Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji atoroka katika kituo cha kazi baada ya kutuhumiwa kuiba Sh milioni 25 za ujenzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,275
2,000
MGANGA Mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji cha Kibena wilayani Iringa, Hope Mwale ametoroka katika kituo chake cha kazi baada ya kutuhumiwa kuiba Sh milioni 25 za ujenzi wa choo cha jengo la wagonjwa wa nje la Kituo cha Afya cha Kibena unaoendelea kijijini hapo.

Taarifa ya kuibwa kwa fedha hizo na mganga huyo ilitolewa na mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Nicco Kasililika kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi aliyefanya ziara kijijini hapo kukagua shughuli za maendeleo na kusikiliza kero za wananchi akiwa katika awamu ya tatu ya ziara yake ya ujenzi wa Iringa, ijulikanayo kama ‘Iringa Mpya’.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, Mkuu wa Mkoa alimuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Juma Bwire kupitia askari wake kuongeza kasi ya kumsaka na kumtia nguvuni mganga huyo.

“Siamini kama kiasi hicho cha pesa kinaweza kumpeleka mganga huyo mahali ambapo inaweza kuwa ngumu kufikiwa na vyombo vya dola,” alisema.

Wakati Mganga huyo akitafutwa, Hapi alilitaka jeshi hilo la Polisi kufanya pia upelelezi wa kina wa wizi huo kwani una kila dalili kwamba haukuhusisha mtu mmoja kwa kuzingatia taratibu za utoaji na matumizi ya fedha za umma.

Awali mhandisi wa halmashauri hiyo alisema, halmashauri ya wilaya hiyo kwa kupitia kituo cha afya Kibena ilipokea Sh milioni 200 kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo na choo chake.

Ujenzi wa majengo hayo ulianza Juni, mwaka huu kwa kuanza na jengo la wagonjwa wa nje ambalo wananchi walilichangia zaidi ya Sh milioni 1.8. Alitaja kazi zilizofanyika na kukamilika kwa asilimia 100 hadi sasa katika jengo hilo kuwa ni pamoja usafishaji wa eneo lote la ujenzi, uchimbaji wa msingi na kuta na kwamba kwa sasa wapo katika hatua ya kuezeka ambao umefikia asilimia 70.

“Kwa ujumla kazi za ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje zimefikia asilimia 65 na tunatarajia kukamilisha ujenzi huo ifikapo mwishoni kwa Septemba,”alisema. Aidha katika ziara hiyo Hapi ametembelea shule ya sekondari ya wasichana ya Ifunda na kukagua maendeleo ya ukarabati wake.

Hapi alisema kwa kupitia ukarabati huo, serikali ilitoa zaidi ya Sh milioni 700 kufanikisha kazi hiyo huku yeye akiahidi kuchangia mifuko 100 ya saruji katika kuboresha zaidi mazingira ya shule hiyo.

Pamoja na ukarabati huo wa shule hiyo ya wasichana, Hapi alisema serikali ilitoa pia zaidi ya Sh bilioni tatu kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe ya Ufundi ya Ifunda, ukarabati ambao tayari umekamilika.

Aliposikiliza kero za wananchi wa kata ya Ifunda, aliwapiga marufuku viongozi wa shule kuwatumikisha wanafunzi katika kazi zisizo kwenye mipango ya shule
 

mkupuo

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,302
2,000
Hii ndiyo shida ya kufanya malipo kwa fedha taslimu.Vinginevyo hiyo pesa yetu isingeangukia ktk mikono isiyo salama.
 

NONIYANG'WAKA

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
1,418
2,000
Kiuhalisia hata wewe ukioewa m25 kwa mikwara ya mabosi unaweza kuosha nazo wakutafute.


Serikali iepushe kulipa kwa keshi, ziende benk kwa benk.


Nimeshuhudia mawakala wa ununuzi wa pamba mkoani shinyanga wakitokomea na pesa kwa ajiri ya kununua pamba.

Kuna dem wangu alipotea na m8 hadi leo sujui alipo
 

Mmwaminifu

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
1,118
1,500
Kiuhalisia hata wewe ukioewa m25 kwa mikwara ya mabosi unaweza kuosha nazo wakutafute.


Serikali iepushe kulipa kwa keshi, ziende benk kwa benk.


Nimeshuhudia mawakala wa ununuzi wa pamba mkoani shinyanga wakitokomea na pesa kwa ajiri ya kununua pamba.

Kuna dem wangu alipotea na m8 hadi leo sujui alipo
Dah! Pole sana mkuu. Maana hapo una maumivu ya kupoteza pesa na dem!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom