Mfumuko wa Bei waongezeka na kufikia asilimia 4.8 mwezi Novemba

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
NBS 2.jpg

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epharaim Kwesigabo akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Novemba mwaka huu, kulia kwake ni Mtakwimu Bw. Muhidini Mtindo.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Novemba Mwaka 2016 umengezeka hadi kufikia asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.5 mwezi Oktoba 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Sensa na takwimu za kijamii kutoka Ofisi ya Takwimu Taifa(NBS) Dkt.Ephraim Kwesigabo alisema ongezko hilo linamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishi mwezi Novemba 2016 imeongezeka ikilinganisha na kasi ya upandaji ilivyokua kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2016.

Asema mfumuko wa Bei ya Vyakula kwa Mwezi Novemba 2016 umeongezeka hadi asilimi 6.4 kutoka asilimia 6.0 mwezi Oktoba 2016, na kwamba baadhi ya Bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na Mbogamboga kwa salimia (7.1.), Unga wa Mahidi(1.5%), Unga wa Ngano(2.4%), Unga wa Muhogo(1.7%), mtama (1.5%), dagaa wakavu(1.1%) pamoja na mchele (1.0%).

Aidha Dkt Kwesigabo aliongeza kuwa thamani ya uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 95 na senti 98 Mwezi Novemba 2016 ikilinganishwa na shilingi 95 na senti 86 ilivyokuwa mezi Oktoba 2015.

Chanzo:
harakatizajiji.blogspot.com
 
Kwa pesa ile ile sasa tunapata vitu vichache. Maana vyanzo vya pesa vimebana na matumizi yapo pale pale au yameongezeka maana tunafyatua watoto.
 
View attachment 444123
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epharaim Kwesigabo akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Novemba mwaka huu, kulia kwake ni Mtakwimu Bw. Muhidini Mtindo.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Novemba Mwaka 2016 umengezeka hadi kufikia asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.5 mwezi Oktoba 2016.

Akizungumza na waandishi wa g=habari mapema leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Sensa na takwimu za kijamii kutoka Ofisi ya Takwimu Taifa(NBS) Dkt.Ephraim Kwesigabo alisema ongezko hilo linamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishi mwezi Novemba 2016 imeongezeka ikilinganisha na kasi ya upandaji ilivyokua kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2016.

Asema mfumuko wa Bei ya Vyakula kwa Mwezi Novemba 2016 umeongezeka hadi asilimi 6.4 kutoka asilimia 6.0 mwezi Oktoba 2016, na kwamba baadhi ya Bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na Mbogamboga kwa salimia (7.1.), Unga wa Mahidi(1.5%), Unga wa Ngano(2.4%), Unga wa Muhogo(1.7%), mtama (1.5%), dagaa wakavu(1.1%) pamoja na mchele (1.0%).

Aidha Dkt Kwesigabo aliongeza kuwa thamani ya uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 95 na senti 98 Mwezi Novemba 2016 ikilinganishwa na shilingi 95 na senti 86 ilivyokuwa mezi Oktoba 2015.

Chanzo:
harakatizajiji.blogspot.com
Vitu vilishuka bei mkanadi uchumi unashuka watu hawana pesa mzunguko wa pesa umepungua.
Sasa swala la mfumuko wa bei naliunga mkono sababu opposite is true
 
Hivi huyu haogopi?ohooo godfather atam-mafuru.
2020 welcome soon
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom