JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Salamu wanabodi !
Habari kuwa Nchi kumi wahisani kati ya 14 wamejitoa kusaidia bajeti ya serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni habari mbaya kupata kutokea.Kwa miaka mingi Nchi yetu haijawahi kukwaruzana na Nchi wahisani kama ilivyo sasa.Kimsingi ni lazima tukubaliane na masharti yao hayo mawili, vinginevyo Nchi imeingia kwenye mtego mkubwa kweli kisiasa na kiuchumi.
Miaka ya 1980 ,serikali ya mwalimu JK ilishauriwa na wazungu ishushe thamani ya shilling yake ,Mwalimu akagoma kwa kusema kamwe hawezi kuendelea kukumbatia masharti ya kinyonyaji ya wazungu.hotuba ile aliitoa akiwa Kigoma, na harakaharaka Nchi nzima tukawa tunaandamana kumuunga mkono mwalimu kwamba tupo pamoja nae walau kwa wazo lile la kuto kukubaliana na masharti ya wazungu.kilicho fuata ilikuwa ni balaa.Uchumi ulidolora kupita kiasi.Hali zaidi ya ile ndio inainyemelea Nchi yetu.Tuombe tusifike huko maana waathirika wa kwanza watakuwa wanafunzi wa higher learning institutions na wafanyakazi wa serikali.miaka ile wanafunzi tulikula ugali dona na kabichi ambayo haija ungwa chochote toka January mpaka Desemba!!
Ushauri wangu kwa serikali ya JPM ni kwamba wakubali bila masharti yoyote kurudi kwenye meza ya majadiliano na chama cha CUF ili wafikie muafaka wa kisiasa lakini pia wakubali kuirekebisha sheria kandamizi ya cyber crimes.Kukubali mapungufu siyo udhaifu,bali iwe ni changamoto kwetu sote ili siku nyingine tusijikwae tena.
Wazo la kujitegemea kisiasa na kiuchumi ni jema lakini kwa Nchi kama yetu iliyo panua ukubwa wa serikali yake namna hii kwa sasa hatuwezi hata tufanye nini,Hatujajipanga. na ndio maana nikasema tujifunze yaliyo mkuta Nyerere!