Mfunze Mwanao kujiajiri, mwambie maisha hayaanzi akiajiriwa, wasomi wakiwa wengi ajira zinakuwa chache

Ila na ukubwa wa mishahara+bonus lkn maisha yao baada ya ajira hua siyaelewi,boss mstaafu wa Tbc baada Tido kwa sasa ndio mwenyekiti wetu wa mtaa na wakubwa wengine kibao hali zao ni mdogo mdogo.
Kumbe unakaa na wakubwa hongera! Nafikiri wewe ndio uko sehemu nzuri na sio kwamba wao wako vibaya.
 
Kumbe unakaa na wakubwa hongera! Nafikiri wewe ndio uko sehemu nzuri na sio kwamba wao wako vibaya.

Hapana mzee baba huku hata majirani choka mbovu kama mimi tuko wengi balaa.

Nilikua nashangaa tu,madaraka/pesa walizoshika na maisha yao ya mtaani sio directly proportional.
 
Sio poyoyo mleta mada yuko sahihi labda wewe hujamwelewa.

Kiukweli ajira hamna na Wasomi ni wengi. Ukweli utabaki

Wasomi waangalie namna ya kujiajiri...anapokuwa shule asiwaze ajira awaze kutafuta pesa....

Biashara wala haihitaji uzoefu toka kwa wazazi hayo ni mawazo tu mgando....you can make your own life....

Anyway

Mimi nitawaelimisha watoto wangu kuwa usomi sio ajira wajifunze namna ya kutafuta pesa nje ya ajira. Na nitawapeleka veta.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu asikuumize kichwa huyo bibi.

Watoto wengi mama zao wauza maandazi,nyanya na samaki.

Lakini wazazi hao huiwaambia watoto wao wasome na watoto wanasoma na kuja kuibuka videdea huko mbeleni.

Watoto wengi sana wazazi wao wako tofauti na wao.

Labda angesema mzazi anaathiri mtoto ikiwa hamfanyii maongezi ya kumuambia kipi kizu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hakuna anedanganya mtu hapa, kwa kazi unayoifanya ya kuuza dagaa umejiajiri wale usijipuuze. Kitu kimoja tambua kuna tofauti kati ya kujiajiri na kufanya biashara. Anza kufikiria kufanya biashara sasa.

Mtu aliyejiajiri huwa akitaka kuajiri atatafuta mtu anayemzidi kwa mambo mengi ili aweze kumcontrol ila anayefanya biashara principle inasema only employ people who are more inteligent than you.

Sent using Jamii Forums mobile app


Huyo naye haeleweki..mara dagaa mara samaki..watu wanatajirikia kwenye hizo mishe yy anaona km mateso? Lols
 
We jamaa tuache kudanganya hapa JF! Sema kweli mimi nimebahatika kupata Elimu japo sijamaliza na katika masomo yangu nilibahatika kujaribu mambo mbali mbali. Isitoshe mimi katika mambo ya IT nipo vzr sana hasa katika upande wa sim japo sijasomea hayo mambo!

Kilinisaidia sana ni kutumia smartphone toka nipo kidato cha pilo nikawa nasoma sana mtandaoni. Ukweli n kwamba mtandaoni kuna vitu vingi sana na vyema faida. Lakini ili uvipate hivi vitu lazima uwe vzr mfukoni na kiakili pia. Hivi vitu vinahitaji device kama smartphone, laptop au desktop kaka usidanganye Watanzani.

Na nimekuja kuiva sana katika mambo hizi lipoenda chuoni nikasoma Course mbili zinazohusiana na mambo ya technology japo mimi n mwalimu kitaaluma. Ukisema Online shopping kwa Tanzania hata ile mifumo ya Malipo for Online Shopping hajawa sawa kama inavyotakiwa mkuu

Ukiangalia mifumo vingi inatakiwa ukamilishe malipo ndani ya saa 1 toka ku-order bidhaa. Na hii nina ushahidi mwanzani mwa mwaka huu nilipita mtandao fulan hivi nikaona kuna bidhaa kama frash na memory card zilikuwa zinauzwa kwa bei rahisi sana mtandaoni nikaoda bana baada ya kupokea namba malipo nigaingia zangu M-pesa nikafanya malipo. Baada ya kumaliza sms ya muamala haikuja mpaka kesho yake kucheki bidhaa haijalipiwa. Afu sikupata msaada.

Kwahiyo msiwe mnakuja kutupa mambo ya uongo hapa kaka kuna mengine tumeishayafanya. Mpaka tukaamua kurudi kupambana kwa shughuli za kawaida tu. Ila sikatai kuwa fursa hazipo zipo nyingi tu lkn n ambao tayari wana mtaji wa kutoshaa.


Walau UNgetaka kuelewa amemaanisha nn kutoka kwenye COMFORT ZONE USINGEBISHA!
 
Mkuu mc gregor nilianza na mtaji mdogo sana coz nina shamba la ekari mbili tangu mwaka 2005 nilikuwa napanda mahindi ya kawaida lakini kwa sasa ninapanda mahindi ya hybrid kutoka kampuni ya seed-co arusha na pia na kodisha mashamba ya wengine;
mifuko 10@12000=120000
trekta 2eka@45000=90000
dawa ya multi afa plus,booster kitu kama 50000
jumla 260000~300000/=
kununu mahindi kutoka shambani kutegemea na msimu 36 mpaka 40 kwa gunia kuuza 60 mpaka 90 kutegemea na eneo.
 
Mkuu Umomi kwenye NGOs wako watu wamesajili kwa lengo la faida tu na sio kusaidia jamii na wanatumia watu waliokwisha kuajiriwa kuepuka gharama,imekuwa kama business kwa sasa mimi natumia fundsforngos.org kutafuta donors,call for proposals zipo nyingi tatizo tumeshajiwekea mtazamo wa kuajiriwa na kukaa tu, kujiajiri inahitaj kujituma kupita kiasi na nidhamu.
 
Mkuu mc gregor nilianza na mtaji mdogo sana coz nina shamba la ekari mbili tangu mwaka 2005 nilikuwa napanda mahindi ya kawaida lakini kwa sasa ninapanda mahindi ya hybrid kutoka kampuni ya seed-co arusha na pia na kodisha mashamba ya wengine;
mifuko 10@12000=120000
trekta 2eka@45000=90000
dawa ya multi afa plus,booster kitu kama 50000
jumla 260000~300000/=
kununu mahindi kutoka shambani kutegemea na msimu 36 mpaka 40 kwa gunia kuuza 60 mpaka 90 kutegemea na eneo.
Unapata gunia ngapi kwa hekari?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Avriel inategemea na mambo haya kwanza ubora wa ardhi,uandaaji mzuri,na mbegu unayopanda.
kwa huku mimi huwa napata gunia 45 kwa heka nikitumia mbegu ya tembo au kitale kutoka kenya.
lakini kama mwaka huu nina tumbili ambayo inakomaa muda mfupi miezi 3 hapo napata 30-35 gunia kwa heka
 
Mkuu Avriel inategemea na mambo haya kwanza ubora wa ardhi,uandaaji mzuri,na mbegu unayopanda.
kwa huku mimi huwa napata gunia 45 kwa heka nikitumia mbegu ya tembo au kitale kutoka kenya.
lakini kama mwaka huu nina tumbili ambayo inakomaa muda mfupi miezi 3 hapo napata 30-35 gunia kwa heka
Gunia moja bei gani?
 
Back
Top Bottom