#COVID19 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, Tumbi Hospital adaiwa kulazimisha watumishi kuchanjwa kinyume na hiari yao

Pumbav, tangu lini majaribio ya chanjo yakalazimishwa......majaribio mara zote ni jambo la kuomba ridhaa kutoka kwa wahusika baada ya kuwapa maelezo yote kuhusu majaribio kwa uwazi, hii inajulikana kwa kimombo kama 'informed consent' .Jambo jingine, majaribio kama haya ya kitabibu ambayo mhusika anaweza kupata madhara ya muda mrefu na mfupi au hata kupelekea kifo ni lazima kulipa wahusika waliojitolea fidia, huyo daktari anayelazimisha watu kushiriki kwenye jaribio la chanjo apimwe mkojo mara moja.......
 
Zoazi la kuzuia kuambukizana limeshindikana mfano hapa Dar tu level seat imewashinda kusimamia halafu et tunataka kulazimishana hivyo vichanjo milioni moja et kwa ajili ya kinga!
Wenzetu huko waliweka hadi Lockdown ili kudhibiti maambukizi wamekuja kufungua baada ya kuchanja watu wao kwa wingi ila sisi tumeachia watu waambukizane watakavyo halafu et tunataka kulazimishana hivyo vichanjo vichache et kwa ajili ya kinga, waseme tu wameona zinakaribia ku expire basi ndio maana wanataka kuzimaliza.
ajenda za siri
 
Kuna vitu vinashangaza sana kwa wasomi wetu wa kada ya afya....

Hawa wako vitani....mstari wa mbele kabisa....inakuwaje kukataa chanjo ilihali wako maeneo hatarishi tena wanawatibu wagonjwa wa UVIKO 19?!!!

#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#TujitokezeniKuchanjwa
Jua kwamba hawaamini uwepo wa Corona na wana siri nyingi juu ya hiki unachoambiwa Corona ni hatari. Sina Tz tu,sehemu nyingi watumishi wa umma wanalazimishwa kuchanjwa.
 
Itakuwa upumbavu kwa watumishi wa sekta ya afya kukataa kuchanja wakati wao wapo katika mazingira hatarishi ya kuambukizwa Covid-19 kuliko kada yoyote. Ilipaswa iwe lazima.
Inachekesha sana nchi hii yaani dr anapinga chanjo ndiyo maana wahudumu wa afya nchi hii waliowengi wanakufa na ukimwi.
Dr anajua madhara ya kutembea peku lakini ndiyo wanaongoza kupiga kavu
 
Ni mpumbavu peke yake ndiye atakayewalaumu wafanya kazi wa wizara ya afya wakikataa kuchanja kwa kuwa wana nafasi ya kusikia propaganda, kuona matokeo ya chanjo ya muda mfupi, na scientific confidence juu ya uwiano wa madhara na faida za chanjo hiyo kwa muda mfupi na muda mrefu.
Unaongelea hawa wataalamu wetu ambao wanakalili vitini vya wazungu?
 
Kuna vitu vinashangaza sana kwa wasomi wetu wa kada ya afya....

Hawa wako vitani....mstari wa mbele kabisa....inakuwaje kukataa chanjo ilihali wako maeneo hatarishi tena wanawatibu wagonjwa wa UVIKO 19?!!!

#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#TujitokezeniKuchanjwa
Chanjo zote za COVID 19 zilizopo sasa bado ziko kwenye clinical trial ndiyo maana ni lazima usaini makubaliano na ndiyo sababu hairuhusiwi kumchanja mtu chini ya miaka 18 kwa kuwa kisheria hawezi kuingia kwenye makubaliano ya kisheria. Be informed Jumbe Brown kama umechanja tunashukuru ili uwe mmoja wa wananchi waliojitolea kufanyiwa majaribio ya chanjo ya Covid 19
 
Inachekesha sana nchi hii yaani dr anapinga chanjo ndiyo maana wahudumu wa afya nchi hii waliowengi wanakufa na ukimwi.
Dr anajua madhara ya kutembea peku lakini ndiyo wanaongoza kupiga kavu
Kama anajitambua je? Chanjo ya majaribio sio lazima kuchanjwa ila chanjo zote zilizokamilika huwa ni lazima kuchanjwa ndiyo maana huwa hakuna kusaini makubaliano ya kisheria na zinachanjwa hadi watoto wadogo lakini hizi za majaribio mtoto ni marufuku kuchanjwa.
 
Conspiracy theories....

Kwa hiyo hata hizi chanjo dhidi ya magonjwa ya watoto ,huyo beberu anatumaliza nazo?!!!

Tunameza vidonge vya UKIMWI kila siku kwa hiyo beberu anatuchakaza nazo?!!

Tunakunywa soda kama COCACOLA NA PEPSI..."materials" yanatoka nje...kwa hiyo BEBERU HUYO anatumaliza eeee?!!!
Wenyemashaka na hizo chanjo za uviko wanasema hazikukamilisha mchakato wa utafiti tofauti na hizo nyengine.
 
Itakuwa upumbavu kwa watumishi wa sekta ya afya kukataa kuchanja wakati wao wapo katika mazingira hatarishi ya kuambukizwa Covid-19 kuliko kada yoyote. Ilipaswa iwe lazima.
Hatari iko kinyume. Mtumishi anaweza kuwaambukiza watu wanaolazwa humo.

Maana Covid jinsi ilivyo, vijana wengi wanatembea na virusi bila madhara. Hatari iko kwa wazee na waliodhoofishwa kinga cha mwili kutokana na magonjwa. Yaani watu haohao wanaofika hospitalini.

Hata mtu mzima asiyeonyesha dalili anaweza kubeba virusi na kuwambukiza wengine. Ukichanjwa uwezekano wa kubeba virusi unapungua sana, pamoja na kujikinga mwenyewe.

Katika ujweli huo iko changamoto ya kuchanja watumishi wa afya,
 
Unajua kuwa watu wanataka sifa tu kwa mama waonekane maeneo yao wamehamasisha chanjo na wengi wamechanja!! Kwa hiho wanatumia vitisho na mabavu ili mama awaone nj watendaji wazuri!! Ila kwa Tz hii, watasubiri sana!! Waendelee tu kutoa data za kupika kuhusu chanjo!!
 
Kumekuwa na malalamiko kuwa mganga mkuu wa Tumbi Hospital amekuwa akitoa vitisho kwa watumishi ambao bado hawajashawishika kuchanja chanjo ya corona!

Mganga mkuu huyo Dr Malima amekuwa akitishia hata ajira kwa ambao hawatakubali kabisa kuchanjwa japo serikali ilishasema chanjo ni hiari.

Kuna tetesi za chini chini kuwa yeye mwenyewe alishachanja na ameathirika na chanjo hiyo. Kwa hiyo analazimisha na wengine wachanje ili kifo cha wengi iwe harusi !!

Inasemekana LEO asubuhi kwenye clinical meeting ameagiza chanjo ziletwe na atawaamuru wasiochanjwa wachanje bila hiari yao ya dhati!! Watu sampuli hii hawafai.

Rais alishatoa maagizo wahusika wasitumie mabavu!! Waelimishe na kushawishi ili watu wachanje kwa hiari. Katika tiba hakuna huduma unayoweza kumpa mtu kwa mabavu. This is contrary to medical ethics!!
Picha ya Mganga mkuu wa Tumbi Dr Amaan Malima ni hii hapa chini. Ajue kuwa tunamjua vizuri. Aheshimu watu.
View attachment 1959681
Tena waleo wabaojataa juchanja awatandike bakora nne nne
 
Back
Top Bottom