Mfungwa akutwa na jinsia mbili - TUJADILI, TUTAFAKARI, TUCHUKUE HATUA

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Mfungwa akutwa na jinsia mbili

Na Stella Ibengwe, Shinyanga (Tanzania Daima)

MFUNGWA mmoja kutoka gereza la Malya wilayanyi Maswa mkoani Shinyanga amebainika kuwa na jinsia mbili huku zote zikifanya kazi.

Hali hiyo imeulazimu uongozi wa gereza hilo kumpa uangalizi wa karibu wakati taratibu za kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili kufanyiwa upasuaji zikiendelea ili kumuondolea jinsia moja.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Afisa Magereza Mkoa wa Shinyanga, Elika Pesha, alisema mfungwa huyo aliyefungwa kifungo cha miaka thelathini alipelekwa katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam baada ya kuonekana kuwa na jinsia mbili.

Pesha alisema tayari taratibu za kumpeleka mfungwa huyo Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam kufanyiwa upasuaji baada ya kupata ushauri kutoka kwa madaktari zimeshakamilika.

Kabla ya upasuaji, mfungwa atapaswa kuchagua ni jinsia gani ifanyiwe upasuaji licha ya wataalam mbali mbali kumshauri abaki na jinsia ya kiume kutokana na kuwa na maumbile yanayoonesha kuwa ni mwanaume.

“Ni kweli huyo mfungwa yupo kwenye gereza la Malya na ana jinsia mbili zote zinafanya kazi na baada ya kugundua hali hiyo tumemuwekea uangalizi wa karibu katika chumba maalum kutokana na utata alionao,” alisema Afisa Magereza.

Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, Issa Magori, aliyesikiliza kesi ya mfungwa huyo na kuitolea hukumu, alisema mwaka 2007 alifikishwa katika mahakama hiyo akituhumiwa kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha akiwa na wenzake watatu kwa kuvamia ofisi ya mfanyabiashara mmoja inayojihusisha na ununuzi wa almasi na kubiba mizani, simu mbili pamoja na mashine ya utambuzi wa madini hayo.

Hakimu Magori alisema kwa kosa hilo, mhusika huyo na wenzake alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela lakini kabla ya kupelekwa gerezani walikaguliwa ndipo ilipogundulika kuwa mfungwa huyo ana jinsia mbili na zote zinafanya kazi ikiwa ni pamoja na kupata hedhi kila mwezi kama walivyo wanawake.

Hakimu Magori alisema tangu aanze kazi hiyo hajawahi kutoa hukumu kwa mtu ambaye ana jinsia mbili na zote zinafanya kazi.

Hata hivyo, alikumbusha kuwa tukio kama hilo lilishawahi kutokea mkoani Kagera ambapo mtu mmoja alikutwa na jinsia mbili lakini katika hizo moja ndiyo ilikuwa ikifanya kazi.




Maoni yangu:


Kwanza huu ni UHUNI! Nauliza, ni kwa Sheria gani Serikali inajipa mamlaka ya kumuondolea binadam huyu jinsia moja, ati kwa kuwa ana muonekano wa kuwa mwanaume? Ina maana, Mungu alikosea kumuumba akiwa na jinsia mbili? Je, kama ...asingefanya uhalifu na kukamatwa, Serikali ingetambua lini kwamba ana jinsia mbili zote zikiwa zinafanya kazi? Kwani, kuwa na jinsia mbili kuna "utata" gani? Ni LINI sisi tulipewa haki na mamlaka na Mwenyezi Mungu kuamua nani awe mwanaume na nani awe mwanamke? Madaktari wanapomshauri kwamba aondolewe jinsia ya kike, ina maana, kuwa mwanamke ni KOSA au ni UTATA?

THIS IS TOO MUCH! Wananchi TUPINGE ubabe huu kwa nguvu zetu zote! Ikiwezekane, tufanye maandamano, siku ambapo mfungwa huyo atakapopelekwa Muhimbili, ili tuoneshe kwamba tumechukizwa na ubabe huu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadam!

SERIKALI HAINA MAMLAKA WALA SHERIA ya kuamua nani awe na jinsia gani! Ameumbwa kama alivyo, na kama isingekuwa kufanya uhalifu, asingejulikana na angeishi hivyo mpaka kufa kwake.

