Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,609
- 1,741
Suala la kuifuatilia Zanzibar na kutaka kuifananisha na mikoa ya Tanganyika lilimtokea puani Waziri Mkuu Pinda na hadi hii leo hatamani hata kulizungumza na hivyo hivyo lilimpelekea Raisi Kikwete kusema Zanzibar ni Nchi.
Leo hii Mheshimiwa Mbowe nae anataka kujivika koti la ukamandoo kuhoji Zanzibar na kama haitoshi eti atafikisha Bungeni ,salaam kutoka Zanzibar zinakutakia kila la kheri Mheshimiwa Mbowe kulifikisha suala hilo Bungeni.Na jikaze kisabuni katika kutaka kulivalia njuga maana kama Hamad hakukutosha basi utapata watakaokutosheleza na uhakika wa kutolizungumzia tena ndipo utakapokufikia wakati huo.Mbowe usifikiri unatishwa ,hapana ,furaha yao Wazenji suala hilo ukilifikisha huko.
Huyu Mbowe anaonekana hana uwezo na kufikiri kwake ni finyu na uwono wake ni mdogo na usomi wake ni wa papo kwa papo,hajui kuwa zanzibar ina baraza la kutunga sheria ? Hajui kuwa zanzibar kuna rais na mawaziri wake,pia ina mahakama kuu ? Hajui yakuwa zanzibar ni nchi inakatiba yake na ndio ilizaa tunda ambalo linaitwa Tanzania ?
Hivi hawa waTanganyika hawajui yakuwa katiba ya Tanzania ndio siku zote inayovunja katiba za nchi mbili ambazo ndio zimesababisha kuundwa katiba hiyo ya Tanzania ? Katiba ya Tanzania ilikuwa na mambo 10 tu ambayo tuliokubaliana nayo,lakini sasa kuna zaidi ya 40,hamuoni yakuwa mumevunja katiba ya zanzibar kwa sababu mulipo jaza viraka katika katiba hiyo hamukuishauri zanzibarkwa maana hayakuridhiwa na baraza la wawakilishi la Nchi ya Zanzibar ?
Ila mheshimiwa Mbowe usije ukaingia katika mtego huo kama unatumiwa sawa endelea.