Mgambo wa City Mkiacha Rushwa Hii Posta, Kariakoo inaweza kuwa safi Kama Moshi mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgambo wa City Mkiacha Rushwa Hii Posta, Kariakoo inaweza kuwa safi Kama Moshi mjini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mgt software, Apr 2, 2012.

 1. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  Leo nimetembelea maeneo ya kariakoo na posta angalau kwa siku ya leo kumeonekana kuwa safi, hasa pale kariakoo , packing zote zilikuwa safi, hata pale stendi ya kawe na Tegeta.
  Nasema kwamba kama mgambo wote wakiwa waaminifu jiji linaweza kuwa safi, ila cha kushangaza mgambo huwa wanapitia Tshs 1000 mpaka tshs 2000 kwa wote wanaopanga vitu barabarani au kingo za barabara hata stend za mabasi,.
  Cha kukufanya kuhusu hili.
  1. Kila Mgambo wapewe eneo husika kwa makundi, alafu mkuu wao apitie kila baada ya muda fulani, akikuta eneo husika ni chafu au kuna wapanga bidhaa barabarani, achukuliwe hatua hata kufukuzwa kazi.

  2. kila mmiliki wa nyumba au mpangaji awe anatoa taarifa za eneo lake kuhusu uvamizi wa eneo lililopo mbele yake kwa mgambo.

  3. kuwepo kamera za kurekodi matukio hasa ambapo kuna uchafu mwingi imulike waliosabababisha na kuchukuliwa hatua, na itaondoa mgambo wala rushwa, mie nawaona sana wakila rushwa ila sina kamela mzuri.

  4. Kuwaadhibu wote wanaotiririsha maji machafu bila kujali ni nyumba ya nation housing au serikali
   
 2. broken ages

  broken ages Senior Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 160
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kwani wewe unafikiri kwenye hilo kuna ambaye yuko serious kulitatua? Si mgambo wala hao watakaojiita viongozi wao kutoka city maana haiwezekani wakawa wanalinda watu kutokupanga bidhaa barabarani kila siku na bado bidhaa ziendelee kupangwa barabarani na kesho yake waamke waende kusaini ofisini waingie kazini mitaani kwa swala lile wasifanikishe miaka bado wasipange mikakati mipya ama kungalia ni wapi inapowashinda ili pafanyiwe marekebisho kwa siku inayofuata,hapa kuna vijana wanaokatiwa mali ni ambao jana ama kuna siku hawakuwapa Hawa mgambo pesa yao elfu mbili.kwa kweli ni kero huwezi kuendesha gari mitaa ya kariakoo wenye maduka wanaolipa kodi za serikali pamoja na kodi za nyumba waanapata shida sana mbele ya milango yao madukani hapapitiki.ni city wangetoa ajiraa kwa makampuni ya cecurity wakafanya hiyo kazi maana wao imewashinda
   
 3. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  siku zote bidhaa zote za jioni huwa ni masalia ya kuokoteza, waokotaji hao ikifika jioni hawajafanikiwa kuuza, huwa wanaacha pale hasa nyanya mbovu pilipili hoo na ndizi mbivu, sasa imefika sehemu kuzuia kuuza bidhaa adui wa mazingira sehemu isiyohusika, yatupasa kuungana wote kudhibiti hii hali kwa kuwa hela nyingi hutumika kuzoa taka.
   
 4. H

  Haika JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ili. Iweje?
   
 5. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  ili iwe hivyo hivyo ulivyoelewa, unaonekana kupenda sana uchafu!!!
   
 6. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  mani , jamani jamani, leo nimeona tena live mgambo wa kike akichukua 1000tshs na kusema ahsante mola!!!!
   
Loading...