Mfutakamba na ardhi ya milima ya kilolo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfutakamba na ardhi ya milima ya kilolo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alexism, Jul 19, 2012.

 1. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Wanajamvi kuna tuhuma nzito na dhambi ambayo itamuandama mh. Mfutakamba kwa kuwazulumu wananchi wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa. Mfutakamba wakati akiwa mkuu wa wilaya ya Kilolo alidiriki kuuza eneo kubwa la milima ya kilolo mpaka kufika mpaka wa Kilolo na Morogoro kwa wale wanaoitwa wawekezaji wa kizungu wanao miliki kampuni inayoitwa New Forest. Mfutakamba hakuwai kuwashirikisha wakazi na wananchi wa maeneo hayo bali aliamua kama yeye kitu ambacho si sahii. Wananchi wa maeneo hayo yaliyouzwa wamejikuta hawana ata sehemu ya kuchanja kuni,kulisha mifugo na mtu akikutwa huko basi ni taabu tu kwani anaweza kufungwa au kupigwa pamoja na faini.
  Viongozi kama hawa hawatufai na inabidi wawajibike kwa makosa na ufisadi kama huu kwani tunapoendelea kuyafumbia macho mambo kama haya mbeleni itakuja kuwa shida na inawezekana tukawa kama Zimbabwe.
  Mfutakamba popote ulipo rahana zitakufuata na dhambi hii mpaka mwisho wako.
   
 2. J

  Jizalendo Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na lana ya CCCC je nayo itamwacha.
   
Loading...