Mfumuko wa bei huku mtaani unashamiri, kuna nini kinaendelea?

Salaamu watoto wa Jamhuri ya Muungano!

Kiukweli huku MTAANI vitu vinazidi kupanda bei siku Hadi siku.Nyama saizi 8000 Toka 7000. Juzi nimeenda dukani kununua Colgate naambiwa Sasa ni 5000/= ikiwa hapo awali nilikuwa nanuna 3500/.

Kwa ujumla vitu vingi bei vimepanda na sijaona tamko lolote kutoka mamlaka za serikali kuhusu hili. Je, Kuna inflation inapiga raia kimya kimya na serikali haitaki tamka rasmi?

Wataalamu naombeni uchambuzi ni ni kimesababisha Hali hii ghafla hivi.

sasa inflation inahitaji tangazo?
 
Ni hatari sana, na mimi ndo kipindi nilikuwa nafanya ujenzi nondo ilikuwa around elf 18, sementi ya dangote elf 11 material ya finishing ndo hayakamatiki kwa sasa, ngoja niendelee kujikongoja kwenye gofu langu ilimradi umejikinga na mvua na jua.......hapa sasa nimetoka kununua gesi ule mtungi wa mihan nilionunua mara ya mwisho elf 43, leo nimetoa elf 50, tunaenda kutengeneza jangwa hivi karibuni maana watu ambao walikuwa wameanza kutumia gesi wanarudi kwenye mkaa kwa kasi ya 5G, na mimi ni mmoja wao...........
Hatari mzee, huko kwny finishing ndio balaa, gypsum board kwaajili ya partation zilikuwa zinauzwa 22,000/ pc Kamaka sasahv wanauza 35000/pc hii ni hatari.
 
Pesa ikimwagwa nyingi mtahani. Nilazima hali kama hiyo itokehe mfumuko wa bei
Kwa maana pesa sasa inamilikiwa na wananchi.
 
Hayo ndo madhara ya rais kufariki akiwa madarakani, nchi inakosa uthibiti kabisa.......tunaposema mchakato wa katiba mpya uanze ni pamoja a kuweka sawa mambo kama haya ya succession plan.
Hata katiba ya sasa ina succession plan. Unaongea porojo za kichadema ambazo hazina kichwa wala miguu kwenye issue ya uchumi.
 
Salaamu watoto wa Jamhuri ya Muungano!

Kiukweli huku MTAANI vitu vinazidi kupanda bei siku Hadi siku.Nyama saizi 8000 Toka 7000. Juzi nimeenda dukani kununua Colgate naambiwa Sasa ni 5000/= ikiwa hapo awali nilikuwa nanuna 3500/.

Kwa ujumla vitu vingi bei vimepanda na sijaona tamko lolote kutoka mamlaka za serikali kuhusu hili. Je, Kuna inflation inapiga raia kimya kimya na serikali haitaki tamka rasmi?

Wataalamu naombeni uchambuzi ni ni kimesababisha Hali hii ghafla hivi.
Mafuta ya kupikia je?
 
Hata katiba ya sasa ina succession plan. Unaongea porojo za kichadema ambazo hazina kichwa wala miguu kwenye issue ya uchumi.
Kama kuna succession plan ile power struggle iliyouwa inafanyika nyuma ya pazia kipindi rais alipokuwa amezidiwa hadi tukawa tunadanganywa kwamba rais ni mzima wa afya anachapa kazi ni kitu gani. Succession plan inayoleta mantiki ni kwa spika wa bunge au jaji mkuu kukaimu madaraka ya rais na kuitisha uchaguzi ndani ya miezi sita, vinginevyo ndo tunabaki kushuhudia nchi inakosa uthibiti kila mmoja anajiona kambale. Na hii inatoa mwanya kwa makundi yenye maslahi binafsi kum blackmail rais anayerithi madaraka kana kwamba ndo yamehusika na yeye kupewa mamlaka na kuanza kumyumbisha, tujaribu kuwa realistic......​
 
Hayo ndo madhara ya rais kufariki akiwa madarakani, nchi inakosa uthibiti kabisa.......tunaposema mchakato wa katiba mpya uanze ni pamoja a kuweka sawa mambo kama haya ya succession plan.

Haiingii akilini mtu ambaye hachaguliwa kwa kura kwenye nafasi kubwa kama ya rais asimikwe kwenye nafasi hiyo kwa miaka zaidi ya minne.

Kwa uelewa wangu madaraka ya rais hayawezi kukaimiwa kwa zadi ya miezi sita kabla ya kufanya uchaguzi upya.
Katika eneo hilo la kukaimu,watawala wajue katiba ina changamoto,mimi nilitaka baada ya miezi sita uchaguzi uitushwe.
 
Hata deflation humgusa kila mtu.

Usililie deflation ni mbaya sana ndugu yangu, ni ujamaa ule wa kuleta umaskini. Unatakiwa kuchakarika kuikimbiza thamani ya pesa, ongeza uzalishaji wako.

Sikia mtaani pesa ikiwa nyingiiii hakuna bidhaa hiyo ni inflation mbaya sana. Hivyo hivyo kukiwa na bidhaa kila sehemu ila pesa hakuna ni mbaya sana. Pengine mbaya zaidi.

Inatakiwa inflation inavyoongezeka raia wachakarike na uzalishaji ili iwe sawa na uzalishaji na thamani ya pesa nje ya nchi ipande huku serikali ikihakikisha money supply haizidi uzalishaji. Mnakutana kwenye equlibrium.

Mfano , dola moja ss kwetu ni elfu mbili na ushee, ila parachichi unalonunua hapa mia tano marekani atalinunua dola mpaka mia almost laki mbili na ushee. Hiyo ni inflation kwao lakini isiyo na madhara kwenye uchumi wao bali faida.
Duuh! Acha uwongo ndugu yangu! Marekani ukienda n dollar 100 unanunua mazaga ya week nzima sasa hii ya parachichi la dollar 100 umenunua wapi?
 
fikiri kama mtu mwenye elimu hata unaweza hata kutumia internet. Sera hiyo ilikuwa ya hovyo sana na ilidumaza maisha ya wakulima ambao ni zaidi ya 70% ya watanzania wote. Ilikuwa sera ya hovyo iliyoasisiwa pasipo kufanyiwa utafiti
Ulitaka tufe njaa..unauwezo kununua mchele kilo kwa elfu 5..au unaropoka tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom