Tajiri Mapesa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2020
- 707
- 695
Habarini ndugu zangu, kwanza poleni na mihangaiko yote ya hapa jukwaani,
Kwa majina naitwa Shukuru ni mkazi wa Misungwi nina umri wa miaka 35.
Katika harakati zangu za kutafuta maisha nilipata kushawishiwa na rafiki yangu kwenda kutafuta pesa za majini ambapo mimi na rafiki yangu tulikwenda kwa mganga mmoja huko maeneo ya njombe.
Mganga alitupatia utajiri lakini kwa masharti ya kutoshiriki tendo la ndoa na mwanamke yeyote yule wala kuoa. Nimefanikiwa kufuata masharti hayo kwa asilimia 100, mpaka sasa nina miaka 10 sijashiriki tendo la ndoa na mwanamke yeyote. Nina majumba, magari na utajiri mkubwa ila sijaoa.
Sasa wazazi wangu walivyoona nakaa muda mrefu bila kuoa wamenijia juu wanataka nioe na wanahitaji wajukuu. Nipo njia panda sijui la kufanya. Naombeni ushauri wakuu nifanyeje.