Mbona wapo watu wenye muonekano wa kuwa wanawake, lakini wana jinsia mbili, na zote zinafanya kazi, na hawajulikani, na hawajakamatwa ili WAONDOLEWE jinsia moja? Ina maana, sasa Serikali itajitwalia mamlaka ya kuwatafuta watu wote wenye jinsia mbili ili kuwaondolea jinsia moja kuondoa UTATA? Utata gani? Mungu anakosea kutuumba kwa alivyotuumba? Kwa kweli NIMEKERWA na hali hii! Nitaipinga kwa kila hali!

Tukikaa kimya, Serikali itakuwa imejitwalia haki, kama ilivyojitwalia haki ya KUUA, kazi ambayo ni ya Mungu, na tutashindwa kabisa kupinga hapo baadaye! Kisheria inaitwa "precedence". Ukinyamaza, ina maana umekubali. Fikiria, kama ni nduguyo anayefanyiwa hivyo, utajisikiaje? Ati ameambiwa anapaswa kuchagua ni jinsia gani atabakia nayo!

HUU NI UFISADI! TUUPINGE JAMANI!
 
hivi tume ya haki za binadamu ipo na wanaharakati au wanasubiri afanyiwe operation ndiyo wakemee , kimsingi operation hii ni ya kulazimishwa angekuwa anapenda angeshafanyiwa siku za nyuma naamini ni beyond 18
 
Ushamba huu!kuwa na jinsia mbili is common na anatakiwa afungwe kwenye gereza lake/chumba chake.period!

It is inhuman beyond words kumfanyia operation ya kulazimishwa.

By the way, nani kawaambia zote mbili zinafanya kazi?? mfungwa mwenyewe?
 
Nafikiria - kinadharia huyu anaweza kuingia katika Guinness book of records akikubali kushika mimba kwa mbegu zake mwenyewe (japo kwa artificial insemination).
 
Ushamba huu!kuwa na jinsia mbili is common na anatakiwa afungwe kwenye gereza lake/chumba chake.period!

It is inhuman beyond words kumfanyia operation ya kulazimishwa.

By the way, nani kawaambia zote mbili zinafanya kazi?? mfungwa mwenyewe?


Kwa mujibu wa uchunguzi wa madaktari wa Bugando, mfungwa huyo anapata hedhi kila mwezi kama ilivyo kwa wanawake. Nadhani hukusoma hiyo article vizuri ukaielewa.
 
Nafikiria - kinadharia huyu anaweza kuingia katika Guinness book of records akikubali kushika mimba kwa mbegu zake mwenyewe (japo kwa artificial insemination).

mmh! siyo ataongeza tena kama yeye! you never know issue za kibailojia unaweza kukuta akaleta mwenye jinsia moja ila zime double! yaani kama me-zinakuwa mbili, na ke-zinakuwa mbili!!
 
How do you know that jinsia zote mbili zinafanya kazi? Wamejuaje? Hili swala la kumfanyia opereshini ni kama vile kumlazimisha bila matakwa yake yeye mwenyewe its in human
 
Wamwache kabisa na wasiziondoe, huyu jamaa kimsingi hawezi kuhangaika kutafuta "mwenza" yeye ni Self service kwa raha zake.:kev::violin::preggers:
 
Jamaa anatia huruma, lakini kama alikuwa jambazi sugu la kiume acha afanyiwe upasuaji abakie njemba. Kesi yake ni kama ya Caster Semenya wa SA. Yeye kabakia mwanamke.

Ila wanamtorture psychologically.
 
Cha msingi huyo mfungwa agome ku sign form ya kufanyiwa operesheni serikali kama ina ubavu isign on his/her behalf
 
Kwani sheria imekiukwa wapi? Kiutaratibu anatakiwa afanyiwe counseling na watu wa afya ambapo ye mwenyewe ataamua kama anakubali afanyiwe upasuaji. Akikubali anachagua jinsia aitakayo na kuweka sasahihi ambayo itaonyesha consent yake ye kufanyiwa operation. Hapa serikali isaidiacho kwa kuwa yeye ni mfungwa atafanyiwa upasuaji bure na serikali ya Tanzania. Naomba mchunguze vizuri mtakuta hayo ndo yaliyofanyika.
 
