Mfungwa anapotoroka akiwa analima kwenye shamba la vigogo - Abuse of Authority

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,458
956
Watanzania.. hatutaacha kushangaa kila kukicha. Leo 7/8/08,kwenye taarifa ya habari, tumesikia taarifa ya kutoroka kwa mfungwa aliyekuwa anatumikia kifungo cha miaka 30 katika gereza la Karanga, kwa kosa la ujambazi akiwa analimishwa kwenye shamba la muwekezaji!!!Hii imekuja baada ya Kamishna Mkuu wa Magereza kupiga marufuku " utumikishwaji" huo.
Hebu someni habari hiyo hapo chini ......wonders! wonders!


Marufuku vigogo kuwatumia wafungwa

2007-11-27 15:47:21
Na Patrick Chambo, PST Moshi


Kamishina Mkuu wa Magereza Nchini, Bw. Augustino Nanyaro, amewapiga marufuku baadhi ya wakuu wa magereza nchini tabia ya kuwakodisha wafungwa kwa wawekezaji wa mashamba makubwa kwa ajili ya kuwalimia huku wafungwa hao wakiwalipa sigara, bangi na sabuni.

Kamishna Nanyaro aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika Gereza Kuu la Wagonjwa Tanzania la Karanga, Manispaa ya Moshi baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wafungwa na mahabusu zaidi ya 2,000 dhidi ya uongozi wa Gereza hilo.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Joel Bukuku, alithibitisha jana kutolewa kwa agizo hilo katika kikao chake na wafungwa na mahabusu alipokuwa akipokea malalamiko yao.

Imedaiwa kuwa, wafungwa hao walimueleza Kamishna kuwa, licha ya gereza hilo kutambulika kuwa ni la Wagonjwa Tanzania na sio la kilimo, wamekuwa wakilimishwa kwa wawekezaji, wakuu wa magereza, wilaya, mkoa hadi taifa zaidi ya ekari 300.?

Mmoja wa maofisa wa magereza, alisema mashamba ya wakubwa na wafanyabishara ndiyo yanayochochea biashara za kulawitiana magerezani.

Wakizungumza jana na PST baadhi ya wafungwa na mahabusu katika Mahakama Kuu Kanda ya Kilimanjaro na hospitali ya KCMC, walisema wamefurahishwa na kauli ya Kamishna Mkuu huyo.

Wameyataja maeneo yenye mashamba hayo kuwa ni Mbatakero, KIA, Longoi Mashine Tools na Kibosho kwa mwekezaji mmoja, Njiapanda ya Himo na maeneo TPC walikokuwa wakimlimia kiongozi mmoja wa serikali wilayani Moshi.

`Tukitoka gerezani, tunatoka kama RPC Genge, RPO Genge, CCP Genge au RC Genge, lakini tunakwenda kulima kwa wakubwa au wazungu na wananchi, na tukifika shambani, tunapewa sigara, bangi na sabuni, huku mnapewa soda na nyama mnalima ekari zaidi ya 100,? alisema mmoja wa mahabusu na kuongeza ?na hapo ndipo tunapohoji, mbona gerezani tumekunywa uji usio na sukari, ugali na mboga havina mafuta, je kweli ni shamba la Gereza.?

Wafungwa hao walimuomba Kamishana wa Magereza kuwalinda wasipewe adhabu ya kunyimwa kifungo cha nje na Parole kwa kuwa maofisa magereza wanawaandama na kuwasakama kuwa kwanini walitoboa siri nakuwa katika majalada yao watawaandikia wana tabia mbaya gerezani wasitoke kama njia ya kuwakomboa.

Bw. Nanyaro alisema amesikitishwa na taarifa za wafungwa kuna? baadhi ya wakuu wa magereza hapa nchini wanaowakodisha wafungwa na kwenda kulima katika mashamba ya matajiri na viongozi huku wakijua wazi vitendo hivyo ni kinyume cha taratibu za magereza.

Baadhi ya maofisa magereza waliozungumza na PST walisema, Kamishna Nanyaro ameahidi kuchukua hatua kali dhidi ya wakuu wa magereza na viongozi wa gereza hilo kama watabainika kuwa walikuwa wakiwakodisha wafungwa kwa wazungu wa mashamba ya maua na wananchi ikiwemo mashamba yao.
 
Huu mbona ni ufisadi huko magerezani tulisha piga kelele sana hata hapa lakini kwa vile mfungwa anakuwa amesha poteza haki zake za msingi watu wananyamaza tu hawashupalii na kushikia bango....kutoroka kwa mfungwa hujo wa miaka 30 ni dili tu wamecheza na maofisa wa gereza navyo jua mfungwa anaye hukumiwa kifungo cha miaka mingi iwa hawatoki mbali na gereza na ulinzi wao iwa unakuwa mkubwa sana.Kutoroka kwa huyu ni dili limechezwa si bure kwa nini walimpeleka kufanya kazi mbali na gereza???
 
HUYU KAMISHNA NANYARO AACHE UNAFIKI MBONA HUKU DAR WANAMSAIDI a\
MASHAMBANI MWAKE NA PI ANAWAPELEKA KWENYE MASHAMBA YA WAKUBWA ...TATIZO HAWA WAFUNGWA WASHAFANYWA MAHOUSIGELI JAMANI NA SI KUWAFUNZA TENA NENDA PALE GEREZANI UKONGA UONE WALIVYOTANWANYWA KWENYE VYUMBA VYA WAKUBWA

HAYA MAMBO NASHUKURU KWA KUYAWEKA BAYANA WENGINE WANINGIZWA VYOONI KWA WAKUUBWA WA MAGEREZA KUSAFISHA MAVI YAO HAYA MAMBIO SI UUNGWANA NAUNAFIKI ACHA MZEE NYARO FANYIA KAZI NA SI KULAUMU VITU UNAVYOVIJUA HATA KABLA UJACHAGULIWA HAO NI BINADAMU KUMBUKA MNAVYOWATESA KUNA AMBAO WAMEINGIA PASIPO NA HATIA DAMU ZAO ZITAKURUDIA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom