MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 705
Mfungwa akutwa na jinsia mbili
Na Stella Ibengwe, Shinyanga (Tanzania Daima)
MFUNGWA mmoja kutoka gereza la Malya wilayanyi Maswa mkoani Shinyanga amebainika kuwa na jinsia mbili huku zote zikifanya kazi.
Hali hiyo imeulazimu uongozi wa gereza hilo kumpa uangalizi wa karibu wakati taratibu za kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili kufanyiwa upasuaji zikiendelea ili kumuondolea jinsia moja.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Afisa Magereza Mkoa wa Shinyanga, Elika Pesha, alisema mfungwa huyo aliyefungwa kifungo cha miaka thelathini alipelekwa katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam baada ya kuonekana kuwa na jinsia mbili.
Pesha alisema tayari taratibu za kumpeleka mfungwa huyo Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam kufanyiwa upasuaji baada ya kupata ushauri kutoka kwa madaktari zimeshakamilika.
Kabla ya upasuaji, mfungwa atapaswa kuchagua ni jinsia gani ifanyiwe upasuaji licha ya wataalam mbali mbali kumshauri abaki na jinsia ya kiume kutokana na kuwa na maumbile yanayoonesha kuwa ni mwanaume.
Ni kweli huyo mfungwa yupo kwenye gereza la Malya na ana jinsia mbili zote zinafanya kazi na baada ya kugundua hali hiyo tumemuwekea uangalizi wa karibu katika chumba maalum kutokana na utata alionao, alisema Afisa Magereza.
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, Issa Magori, aliyesikiliza kesi ya mfungwa huyo na kuitolea hukumu, alisema mwaka 2007 alifikishwa katika mahakama hiyo akituhumiwa kufanya unyanganyi wa kutumia silaha akiwa na wenzake watatu kwa kuvamia ofisi ya mfanyabiashara mmoja inayojihusisha na ununuzi wa almasi na kubiba mizani, simu mbili pamoja na mashine ya utambuzi wa madini hayo.
Hakimu Magori alisema kwa kosa hilo, mhusika huyo na wenzake alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela lakini kabla ya kupelekwa gerezani walikaguliwa ndipo ilipogundulika kuwa mfungwa huyo ana jinsia mbili na zote zinafanya kazi ikiwa ni pamoja na kupata hedhi kila mwezi kama walivyo wanawake.
Hakimu Magori alisema tangu aanze kazi hiyo hajawahi kutoa hukumu kwa mtu ambaye ana jinsia mbili na zote zinafanya kazi.
Hata hivyo, alikumbusha kuwa tukio kama hilo lilishawahi kutokea mkoani Kagera ambapo mtu mmoja alikutwa na jinsia mbili lakini katika hizo moja ndiyo ilikuwa ikifanya kazi.
Maoni yangu:
Kwanza huu ni UHUNI! Nauliza, ni kwa Sheria gani Serikali inajipa mamlaka ya kumuondolea binadam huyu jinsia moja, ati kwa kuwa ana muonekano wa kuwa mwanaume? Ina maana, Mungu alikosea kumuumba akiwa na jinsia mbili? Je, kama ...asingefanya uhalifu na kukamatwa, Serikali ingetambua lini kwamba ana jinsia mbili zote zikiwa zinafanya kazi? Kwani, kuwa na jinsia mbili kuna "utata" gani? Ni LINI sisi tulipewa haki na mamlaka na Mwenyezi Mungu kuamua nani awe mwanaume na nani awe mwanamke? Madaktari wanapomshauri kwamba aondolewe jinsia ya kike, ina maana, kuwa mwanamke ni KOSA au ni UTATA?
THIS IS TOO MUCH! Wananchi TUPINGE ubabe huu kwa nguvu zetu zote! Ikiwezekane, tufanye maandamano, siku ambapo mfungwa huyo atakapopelekwa Muhimbili, ili tuoneshe kwamba tumechukizwa na ubabe huu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadam!
SERIKALI HAINA MAMLAKA WALA SHERIA ya kuamua nani awe na jinsia gani! Ameumbwa kama alivyo, na kama isingekuwa kufanya uhalifu, asingejulikana na angeishi hivyo mpaka kufa kwake.
Mbona wapo watu wenye muonekano wa kuwa wanawake, lakini wana jinsia mbili, na zote zinafanya kazi, na hawajulikani, na hawajakamatwa ili WAONDOLEWE jinsia moja? Ina maana, sasa Serikali itajitwalia mamlaka ya kuwatafuta watu wote wenye jinsia mbili ili kuwaondolea jinsia moja kuondoa UTATA? Utata gani? Mungu anakosea kutuumba kwa alivyotuumba? Kwa kweli NIMEKERWA na hali hii! Nitaipinga kwa kila hali!
Tukikaa kimya, Serikali itakuwa imejitwalia haki, kama ilivyojitwalia haki ya KUUA, kazi ambayo ni ya Mungu, na tutashindwa kabisa kupinga hapo baadaye! Kisheria inaitwa "precedence". Ukinyamaza, ina maana umekubali. Fikiria, kama ni nduguyo anayefanyiwa hivyo, utajisikiaje? Ati ameambiwa anapaswa kuchagua ni jinsia gani atabakia nayo!
HUU NI UFISADI! TUUPINGE JAMANI!