Mfumo wa utendaji kazi serekalini unahitaji mabadiliko makubwa

Sep 20, 2007
69
2
Pamoja na mabadiliko ya mawiziri ambayo tunayatarajia, pia mfumo wa utendaji kazi serekalini unahitaji mabadiliko makubwa.

Mpaka sasa mfumo wa utendaji kazi serikalini, kwa kiasi kikubwa umebakia ni ule uliorithiwa kutoka katika serikali ya kikoloni mwaka 1961. Mfumo huu umejaa usiri mkubwa usio wa lazima huku kila document ikipigwa chapa ya neno "CONFIDENTIAL" bila sababu za msingi. Pamoja na wimbo wa utawala bora amboa serikali imekuwa ikiuimba kila siku, mpaka kuanzisha wizara inayoshughulika utawala bora, hali imekuwa tofauti na dhana hiyo ambayo ina himiza UWAZI.

Pamoja na wizara kuwa na dira (Vision), mikakati (Strategic plan), sera (Policies) n.k lakini document hizo ambazo hugharimu fedha nyingi wakati wa uandaaji wake ikiwa ni pamoja na semina nyingi bagamoyo, mwisho wa siku huwekwa katika makabati na kuliwa na mende.

Kazi nyingi za wizara zimekuwa ni za zima moto, bila kufuata mipango zilizojiwekea, zikiambata na re-allocation za mafungu, kutoka kwenye kazi zilizopangiwa kwenda kwenye kazi ya zima moto. Mfano mzuri ni ziara ya mawaziri miezi michache iliyopita ambayo iligharimu zaidi ya Shs 100m, kazi ambayo haikuwepo kwenye mipango ya kazi ya wizara. Hali hii inasababisha kuto kusonga mbele ki maendeleo, kwani maafisa wengi huwa katika pilika pilika za kufanya kazi za zima moto na hivyo kutojipanga.

Muundo wa serekali umekuwa ni ule ule tangu miaka ya 70 pamoja na mabadiliko ya kitekinolojia, kiuchumi na kijamii ambayo yametokea katika miaka ya hivi karibuni, hivyo kuto kwenda na wakati. Muundo huu hauna tija kwani hata vyeo vingi vya serikali haviendani na majukumu mtu anayofanya, Vyeo kama Mchumi daraja I, Afisa ardhi daraja II, Afisa kilimo III n.k ambapo hukuta kama ni idara ya kilimo basi watu wote watakaojiriwa watakuwa ma afisa kilimo, halafu ndo hupangiwa kazi zingine za kufanya mfano kuchambua sera, kukusanya na kutunza takwimu, kupanga budget bila kuwa na taaluma stahili.

Pamoja na kwamba serikali ina watumishi wengi waliosoma vizuri, lakini mfumo wa sasa hauwaruhusu wataalam hao katika kutumia ujuzi wao kwa ufanisi. Mawaziri hujirundikia madaraka na kufanya maamuzi ambayo wakati mwingine huigharimu serikali hata kama wataalamu wanashauri vinginevyo.

Mimi naona hili ni tatizo kubwa, sijui wenzangu mnaonaje?
 
Pamoja na kwamba serikali ina watumishi wengi waliosoma vizuri, lakini mfumo wa sasa hauwaruhusu wataalam hao katika kutumia ujuzi wao kwa ufanisi. Mawaziri hujirundikia madaraka na kufanya maamuzi ambayo wakati mwingine huigharimu serikali hata kama wataalamu wanashauri vinginevyo.

Shukurani kwa kulileta hili ingawa nitatofautiana na wewe kidogo.

Tatizo nionavyo mimi ni kuwa hao wasomi na wanataaluma kushindwa kusimamia taaluma zao hata pale wanapoona waziri anakosea au anakiuka taratibu. Watendaji wameona kuwa kazi yao ni kuhalalisha vitendo vya wanasiasa badala ya kuwa washauri wao wakuu. Itakuwaje watendaji wazoefu kama Kazaura na Mgonja waogope kusimamia haki? Kama alivyouliza Mwakyembe & Co. itakuwaje Bodi ya Tanesco ibaki ikidunda baaada ya kudhalilishwa kiasi kile? Naamini kama wangefanya hivyo, hii Richmond isingefika mbali. Mawaziri wanajilundikia madaraka kwa sababu watendaji wanawaachia. Itakuwaje Katibu Mkuu ana'sign' mkataba anaojua ni bomu kwa vile ameagizwa na waziri? Wa kulaumiwa hapa nani? Waziri au Katibu Mkuu?

Kitu kinachojitokeza wazi katika kashfa hii ni umuhimu wa kuwa na watendaji walio huru. Watendaji wasio sehemu ya mfumo wa kisiasa na ambao wajibu wao ni kwa taifa letu tu na si kwingine. Kuna haja ya kuongeza utaalamu wa hao watendaji na uwezo wa kusimamia maamuzi yao. Watendaji wazawadiwe kwa utendaji na si loyalty kwa chama.

ulichosema juu ya kukithiri kwa siri ni kweli tupu. Mengi ya hayo yanayoitwa confidential hayana usiri wowote.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom