Mfumo wa utoaji matokeo ya mitihani ubadilike, huu wa sasa unashawishi udanganyifu

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
9,025
2,000
Hili ni suala la kisera linalohitaji utashi wa kisiasa. Kwa matokeo ya darasa la saba kwa mfano, kinachotakiwa ni alama na grade kwa kila mtoto maana ndicho kigezo kinachotakiwa ili mtoto aweze kuendelea na masomo au la na ndicho kipimo cha ufaulu wa mtoto.

Kuhusu shule kupangwa ipi ya kwanza hadi ya mwisho hapo ndipo panaposhawishi udanganyifu ili shule ionekane juu na kuvutia wazazi.

Hakuna sababu ya kuzipanga shule maana madhara kwa Taifa ya kuzipanga shule ni mabaya zaidi kuliko tija yake. Badala yake grade ya wastani wa shule ndiyo itajwe badala ya wastani wa marks/alama. Waziri wa elimu tafadhari tafakari hilo.

Nawasilisha.
 
zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
4,600
2,000
Umeongea Ponti sana.

Kuweka orodha ya Shule 10 Bora zilizo fanya vizuri ni kuchochea udanganyifu zaidi.

Baraza letu la mitihani linapaswa libadilike.
 
Gangaboe

Member
Jun 26, 2021
13
45
Mimi naona wako sawa tu kwa sababu zifuatazo.
1.Hiyo ni kama motisha kwa shule zilizofanya vizuri,pia na shule zilizo kwenye kumi mbovu ni kama adhabu kwao,inasaidia kuja na mbinu mbadala kama vile makambi ya madarasa ya mitihani ,hiyo inachangia kufanya vizuri.
2.Usimamizi ,ulinzi na usalama wa wenye mtihani mpaka utoaji wa matokeo hauruhusu mwanya wa rushwa hata kidogo.
=> Nashauri kuaminiwa kwa baraza ,na zaidi tuendelee kuwapa namana na mbinu za kuboresha usiri wa mchakato mzima wa uandaaji mpaka utolewaji wa vyeti.
 
Uhalisia ni kwamba shule zinafanya sana udanganyifu ili kupata sifa na ku utia wazazi. Udanganyifu una hasara kubwa sana kwa Taifa. Kuna shule hufanya sana udanganyifu lakini kichocheo chake ni kutaka kuwa kumi bora. Lakini wakisema labda shule X ina wastani wa A, ni shule nyingi tu zina zinz A, kwa hiyo athari yake ni ndogo. Kama ni mwongozo kwa wazazi huo wastani wa grade bado ni mwongozo tosha.
 
Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
3,004

Mkuu kama mdau ebu taja hiyo/zo shule zifanyazo udanganyifu ili ziweze kuwajibishwa
 
mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
9,025
2,000
Mkuu kama mdau ebu taja hiyo/zo shule zifanyazo udanganyifu ili ziweze kuwajibishwa
Hivi wewe unaishi Tanzania au unaishi wapi? Hakuna mwaka ambao wakati wa kutoa matokeo hatukuambiwa juu ya wanafunzi waliofutiwa matokeo kwa udanganyivu. Mara kwa mara shule kadhaa huwa zinafutiwa kuwa kituo cha mitihani kwa ajili ya udanganyifu. Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo huwepo kila mwaka ndio nimekuja na mawazo ya kubadili utaratjbu wa kutoa matokeo. Hakuna upungufu wowote kama Taifa kama utaratibu wa kuzipanga shule toka ya kwanza hadi ya mwisho. Hiyo haibadili wastani wa grade ya shule wala haimpunguzii mwanafunzi ufaulu wake. Ila itaondoa kabisa kichocheo cha udanganyifu kwenye mitihani.
 
Artificial intelligence

JF-Expert Member
Jan 28, 2021
716
1,000
Hili ni suala la kisera linalohitaji utashi wa kisiasa. Kwa matokeo ya darasa la saba kwa mfano, kinachotakiwa ni alama na grade kwa kila mtoto maana ndicho kigezo kinachotakiwa ili mtoto aweze kuendelea na masomo au la na ndicho kipimo cha ufaulu wa mtoto.
Kuhusu shule kupangwa ipi ya kwanza hadi ya mwisho hapo ndipo panaposhawishi udanganyifu ili shule ionekane juu na kuvutia wazazi.
Hakuna sababu ya kuzipanga shule maana madhara kwa Taifa ya kuzipanga shule ni mabaya zaidi kuliko tija yake. Badala yake grade ya wastani wa shule ndiyo itajwe badala ya wastani wa marks/alama. Waziri wa elimu tafadhari tafakari hilo.
Nawasilisha.
Kwa taarifa yako mitihani inaibwa kuanzia ngazi ya mkoa, kwahiyo kunusuru elimu ya Tanzania ni kubadili Sera ya elimu tu.
 
Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
3,004
2,000
Hivi wewe unaishi Tanzania au unaishi wapi? Hakuna mwaka ambao wakati wa kutoa matokeo hatukuambiwa juu ya wanafunzi waliofutiwa matokeo kwa udanganyivu. Mara kwa mara shule kadhaa huwa zinafutiwa kuwa kituo cha mitihani kwa ajili ya udanganyifu. Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo huwepo kila mwaka ndio nimekuja na mawazo ya kubadili utaratjbu wa kutoa matokeo. Hakuna upungufu wowote kama Taifa kama utaratibu wa kuzipanga shule toka ya kwanza hadi ya mwisho. Hiyo haibadili wastani wa grade ya shule wala haimpunguzii mwanafunzi ufaulu wake. Ila itaondoa kabisa kichocheo cha udanganyifu kwenye mitihani.
Mada yako unasema kuna shule zinafanya udanganyifu na kupata matokeo mazuri...Kwakua mimi ni mdau wa Elimu niliomba ututajie hizo shule ili tuwajibike.
Kutokea udanganyifu kwa shule au mwanafunzi kupo ila atuwezi tukafanya hitimisho kua shule zote zinazofanya vyema zinafanya udanganyifu mkuu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom