Umomi
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 677
- 983
We jamaa tuache kudanganya hapa JF! Sema kweli mimi nimebahatika kupata Elimu japo sijamaliza na katika masomo yangu nilibahatika kujaribu mambo mbali mbali. Isitoshe mimi katika mambo ya IT nipo vzr sana hasa katika upande wa sim japo sijasomea hayo mambo!Kijana mwezangu, maisha siyo rahisi , but ni rahisi kwa wale wanaothubutu na kutoka nje ya comfort zone. Alafu usipende sana kutaka kuhurumiwa tena hasa unapokuwa mtoto wa kiume, ni hatari sana. Alafu usiwe unajiaminisha maisha unayopitia wewe basi wengine hawayajui au hawajayapitia, wanayapitia ila wanapambana na changamoto zilizo mbele yao na kuzishinda, na hiki ndiyo kipimo cha elimu uliyoipata huko chuo kiku.
Kwahiyo ww unaamini kila mwenye mtaji ni lazima atoke kwenye daraja la maisha ya kati? Unazungumzia 100k? Toka nje ya Comfort Zone utaipata tu hiyo 100k, usianze kuangalia wanaokuzunguka watakuonaje au watakuchukuliaje, believe me or not ukifika stage hiyo utaipata hiyo 100K. Hata sisi tulipitia huko.
NOTE: LIFE BEGINS AT THE END OF YOUR COMFORT ZONE
Kilinisaidia sana ni kutumia smartphone toka nipo kidato cha pilo nikawa nasoma sana mtandaoni. Ukweli n kwamba mtandaoni kuna vitu vingi sana na vyema faida. Lakini ili uvipate hivi vitu lazima uwe vzr mfukoni na kiakili pia. Hivi vitu vinahitaji device kama smartphone, laptop au desktop kaka usidanganye Watanzani.
Na nimekuja kuiva sana katika mambo hizi lipoenda chuoni nikasoma Course mbili zinazohusiana na mambo ya technology japo mimi n mwalimu kitaaluma. Ukisema Online shopping kwa Tanzania hata ile mifumo ya Malipo for Online Shopping hajawa sawa kama inavyotakiwa mkuu
Ukiangalia mifumo vingi inatakiwa ukamilishe malipo ndani ya saa 1 toka ku-order bidhaa. Na hii nina ushahidi mwanzani mwa mwaka huu nilipita mtandao fulan hivi nikaona kuna bidhaa kama frash na memory card zilikuwa zinauzwa kwa bei rahisi sana mtandaoni nikaoda bana baada ya kupokea namba malipo nigaingia zangu M-pesa nikafanya malipo. Baada ya kumaliza sms ya muamala haikuja mpaka kesho yake kucheki bidhaa haijalipiwa. Afu sikupata msaada.
Kwahiyo msiwe mnakuja kutupa mambo ya uongo hapa kaka kuna mengine tumeishayafanya. Mpaka tukaamua kurudi kupambana kwa shughuli za kawaida tu. Ila sikatai kuwa fursa hazipo zipo nyingi tu lkn n ambao tayari wana mtaji wa kutoshaa.