Mgambo Auawa Stand ya daladala Mwenge

Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,282
247
Askari wa kikosi cha mgambo cha manispaa ya Kinondoni ambaye hadi sasa amefariki baada ya kupigwa na kitu kizito leo asubuhi walipo kuwa kwenye operesheni ya kuondoa vibanda vya wafanyabiashara ndogondogo kwenye stendi ya daladala ya Mwenge.

Mpaka nakuleteeni habari hii hali si shwari pale mwenge stand, ni vurugu mtindo mmoja.
 
Dah pole mgambo, poleni wagambo.
Inauma sana mgambo anapo nyang'anya mali za wamachinga alafu anaenda kuuza.
 
TATIZO la umachinga na biashara ndogondogo, litaleta maafa makubwa hapa nnchini siku si nyingi, hii ni trela, ipo movie kamili inakuja.
nasema hivyo kwasababu hakuna sera za pamoja ktk kujua namna gani hawa vijana wanawezeshwa kufanya kazi zao vyema.
wakati wakandolo na Lowassa waliondolewa, na kulikua na msisitizo mkubwa wakuhakikisha hawarejei ktk maeneo ya stand na pepezoni mwa barabara.
Alipo kuja huyu mwalimu wa upe, mkuu wa mkoa mpya , akawaruhusu wafanye biashara kwa amani yao, ila wenye vyakula/mama lishe wahakikishe wanakaa maeneo masafi.
Machinga wakajitafutia tena vimitaji vyao , wakarejea kwa kasi jijini, sasa leo anakuja sijui mkuu wa ilaya anatoa maagiizo yakuwafukuza, wanapigwa na kunyang'anywa mali zao. unataraji nini ?
kisasi na vurugu, ipo siku tutaona maafa zaidi na zaidi.
 
mpaka tulipo sidhani kama kuna mtu anaweza akajitokeza adharani na kutangazia uma kuwa tanzania ya sasa ni nchi ya amani, inatisha sana
 
Mwosha huoshwa

Mimi kwa kweli siungi mkono kifo chochote kile. Hapa wa kulaumiwa si Mgambo bali ni watunga sera ambao wanawa-expose hawa Mgambo kwenye unnecessary risks. Kitendo cha kuwatuma kufanya wanayofanya bila kuwa na zana za kujilinda ni upuuzi mkubwa, ingekuwa nchi za wenzetu huyo aliyewatuma angejizulu leo hii hii.

Na huu ni mwaka wa uchaguzi, tutarajie vifo vingi tu vya aina hii kwa ubinafsi wa watawala wetu.
 
mimi kwa kweli siungi mkono kifo chochote kile. Hapa wa kulaumiwa si mgambo bali ni watunga sera ambao wanawa-expose hawa mgambo kwenye unnecessary risks. Kitendo cha kuwatuma kufanya wanayofanya bila kuwa na zana za kujilinda ni upuuzi mkubwa, ingekuwa nchi za wenzetu huyo aliyewatuma angejizulu leo hii hii.

Na huu ni mwaka wa uchaguzi, tutarajie vifo vingi tu vya aina hii kwa ubinafsi wa watawala wetu.

mwendo wa makafara umeanza hivyo, jichunge wewe na hatua zako.
 
Ni kweli jiji au nchi inatakiwa iwe katika utaratibu mzuri na mazingira mazuri ya uendeshaji wa shughulizake kama hizo biashara ndogo ndogo lakini tulichelewa na kuruhusu huu utaratibu mbovu kuwepo, tatizo ni kuwa wakti hao watu wanajenga vibanda hivyo serikali ilikuwa inaona na je kwa nini walikuwa wanasubiri mpaka wamejiimarisha na kufanya kuwa ni sehemu wanayoitegemea ktk maisha yao? Mtu anapokunyang'anya rizki hasa ukiwa na majukumu na mipango nayo lazima uwe mkali sana though it doesn't justify the killings.
 
Matokeo ya Kidato cha nne 2009

Division I + II + III = 42,627 sawa na Asailimia 17.85

Divisheni IV = 130,651 sawa na Asilimia 54.66

Divisheni 0 ( Sifuri) = 65,708 sawa na Asilimia 27.49

Najiuliza hivi hawa Zero + Four ambao ni Asilimia 82.15 Wanakwenda wapi?

Mwaka Jana tumezalisha wangapi? Mwaka Juzi Je na Je Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Mwakani inapunguza hiyo Zero na Four

Je Baada ya Miaka Kumi tutakuwa na Taifa Gani

Serikali iwe Makini maana kila mwaka inazalisaha Wamachinga malaki sasa Baada ya Miaka kumi kutakuwa na Jeshi kubwa sana la Wamachinga na Hao Mgambo hawataweza kupambana
 
Askari wa kikosi cha mgambo cha manispaa ya Kinondoni ambaye hadi sasa amefariki baada ya kupigwa
na kitu kizito leo asubuhi walipo kuwa kwenye operesheni ya kuondoa vibanda vya wafanyabiashara ndogondogo kwenye stendi ya daladala ya Mwenge.
Mpaka nakuleteeni habari hii hali si shwari pale mwenge stand, ni vurugu mtindo mmoja.

Bongo shakalabaghala juzi wasafiri wamewapa kibano baada ya safari kusimamishwa kutokana na madereva kutokuwa na leseni leo mgambo kaua, kule musoma majuzi watu 17 wameua. Waziri wa mambo ya ndani hata kutia neno katika hali kama hii....yuko kimyaaaa kabisa. Inaelekea naye hayamuhusu!
 
hivi kwa nini mauaji ya ajabu ajabu yanatokea kila kukicha!!whats happenin folks??au ni kwa vile iliandikwa nyakati za mwisho watu watauana kama wanyama ???
 
Askari wa kikosi cha mgambo cha manispaa ya Kinondoni ambaye hadi sasa amefariki baada ya kupigwa
na kitu kizito leo asubuhi walipo kuwa kwenye operesheni ya kuondoa vibanda vya wafanyabiashara ndogondogo kwenye stendi ya daladala ya Mwenge.
Mpaka nakuleteeni habari hii hali si shwari pale mwenge stand, ni vurugu mtindo mmoja.
Hiki kiswahili mbona kimekaa upande upande.... ambaye hadi sasa amefariki baada ya kupigwa (!?)
 
Muungwana yuko majuu anawaambia vijana nyumbani msiwe na shaka mambo SHWARI!! Huku mgambo wanapigwa nondo na watu wanachinjana Tarime!!
Amiri jeshi mkuu bado anahitaji mda kuvuta donors....
 
serikali iko uturuki kulamba PhD... ikirudi yataisha haya
Hivi Rais hana wasaidizi lazima kwenye kila tukio hawepo?

Waziri wa mambo ya ndani anafanya kazi gani? Mkuu wa Polisi naye hayupo!? Wakuuu wa mikoa na wilaya kazi zao ni zipi!?
 
Back
Top Bottom