Malalamiko ya mfumoko wa bei yamekuwa makubwa.
Kuanzia bei ya chakula, vipuri, mafuta, vifaa vya ujenzi nk.
Hii ni hali halisi sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania. Takwimu zinazotolewa na TBS zinaonesha kuwapo na ongezeko la bei za vitu mbalimbali. Hali hii ipo pia nchi nyingine kama Marekani ambapo mwezi Oktoba 2021 walirekodi mfumuko wa bei mkubwa sana ambao haujawahi kutokea kwa miongo kadhaa. Nchini Uingereza pia na nchi nyingine za Kiafrika.
Sababu kubwa ni ipi;
1. Katika kipindi cha Korona uzalishaji ulipungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya lockdown zilizokuwepo. Kwa hivyo baada ya muda athari yake ndio inaanza kujitokeza ambapo mahitaji yamekuwa makubwa kulinganisha na bidhaa zilizopo.
2. Kwa upande wa mafuta, kumekuwa na control kubwa sana ya kuzalisha mafuta yanayoenda kuuzwa kupitia OPEC na wazalishaji wengine. Matokeo yake, yanatengeneza uhitaji ambapo bei inapanda. Mfano hai ni pale Marekeni ilipoamua kuachia akiba yake ya mafuta ili kuweza kupambana na hizi nchi zinazozalisha mafuta kidogo. Pamoja na chagua hilo, hawakufanikiwa. Itakumbukwa kwamba huko nyuma mafuta yamewahi kuuzwa kwa NEGATIVE PRICE. Hii ilitokana na uzalishaji mkubwa.
3. Mikopo iliyotolewa kupitia mapambano dhidi ya UVIKO-19 pamoja na ile mingine, imeongeza mzunguko wa fedha. Maana fedha imekuwa nyingi na hatimaye madhara ndio haya.
Pamoja na sababu hizi zipo nyingine nyingi tu zinazoongeza bei ya bidhaa.
Hivi karibuni tumesikia Serikali ikitaka uchunguzi wa bidhaa kuadimika au hata kupanda bei. Ukweli mchungu ni kwamba, malighafi za bidhaa husika zimepanda bei, hivyo wazalishaji hawaoni faida tajwa.
Zipo njia kadhaa za kupambana na huku kupanda bei;
1. Kuruhusu ushindani kutoka kwa wazalishaji wengine hata nje ya nchi kama uzalishaji wetu utakuwa ni wa gharama kubwa. Lakini madhara ya hili, ni kufifia kwa viwanda vyetu na kuua uchumi wa viwanda. Hivyo ni vyema kuona kama wazalishaji watapewa motisha fulani ili angalau uzalishaji wao uwe wenye tija kwa wananchi na kupunguza mfumuko wa bei.
2. Kutazama sana sera zetu za kifedha kama tunaingiza sana fedha kwenye mzunguko.
3. Kuongeza uzalishaji na kupunguza utegemezi wa malighafi.
Pamoja na hivyo, tutegemee kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa miezi kadhaa mpaka pale uzalishaji duniani utakapoimarika.