Mgambo wagoma kupiga kura Handeni


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
705,438
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 705,438 280
Mgambo wagoma kupiga kura Handeni Send to a friend Monday, 01 November 2010 06:18 0diggsdigg

Mwandishi Wetu Handeni
WANAMGAMBO zaidi ya 100 wa Jimbo la Handeni wametishia kutopiga kura baada ya kukosa kupangiwa vituo vya kusimamia kazi ya kupiga kura, licha ya kupewa mafunzo ya kusimamia.

Wakizungumza na wandishi wa habari jana wanamgambo hao walidai walipewa mafunzo ya jinsi ya kusimamia uchaguzi, lakini jana waliitwa na msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Handeni Hassan Mwachibuzi majira ya jioni na kuambiwa kuwa vituo vyote tayari vinawasimamizi.

Walisema taarifa hiyo, iliwavunja moyo sana kwa kuwa wamekopa fedha za kushonea sare (magwanda)na kwamba hawajui ni wapi watapata fedha za kulipia gharama za mashono hayo.


"Tumekopa fedha kwa ajili ya kushonea gwanda, kushona gwanda moja ni Sh 30,000 tumetumia muda wetu mwingi katika mafunzo halafu tunaambiwa eti vituo vimejaa hii inasikitisha sana," alisema Juma Mjaramba (78) na Rashidi Hassani(30) kwa nyakati tofauti.

Akizungumzia sakata hilo, katibu wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Handeni ambaye pia ni Afisa Usalama wa Wilaya Gerald Kusaya ambae alishiriki katika harakati za kutatua mgogoro huo, alisema tatizo hilo, limejitokeza ila walitalimaliza na mgambo hao wataendelea kupiga kura hata kama wamekosa vituo vya kusimamia.

"Hilo jambo ni kweli tatizo hili lilikuwepo unajua sisi kama kamati ya ulinzi na usalama wilaya tuliwaandaa hawa mgambo kwa ajili ya kusimamia kumbe katika maeneo mengine watendaji ambao ni wasimamizi uchaguzi kata nao waliandaa wanamgambo hivyo wa hapa wilayani wasingepata nafasi.


Mgambo hao, walikuwa 120 na 80 walipata vituo vya kusimamia na 40 walikosa na kuombwa radhi kwa tatizo hilo, lililotokea,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Kapteni Mstaafu Seif Mpembenwe alisema watazungumza na mkurugenzi kuhusu tatizo hilo, ili mgambo waliokosa vituo vya kusimamia walipwe fedha walizokopa.

"Tutakaa na mkurugenzi ili kujadili kuhusu waliokopa fedha na kuwalipa, wasihofu kuhusu hilo, tutaliweka sawa," alisema Mpembenwe.

Jimbo la Handeni linavituo 370 vya kupigia kura na wananchi wamejitokeza kwa wingi kupiga kura huku amani na utulivu ikiwa imetawala maeneo m
 

Forum statistics

Threads 1,252,233
Members 482,048
Posts 29,801,271