Mfungwa jinsia 2 Shinyanga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfungwa jinsia 2 Shinyanga!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mgoyangi, Dec 8, 2010.

 1. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #1
  Dec 8, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katika Gereza la Malya amepatikana mfungwa mwenye jinsia mbili, ana kifungo cha miaka 30, kwa wizi wa mtambo wa kubaini almasi.

  Awali alifungwa kama mwanaume, lkn baadae ikaonekana zote mbili zinafanya kazi! Fikiria hali ya gerezani!

  Sasa wameamua kumuweka chumba cha peke yake!
   
 2. chokambayaa

  chokambayaa JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 528
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mhh kazi kweli kweli.......
   
 3. k

  kinubi Senior Member

  #3
  Dec 8, 2010
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 130
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Provide the source plz
   
 4. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,513
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  Hata bila source, it is a good story. Ok yeye ndo source
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Dec 8, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ahahahaaah! Zote zinafanya kazi! Ni balaa!
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ahhhh!
   
 7. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Atumikie nusu ya kifungo gereza la wanaume na nusu nyingine gereza la wanawake. Apate huduma zote mbili na aweze kuhudumia jinsia zote mbili
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  duh sasa sijui atalindwa na maskari wa jinsia gani katika hicho chumba cha peke yake - askari wa jinsia zote hawakawii kugombania zamu za kumlinda.
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  hii kali!zote ana pata ejaculations?
   
 10. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  huyo hana shida kabisa maana akipata hamu anweza kujishughulikia........kaz kwelikweli........
   
 11. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2010
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Wamuache na wanawake kule, noma akiwa kwa wanaume...wampe kondoms tu
   
 12. e

  ejogo JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mfungwa aliyehukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha, ameuweka katika wakati mgumu uongozi wa Magereza Mkoa wa Shinyanga, baada ya kukutwa na jinsia zote mbili na zote zikifanya kazi kama kawaida.
  Mfungwa huyo alikuwa katika Gereza la Malya lililoko wilayani Maswa baada ya kuhukumiwa, hali iliyosababisha mkanganyiko kwa uongozi huo kuhusu sehemu ambayo anapaswa kuwekwa gerezani.
  Hayo yalisemwa jana na Ofisa Magereza mkoani hapa, Elika Pesha, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkasa huo.
  Hata hivyo, ofisa huyo alikataa katakata kutaja jina la mfungwa huyo kwa madai kuwa kufanya hivyo ni sawa na kumdhalilisha.
  Alisema baada ya uongozi wa gereza kuona utata huo, uliamua kumpeleka mfungwa huyo hospitali ya Bugando jijini Mwanza kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu ndipo iligundulika kuwa jinsia zote zinafanya kazi.
  Pesha alisema kuwa tayari taratibu za kumpeleka Muhimbili jijini Dar es Salaam kufanyiwa upasuaji baada ya kupata ushauri kutoka kwa madaktari zimekamilika na kwamba mfungwa huyo atapatiwa fursa ya kuchagua ni jinsia gani iondolewe.
  Alisema katika upasuaji huo kitakachozingatiwa zaidi ni ushauri wa wataalamu, ambao wengi wanaona kuwa ni bora abaki na jinsia ya kiume kwa sababu umbile lake linaonyesha kuwa ni mwanaume.
  Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mkoa wa Shinyanga, Issa Magori, aliyesikiliza kesi ya mfungwa huyo na kuitolea hukumu alisema mwaka 2007, mfungwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga kwa kosa la unyanganyi wa kutumia silaha akiwa na wenzake watatu.
  Alisema walivamia kwenye ofisi ya biashara ya almasi na kuiba mzani wa kupimia madini hayo, simu mbili pamoja na mashine ya utambuzi wa almasi.
  Hakimu Magori alisema mfungwa huyo pamoja na wenzake walikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na walipokaguliwa kabla ya kupelekwa gerezani ndipo walipogundua kuwa mmoja wa wafungwa hao anajinsia mbili na zote zinafanya kazi.
  "Mfungwa huyo hana maziwa, isipokuwa ana ndevu sauti yake ni ya kiume na jina lake ni la kiume kwa ujumla muonekano wake ni wa jinsia ya kiume kutokana na hali hiyo uongozi wa magereza umeamua kumuweka chumba maalumu chini ya uangalizi mkubwa," alisema.
  Alieleza kuwa tangu aanze kazi hiyo hajawahi kutoa hukumu kwa mtu ambaye ana jinsia mbili na zote zinafanya kazi na kwamba tukio kama hilo lilishawahi kutokea mkoani Kagera kwa mtu ambaye alikuwa ana jinsia mbili, lakini kati ya hizo moja ndiyo ilikuwa ikifanya kazi.
  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...