Mfumuko wa bei kwa mwezi Februari wabaki asilimia 3 kama Januari huku vyakula vikishuka bei

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
MFUMUKO wa bei kwa mwezi Februari umebaki kuwa asilimia tatu kama ilivyokuwa Januari mwaka huu, taarifa ya Ofi si ya Taifa ya Takwimu (NBS) imebainisha.

Akizungumza jana jijini hapa, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii wa NBS, Ephraem Kwesigabo alisema mfumuko huo umebaki sawa kama ulivyokuwa Januari kutokana na kuwapo kwa mabadiliko kidogo sana katika bei za huduma mbalimbali huku vyakula vikishuka bei.

“Hii inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Februari mwaka huu, imebaki sawa na kasi ya iliyokuwepo ya Januari mwaka huu,” alisema Kwesigabo. Alisema Mfumuko wa Bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi. Kwesigabo alifafanua hali hiyo imechangiwa na kupungua bei kwa baadhi za bidhaa za vyakula na bidhaa zisizokuwa za vyakula.

Alizitaja bidhaa za vyakula zilizopungua bei kuwa ni mchele (3.0%), unga wa mahindi (6.4%), mtama (5.1%) unga wa muhogo (6.9%), maharage (4.5%) na viazi vitamu vilivyoshuka bei kwa asilimia (8.2%).

Hata hivyo, alisema bidhaa zisizokuwa za vyakula ambazo bei zimepanda ni pamoja na mavazi (2.7%), mkaa (10.1%), majokofu (2.1%) na gharama za kumuona daktari kwenye hospitali binafsi kwa asilimia 4.6.

Pia Mkurugenzi huyo wa Takwimu za Sensa alisema mfumuko wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Februari mwaka huu, umepungua hadi asilimia 0.5 kutoka asilimia 0.7 ilivyokuwa Januari mwaka huu. Akizungumzia hali ya mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki, alisema Uganda mfumuko wa bei kwa Februari mwaka huu, umeongezeka asilimia 3.0 kutoka 2.7, Kenya umepungua hadi asilimia 4.14 kutoka asilimia 4.70 kwa mwaka ulioishia Januari mwaka huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unga wa mahindi umepungua asilimia 6.4 hivyo kama mangi mwezi wa kwanza alikuwa anauza. 900 sasa anatakiwa kuuza 840.24 mmoja wapo kati ya mangi au mama watoto ananiibia mbona bado nalipa 900?
 
Ni lini hao NBS wamewahi kutoa takwimu za mfumuko wa bei kupanda ??

#PoliticallyMotivatedTakwimu.
 
unga wa mahindi umepungua asilimia 6.4 hivyo kama mangi mwezi wa kwanza alikuwa anauza. 900 sasa anatakiwa kuuza 840.24 mmoja wapo kati ya mangi au mama watoto ananiibia mbona bado nalipa 900?
Henda wanachukua takwimu kutoka kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo. So kama Bakhresa alikuwa anauza mfuko elfu 60 na sasa kapunguza mpaka elfu 59, basi hizo ndizo data walizo nazo...
 
Henda wanachukua takwimu kutoka kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo. So kama Bakhresa alikuwa anauza mfuko elfu 60 na sasa kapunguza mpaka elfu 59, basi hizo ndizo data walizo nazo...
Wanachosema kimepungua ni marginal rate hiyo inamaana bei bado inaongezeka kwenye chain value ila hiyop MR inapungua kwakua tunakaribia mavuno.
 
Back
Top Bottom