Kwani sheria imekiukwa wapi? Kiutaratibu anatakiwa afanyiwe counseling na watu wa afya ambapo ye mwenyewe ataamua kama anakubali afanyiwe upasuaji. Akikubali anachagua jinsia aitakayo na kuweka sasahihi ambayo itaonyesha consent yake ye kufanyiwa operation. Hapa serikali isaidiacho kwa kuwa yeye ni mfungwa atafanyiwa upasuaji bure na serikali ya Tanzania. Naomba mchunguze vizuri mtakuta hayo ndo yaliyofanyika.

Tumia akili kaka! Afanyiwe counselling, kwani ni MGONJWA? Umemsikia akilalamika? Kama ameishi miaka yote hiyo bila kusababisha madhara kwa yeyote, na uhalifu umetokana na hali yake duni ya kimaskini, kama angekuwa anaishi maisha mazuri, wala isingekuwa rahisi kumtambua kwamba ana jinsia mbili.

"Kosa" lake ni kukamatwa na kukutwa na jinsia mbili, kisha Serikali kuamua kwamba HAPASWI kuwa na hali hiyo! Kwa MAMLAKA YA NANI?

Tunamkufuru Mungu bila kujijua! Ameumbwa hivyo. Sisi binadam (wala sio mitume) tunajiamulia mambo OVYOOOOOOOOOOOOO!

Mwenyezi Mungu ameamrisha: USIUE!

Serikali inasema: Naua!

Tumekaa kimya!

Na hili pia, la kuamua mtu awe na JINSIA gani, tukae kimya pia?

Huu utakuwa ni UHAYAWANI WA KUVUKA MIPAKA!
 
Wamwache kabisa na wasiziondoe, huyu jamaa kimsingi hawezi kuhangaika kutafuta "mwenza" yeye ni Self service kwa raha zake.:kev::violin::preggers:

Hapo penye blue - nadhani ni Physically impossible
 
Huu ni uonevu usio kipimo. Kwanza inatakiwa mambo haya yawe siri siyo kuwaambia watu hadharani hivi, yeye aliweza kufanya siri na wazazi wake kwa muda wote huo, iweje leo mtu baki anautangazia umma!... Watu wa namna hii wako wengi tuu hapa duniani na Tanzania. Watu hawa kitaalamu wanaitwa hermaphrodite, wala si ajabu kama inavyotangazwa, sasa sijui watapita kila nyumba na kuwasaka hao wengine?. Yaani hapa serikali inafanya kama vile ni kosa yeye kuwa hivyo! Hii ni kuingilia uhuru wa mtu ambaye aliamua kukubali uumbaji aliofanyiwa.
 
Ndio maana inabidi kuzaliwa hospitalini - hospitali nzuri kwani kwa kawaida watoto wote ufanyiwa uchunguzi kuangalia kama kuna matatizo yoyote na kuyafanyia kazi mapema. Hata mtoto akazaliwa nyumbani lazima apelekwe hospitalini. Yawezekana huyo jamaa alizaliwa nyumbani na hakupelekwa hospitalini kwa kuchunguza dosari na kuangalia afya yake.
 
Sio kitu cha kawaida kukuta mtu ana jinsi mbili na zote zinafanya kazi BTW hiyo jinsi ya kiume wamejuaje kama ipo active?
Lakini pia sidhani kama kuna kosa kufanyiwa ops kwani kama nilivyo elewa ni kuwa baada ya jamaa kugundulika ana jinsi 2 ndio walachunguza na kugundua kwamba zote zinafanyakazi na kilichofuatia ni kushauriwa afanyiwe ops naye amekubali ila swala la kwamba awe na jinsia gani ndio bado hajaamua.
Mimi nadhani kama kuna haja ya kupinga upuasuaji huo, kufanywe baada ya yeye kusema kwamba hataki kufanyiwa na sio sisi tuanze kushinikiza.
Mnaotaka kuonekana wanaharakati,tafuteni nafasi ya kuongea na mfungwa haraka sana na kujua ni nini msimamo wake kuhusu upasuaji na kama anataka upasuaji, aseme ni jinsi gani anaitaka.
MWISHO.
Napenda kujua kwamba kipindi akiwa mahabusu aliwekwa katika kundi la jinsi ipi maana tangu 2007 kesi ilipoanza naamini alikuwa mahabusu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom