Mganga aliyedai ana nguvu za kuzuia risasi apigwa risasi, afariki

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mganga aliyedai ana nguvu za kuzuia risasi apigwa risasi, afariki.

Chinaka Adoezuwe 26 ambae ni mganga wa Kienyeji amefariki baada ya mteja wake kujaribu iwapo ana nguvu za kuzuia risasi kuingia mwilini mwake na kumuagiza mteja wake kumpiga risasi alipokuwa akivaa nguvu hizo za kuzuia risasi katika shingo yake.

Kijana huyo alikuwa amemtembelea mganga huyo ili kupata nguvu za kuzuia risasi ambazo mganga huyo alimpatia, kulingana na mwanakijiji mmoja.

Ili kuthibitisha kwamba nguvu hizo zinafanya kazi, alisimama na kumpatia mteja wake Bunduki. Na hapo ndipo janga likatokea. :

Mwezi Januari, muuzaji wa dawa za kienyeji alikamatwa baada ya mtu mmoja aliyedaiwa kunywa maji ya kuzuia risasi kuuawa.

Muuzaji huyo anayeishi kaskazini magharibi mwa Nigeria aliripotiwa kumhakikishia mtu huyo kwamba hatofariki atakapopigwa risasi.

Polisi Nigeria wamethibitisha kumshikilia kijana huyo.
Chanzo .BBC Swahili.
 
watafta kiki waanze na huyo alietaka kuaguliwa kuzuia risasi, alikua na nia gani? Mganga alikua Majimarefu tu japo kaondoka katuachia hk kituko chenye kichwa kama behewa la treni ya mjerumani,
 
Dogo alikosea; ya Nigeria ni famba ngoma ipo Kigoma au lah ukiona vipi ifuate Congo kabisa kwa wale jamaa wafupii wanapiga mishale hatari SMG cha mtoto.
 
watafta kiki waanze na huyo alietaka kuaguliwa kuzuia risasi, alikua na nia gani? Mganga alikua Majimarefu tu japo kaondoka katuachia hk kituko chenye kichwa kama behewa la treni ya mjerumani,
Mbona na yeye kafia Muhimbili?
Angefia kwenye kilinge chake cha uganga ndio angekufa anasimamia anachokiamini
 
ingefanikiwa hii kinjekitile gwale wa vita ya maji maji uko alipo ,angejutia sana kwa nini hakuijua kipindi icho
 
Back
Top Bottom