Mfumuko wa bei ukiwa 7% na ukuaji wa uchumi 7%, nini tafsiri yake?

GIBRALY

Member
Mar 14, 2017
31
35
Wachumi mnisaidie tafadhari, eti kama uchumi unakuwa kwa 7% na mfumuko wa bei ni 7%, hii inamaana yeyote katika tafsiri za uchumi? [HASHTAG]#elimu[/HASHTAG] [HASHTAG]#education[/HASHTAG] [HASHTAG]#economics[/HASHTAG] #
 
Hiyo inaitwa 'dabal dabal singal', ni namna ya serikali kumtibu mtu kibyongo kwa kumnyoosha kwa mbao mbili...mgongo unanyooka lakini anakuwa keshakufa na hawakawii kukwambia tulikubaliana kumnyoosha mgongo na kamwe hatukuchukua dhamana ya maisha yake
 
Wachumi mnisaidie tafadhari, eti kama uchumi unakuwa kwa 7% na mfumuko wa bei ni 7%, hii inamaana yeyote katika tafsiri za uchumi? [HASHTAG]#elimu[/HASHTAG] [HASHTAG]#education[/HASHTAG] [HASHTAG]#economics[/HASHTAG] #
Jibu: Serikali haijui km umekula ama hujala Nakuja kwenye mada mfano familia yenu mko 7 wewe umebahatika kusoma na ukatoka kimaisha una miliki nyumba 3 na mgari benki una milioni 200 ndugu zako umewasaidi kidogo wao kule wana milioni 5 mahesabu yako hivi ml 200+5=205 hiyo ml205 gawa kwa 7 ni ml29285714.3 maana yake nikwamba hela ambazo zipo gawanya kwa idadi ya Watanzania unaweza kujikuta na wewe uko kwenye mgawo wa milioni 40 kwa mfano wewe huna na hutarajii kuzipata
 
Wachumi mnisaidie tafadhari, eti kama uchumi unakuwa kwa 7% na mfumuko wa bei ni 7%, hii inamaana yeyote katika tafsiri za uchumi? [HASHTAG]#elimu[/HASHTAG] [HASHTAG]#education[/HASHTAG] [HASHTAG]#economics[/HASHTAG] #
Uchumi kukua unamaanisha ongezeko katika uzalishaji wa bidhaa na huduma ndani la nchi (Zao lao taifa=GDP)

Mfumuko wa bei unamaanisha kuongezeka kwa gharama ya ununuzi wa bidhaa na huduma fulani.

Ukuaji wa uchumi unapokua kwa 7% inamaanisha kuna ongezeko la uzalishaji katika sekta zote kwa wastani wa 7%. Hiyo asilimia saba inapatikana kwa kulinganisha uzalishaji wa kipindi fulani huko nyuma na hivi sasa, hii inaweza kuwa mwezi, robo mwaka, nusu mwaka au mwaka mzima wa fedha. Ukitaka kupima ukuaji wa mwezi machi 2017 unaweza kutumia mwezi wowote ndani ya miezi 12 iliyopita. Hii ni kwasababu miezi mingi inatofautiana kwa namna fulani ya vipindi vya kibiashara (business cycles). Mfano sekta ya kilimo kuna vipindi vya mavuno,kuandaa mashamba nk, hivyo mwanatakimu ataangalia kipindi kipi kinafanana na mwezi wa machi 2017 tangu Machi 2016. Kwa ujumla tathimini ya ukuaji wa uchumi ni tatanishi sana kwa wale wasio na taaluma ya takwimu.

Upande wa mfumuko wa bei vinafanana karibu kila taaratibu za tathimini hapo juu za makadirio ya ukuaji wa uchumi. Lakini hapa mwanatakimu huangalia kupanda na kushuka kwa bei za bidhaa au huduma kundi fulani (basket of good or services) inaweza kuwa gharama za usafiri, nafaka au gharama za mawasiliano ya simu.

Angalizo: Taarifa za ukuaji wa uchumi na mfumuko wa bei ni tatanishi sana maana zinaangalia wastani wa sekta zote, hivyo kuna sekta zinaweza kudolola mfano sekta ya uvuvi inawaza kukua kwa 0.000001% lakini kwakua sekta ya madini imekua kwa 20% basi uchumi umekua kwa 10% (huu ni mfano kama nchi ina sekta mbili tu) hivyo basi sekta nyingi zinaweza kuzorota lakini chache zikafanya vizuri, mwisho wastani utaonyesha uchumi umekua kwa ujumla.

Katika suala la mfumuko wa bei, hapa pia sekta zinatofautiana pia zinaathiliwa sana na bei za mafuta kutoka nje. Bei ya mafuta ikipanda kuna uwezekano mkubwa sana bei zikapanda pia maana gharama za usafirishaji wa bidhaa zitaongezeka. Sio mafuta pekee yanayochangia mfumuko wa bei, kuna sababu kama uhaba wa nafaka kama ilivyo sasa pamoja na kupanda kwa riba za mikopo.

Asante.
 
Mkuu hapo kunakitu tunaita Nominal na real growth..
Chochote ukisikia kinakuwa ni real or actual growth kwa maana kwamba tunatafuta ukuaji bila kuingiza madhara ya mfumuko wa bei.. Mfano mdogo
Chukulia tu sisi tunazalisha mihogo (watz), vipindi viwili 2015 na 2016. Mwaka 2015 tumezalisha tan 1 na bei ni tsh 1 per tan pato la taia litakuwa 1×1=1 na 2016 tumezalisha tan 2 na bei ni tsh 2, pata la taifa ni 2×2=4.
Hesabu
Nominal growth=4-1)/1
Actual growth=2-1)/1
Somo n kuwa unaposema uchumi umekuwa inamaana tumeongeza uzalishaji wa mihogo not otherwise
 
Back
Top Bottom