ukiacha sisi makapuku tusio na media coverage.
 
Mbona Corona ilipoingia mwaka jana walitoa matamko tena mengi kwelikweli .... iweje leo wanasema tusisubiri matamko.

Matamko ya wataalamu yanasaidia sana kuwaelewesha watu kipi ni kweli na nini cha kufanya. Kwa sasa hiyo misiba inayoendelea ndiyo itakuwa ni SUPER SPREADER events!!
 
Wewe acha ujinga wewe Kama huwasikilizi wataalam wa afya na madaktari shauri yako...watanzania wote tunazingatia miongozo yao..usiendelee kwa punguwani jomba kwa kukosa maarifa
Inaaminika kabisa kuwa Mungu husikia maombi ya watu; lakini hapendi watu hao hao aliowaumba kwa mikono yake wajimwambify badala ya kumtukuza yeye.Hivyo Anaweza kuwa kawithdraw maombi yetu.Lakini amejaa rehema kama tutapaangalia tulipojikwa.Kumbuka hata nchi zingine ziliamini kuwa Mungu amesikia maombi ya Tanzania
 
THE BEST ANSWER! Wao wanachukua kila aina ya tahadhari pamoja na huduma bora za afya daraja la kwanza lakini wanakufa. Je, sisi ambao huduma zenyewe ni sifuri si ndio tulipaswa kuchukua tahadhari mara elfu kuliko wao? Badala yake tunajiendea kama kuku tu! Asante Chief!
Sasa Waziri mwenyewe wa Afya ambaye pia ni Daktari pia anapigia debe kujifukiza tu as if hiyo ndiyo tiba halisi!! Amesahau science inasema nini kuhusu huu ugonjwa!

Kwa hali ilivyo ni muda sasa kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima na kutoa maximum namba kwenye kila mkusanyiko, social distancing na kwenye vyombo vya usafiri. Pia wahimize hand sanitation kila mahali maana watu hawawezi kutembea na sanitizers kila wanapokwenda. Bila serikali kusema hayo hayatafanyika kila mahali!
 
Magonjwa ya kuambukiza unaelewa maana yake!
Naelewa mkuu. Nashindwa kuelewa kwa nini msomi huyo ana move around the circle na kufanya ulimi usiwe rafiki kutamka the current pandemic desease inayotumaliza aka corona. Anataka wananchi waanze tena kuulizia maswali? Kuna tatizo si bure.
 
Back
Top Bottom