Mganga Atamba Kumroga Cristiano Ronaldo Asifurukute | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mganga Atamba Kumroga Cristiano Ronaldo Asifurukute

Discussion in 'Celebrities Forum' started by MziziMkavu, Oct 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280

  [​IMG]
  CRISTIANO Ronaldo Wednesday, October 21, 2009 1:22 AM
  Mganga mmoja wa nchini Hispania ametamba kumpiga juju nyota wa Real Madrid asifurukute ndani ya Real Madrid na aandamwe na majeraha mpaka msimu utakapoisha. CRISTIANO Ronaldo yuko kwenye hati hati ya kuikosa mechi ya jumapili kati ya Real Madrid na Sevilla katika ligi ya Hispania baada ya kuumia enka yake.

  Kuumia huko kumekuja siku chache baada ya uongozi wa Real Madrid kupokea barua toka kwa mganga Jose Ruz, mwenye umri wa miaka 58 mkazi wa mji wa Malaga, ambaye ni maarufu kwa jina la "Pepe" akiwataarifu kuwa amemroga nyota huyo wa Ureno asifurukute kabisa uwanjani wakati akiichezea klabu ya Real Madrid.

  Pepe amedai kwamba Ronaldo ataandamwa na majeraha msimu mzima na kiwango chake cha soka kitashuka.

  Pepe aliendelea kusema kwamba hana nia mbaya na Real Madrid isipokuwa anatimiza wajibu wake kama mganga baada ya kutakiwa na mteja wake ampige juju Ronaldo.

  "Nafanya kazi yangu kwa mujibu wa matakwa ya mteja wangu ambaye pia mtu maarufu na anajuana vyema na Ronaldo".

  Mganga huyo alidai kwamba mmoja wa wapenzi wa zamani wa Cristiano Ronaldo ndiye aliyemtaka ampige juju Ronaldo kutokana muda aliompotezea baada ya kuwa naye na kisha kumtosa.

  Ronaldo alifunga magoli mawili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Marseille kwenye kombe la mabingwa wa ulaya lakini alitolewa nje ya uwanja akichechemea baada ya kuchezewa faulo mbaya na Souleymane Diawara.

  "Ronaldo atajeruhiwa vibaya sana uwanjani, siwaahidi lini ataumia, lakini subirini muone", alitamba Pepe.

  Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji ghali kuliko wote duniani baada ya kuhama kutoka Manchester United ya Uingereza kuhamia Real Madrid ya Hispania kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia wa paundi milioni 80.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3373038&&Cat=6
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mganga Atamba Kumroga Cristiano Ronaldo Asifurukute
  [​IMG]
  CRISTIANO RonaldoWednesday, October 21, 2009 1:22 AM
  Mganga mmoja wa nchini Hispania ametamba kumpiga juju nyota wa Real Madrid asifurukute ndani ya Real Madrid na aandamwe na majeraha mpaka msimu utakapoisha.CRISTIANO Ronaldo yuko kwenye hati hati ya kuikosa mechi ya jumapili kati ya Real Madrid na Sevilla katika ligi ya Hispania baada ya kuumia enka yake.

  Kuumia huko kumekuja siku chache baada ya uongozi wa Real Madrid kupokea barua toka kwa mganga Jose Ruz, mwenye umri wa miaka 58 mkazi wa mji wa Malaga, ambaye ni maarufu kwa jina la "Pepe" akiwataarifu kuwa amemroga nyota huyo wa Ureno asifurukute kabisa uwanjani wakati akiichezea klabu ya Real Madrid.

  Pepe amedai kwamba Ronaldo ataandamwa na majeraha msimu mzima na kiwango chake cha soka kitashuka.

  Pepe aliendelea kusema kwamba hana nia mbaya na Real Madrid isipokuwa anatimiza wajibu wake kama mganga baada ya kutakiwa na mteja wake ampige juju Ronaldo.

  "Nafanya kazi yangu kwa mujibu wa matakwa ya mteja wangu ambaye pia mtu maarufu na anajuana vyema na Ronaldo".

  Mganga huyo alidai kwamba mmoja wa wapenzi wa zamani wa Cristiano Ronaldo ndiye aliyemtaka ampige juju Ronaldo kutokana muda aliompotezea baada ya kuwa naye na kisha kumtosa.

  Ronaldo alifunga magoli mawili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Marseille kwenye kombe la mabingwa wa ulaya lakini alitolewa nje ya uwanja akichechemea baada ya kuchezewa faulo mbaya na Souleymane Diawara.

  "Ronaldo atajeruhiwa vibaya sana uwanjani, siwaahidi lini ataumia, lakini subirini muone", alitamba Pepe.

  Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji ghali kuliko wote duniani baada ya kuhama kutoka Manchester United ya Uingereza kuhamia Real Madrid ya Hispania kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia wa paundi milioni 80.
  Source:www.nifahamishe.com
   
 3. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
Loading...