Mganga atuhumiwa kumbaka mgonjwa wake, apigwa mpaka kufa

wang'ambo

Senior Member
Nov 29, 2015
113
27
Wananchi wenye hasira kali wamemuua mganga wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Kashinje Kashinje(55), mkazi wa kijiji cha Singita kata ya Usanda wilayani Shinyanga kwa kumshambulia kwa silaha za jadi wakati akijaribu kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 20 (jina linahifadhiwa) aliyefika nyumbani kwa mganga huyo kupata tiba ili apate mtoto.


Mganga huyo alitaka kumbaka mgonjwa wake mkazi wa kijiji cha Ishinabulandi baada ya kumlewesha na dawa za kienyeji.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Muliro Jumanne amesema tukio hilo limetokea Novemba 29,2016 saa tano asubuhi nyumbani kwa mganga huyo..

Amesema mganga huyo alifariki dunia baada ya kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi baada mganga huyo kujaribu kumbaka mwanamke huyo.

Kamanda Muliro amesema chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili na uongo wa kimatibabu wa kutaka kumuingilia kimwili mgonjwa wake baada ya kumlewesha kwa dawa za kienyeji lakini mgonjwa alipiga kelele akiomba msaada ndipo wananchi wakafika eneo la tukio.

Chanzo: Malunde blog
 
Sasa binti si alikua anataka mimba?
Mimba binadamu tunazithamanisha kutokana na mila, desturi na dini.
Mwanamke anapenda kuzaa na mtu ampendae siyo kubeba mimba hovyohovyo na mtu yeyote tu. Haujasikia wanawake kuzaa na kutupa watoto? Ulishatafiti chanzo cha msingi ni nini?
Sababu kubwa ni kujistukia kabeba ujauzito na mtu asiye chaguo lake ama mtu asiyeeleweka.
Sasa huyo marehemu kigagula kibaka, hakuwa chaguo la huyo binti, ndiyomaana yakatokea yaliyotokea.
 
Huyo mganga naye alikosea step tu,, wenzake wanawadanganyaga akina mama kwamba ili ashike mimba dawa inaingizwa kwa dudu ya mganga. Tena wanakubaliana kabisa bila hata kumlewesha madawa! Ila ukute huyo mgonjwa alikuwa ameshaingiliwa tayari ndo dawa ikaisha nguvu akazinduka na kukuta tayari amelowana!!
 
Afadhali huyo binti anajielewa.
Hakuna anachojielewa, huwezi kwenda kwa mganga kutafuta mtoto alafu ukasema Huyo mtu anajielewa Kama Mungu hajakupa mganga yeye ni nani hadi akupe mtoto?
 
Hakuna anachojielewa, huwezi kwenda kwa mganga kutafuta mtoto alafu ukasema Huyo mtu anajielewa Kama Mungu hajakupa mganga yeye ni nani hadi akupe mtoto?
Kila mtu ana imani yake. Labda ni muumini wa African Traditional Religion na si Muislam wala Mkristo.
 
Wanadamu bwana! wanapenda kushiriki mambo ya uganga hadi wanatia hasira, yaani mtoto wa miaka 20 tayari kajiona anatatizo la uzazi anakwenda kwa Mganga! Sasa alidhani mganga angefanya nini kama sio kujifanya anapaka dawa kwenye DUDU yake ndio aisokomeze kunako uzazi:(:(:(
mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu kwa wapenda kugangwa woteee
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom